Mkuu
MTAZAMO , kwanza niendelee kukupongeza wewe ni miongoni mwa wana JF very objective.
Kuna viongozi wanasiasa wa aina tatu na sub groups mbili.
1. Born leaders who are (a) leaders (b) technocrats who are responsible to the people!.
2. Made leaders who are (a) leaders (b) technocrats who are responsible to those who made them!.
3. Self Made Leaders who are not leaders but technocrats, who are responsible only to themselves!.
1. Born leaders who are (a) leaders are responsible to the people, hawa ni wale viongozi wanasiasa waliozaliwa na kipaji cha uongozi kwa wito wa utumishi wa watu, hawa ni selfless leaders ambao kwao ni taifa kwanza, na wameutafuta uongozi kwa juhudi zao wenyewe binafsi kihalali bila kubwebwa na mtu au kutumia rushwa au ukwasi wao kununua uongozi, hivyo wanawajibika kwa watu, na hawawajibiki kulipa hisani kwa yeyote!. Hawa ni viongozi kama Nyerere, Karume Snr, Jumbe, Kawawa, Mkapa na wengine, they are born leaders, wameutafuta uongozi kwa juhudi zao binafsi bila kubwebwa na yeyote au kutumia rushwa, hivyo they were indebted to no one!, na wanaongoza kwa mifano.
Naomba kuliruka kundi la pili la
2. Made leaders who are (a) leaders (b) technocrats who are responsible to those who made them!, na kurukia kundi la
3. La Self Made Leaders who are not leaders but technocrats, who are responsible only to themselves!, kwenye kundi hili ndio kuna Magufuli, huyo ni self made leader ambaye hakuwa a politician but a technocrat ndio maana aliongoza kwa nyapara type na hakuwa indebted kulipa fadhila kwa yeyote ndio maana alitawala as if he own this country ni mali yake na anaweza kufanya lolote!.
Sasa nirudi kwa kundi la pili la
2. Made leaders who are (a) leaders (b) technocrats who are responsible to those who made them!. Kundi hili lina Mwinyi Snr, Karume Jnr, JK, Mwinyi Jnr na Samia. They are made leaders hivyo they are indebted kwa those who made them, ni watu wa shukrani!.
Ni kweli Samia ana nia ya dhati ya kuwania urais 2025 ila ana changamoto 2. Changamoto ya kwanza ni jee ni yeye aliyepangiwa na YEYE kwa 2025?.
Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye!
Changamoto ya pili ni hizi sauti,
Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke
Awamu ya hisani ni hii awamu ya kwanza pekee, Samia akiingia awamu ya pili, hii sasa itakuwa ni awamu yake ya self made leader, atakuwa hawajibiki kulipa fadhila kwa yeyote na hapo sasa ndio Tanzania na Watanzania tutamfaidi the real Samia ambaye ni huyu
Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!”
Let's put our fingers crossed ili 2025 awe Samia, Tanzania na Watanzania tumfaidi Rais Samia kikamilifu!
P