Baraza la Mitihani lakanusha Mtwara kushika nafasi ya mwisho matokeo kidato cha nne, yataka wananchi kupuuza taarifa hizo

Baraza la Mitihani lakanusha Mtwara kushika nafasi ya mwisho matokeo kidato cha nne, yataka wananchi kupuuza taarifa hizo

Haya matokeo ni ya 2016 siyo 2020. Wewe ni utopolo sana!
2016 ni hizi
dd2a1-matokeo22beyopa2bblog.jpg
 
haya matokeo yamepikwa kumfurahisha mkuu ionekane anafanya kazi ila ukweli hakuna kitu sema vile mkuu anapenda sifa anayafumbia macho tu
 
NECTA YAKANUSHA SHULE MTWARA KUBURUZA MKIA
-
Baraza la Mitihani nchini (NECTA) limekanusha taarifa za kuwa shule tisa kati ya kumi zilizoburuza mkia katika matokeo ya kidato cha nne ya mwaka jana zinatoka Mkoa wa Mtwara.
-
Taarifa iliyotolewa na Afisa Habari na Uhusiano wa baraza hilo, John Nchimbi imebainisha kuwa taarifa hizo zililenga kuuchafua mkoa huo na kuwaomba wananchi kuzipuuzia taarifa hizo.
-
“Baraza linapenda kuujulisha umma kuwa taarifa hizo ni za uongo na zinalenga kuupotosha umma, kuleta taharuki na kudhalilisha Mkoa wa Mtwara.” Amesema Nchimbi
-
Nchimbi amefikia kutoa kauli hiyo mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byakanwa mapema hii leo kulitaka baraza hilo kutoa ufanuzi juu ya taarifa hiyo.

Taarifa: habarileo_tz

Haya baada sasa ya Baraza la Mitihani Kutukanushia kwa Kutishwa na Uwoga hebu na huyu RC wa Mtwara akanushe kuwa huo Mkoa hauna Vilaza.
 
Mkuu unataka kusemaje ?

Naona kichwa cha habari na maelezo ya ndani havina ushirikiano.
 
Link hii haa ni matokeo ya SHULE YA SEKONDARI LUKOKODA inayosemwa na NECTA kuwa ni ya mwisho wakati kimkoa ni ya 27 kati ya 33 na kitaifa ni ya 737 kati ya 986 (kundi la shule zenye wanafunzi chini ya 40)


Madudu ya NECTA hyao.

MAENDELEO HAYANA VYAMA!
Tatizo sio necta,bali itakua hackers wameingiza hicho kipande cha shule 10 za mwisho mwisho..
Nekta wasilaumiwe kwa hili hata kidogo..
lt.jpg
 
Baraza waongo Sana.

Jana wamesema pia eti shule iliyoongoza kitaifa Ni PEACELAND ya MWANZA.

Wakati kiuhalisia shule iloongoza ni ST. FRANCIS GIRLS.

Baraza wanakurupuka Sana.
 
Baraza la mitihani nchini NECTA limekanusha taarifa zilizozagaa mitandaoni kwamba mkoa wa Mtwara umeshika nafasi ya mwisho matokeo ya kidato cha nne.

Necta imewataka wananchi kupuuza taarifa hiyo kuwa shule 9 kati ya 10 zilizoshika nafasi za mwisho (umbwigi) zinatoka mkoani Mtwara.

Source: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
Hii ni baada ya waziri mkuu kuwafokea kwani inautia aibu mkoa alikotoka
 
Nimeamua kufanya fact check ili kujiridhisha na hiyo orodha uliyoiweka hapo juu (iliyosambaa mitandaoni)...
Kama necta hawataji shule 10 na mkoa wa mwisho basi hizi hizi ndo tunaendelea kuzitambua kama za mwisho maana Hamna mbadala wake.
 
Nashindwa kuelewa mtu anadhalilikaje kuwa wa mwisho.

Kwenye mtihani lazima kuna wa kwanza na wa mwisho .

Sasa sijui walitegemea nani awe wa mwisho??

Au kuna watu hawapaswi kuwa wa mwisho??

Mambo ya ajabu kabisa haya kutokea duniani eti taasisi ya elimu inasimama kutetea mtahiniwa.

Sasa impartiality hapo itakuwepo kweli.

Credibility ya Necta ni questionable, kwa muktadha huo matokeo yote is a sham.
 
Nashindwa kuelewa mtu anadhalilikaje kuwa wa mwisho.

Kwenye mtihani lazima kuna wa kwanza na wa mwisho..
Kuwa wa mwisho hakuna shida kabisa, kwenye mtihani ni lazima wa mwisho awepo.

Tatizo ni pale inaposemwa kwamba wewe ni wa mwisho wakati wewe si wa mwisho.

Kwa muktadha wa matokeo ya 2016 orodha inayosambaa mitandaoni iko sahihi.

Kwa muktadha wa mwaka 2020 orodha hiyo ni potoshi.

Wewe unaipotezaje imani yako (credibility) kwa NECTA kwa jambo jepesi namna hii lililofafanuliwa.
Au unaamini kwamba NECTA ndio imetoa matokeo ya mwaka 2016 mnamo mwaka 2021 ?
 
Back
Top Bottom