Noti bandia
JF-Expert Member
- May 3, 2020
- 2,684
- 4,315
Mchawi ni muda tu. Tutajua mmekuja kama staili ya NEMC na kelele maeneo ya Bar au mpo siriaz.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Pia wapige marufuku wanawake kuvaa suruali, kwa utamaduni wa Kizanzibari na dini ya Kiislamu mwanamke anatakiwa avae buibui na si kuvaa suruali au gauni au sketi fupi.Serikali ya Zanzibar imesema ni kosa kisheria mwanaume kuingia au kuishi viziwani Zanzibar akiwa amesuka nywele.
''Kwa mujibu wa sheria zetu ukikutwa utatozwa faini ya milioni moja za kitanzania ambayo ni zaidi ya dola 400 za kimarekani au kufungwa jela miezi sita au adhabu zote kwa pamoja,” imeeleza Serikali ya Zanzibar.
Akizungumza na BBC, Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni Zanzibar, Dkt Omar Adam amesema serikali kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi imeanza operesheni ya kukamata wanaume wote waliosuka nywele ikiwa ni utekelezaji wa sheria inayokataza wanaume kusuka nywele ili kulinda maadili na tamaduni za Zanzibar.
Dkt Omar amesema vijana wengi visiwani humo wamekuwa na hulka ya kusuka nywele kinyume na taratibu za wazanzibar.
Alisema,” Sifahamu kama kuna mzee yoyote hapa Zanzibar ambaye atamchukua mwanae wa kiume halafu ampeleke saluni kusuka nywele. Huu si utamaduni wa Zanzibar na sisi kama wasimamia sheria lazima tuzuie hili.”
SOURCE: BBC SWAHILI
Dkt. Adamu anajisafisha nyoyo tu ukilitizama hili shauri kiundani utaona amekosa kufikiria kwa kutumia huo utamaduni anaotaka kuulinda. Ana tumia mila na desturi za kikoloni!Dkt.Omar Adam
Hiyo sheria ni kwa ajili ya zanzibar tuWengine kusuka ni utamaduni.
Sisi sio kabila moja, Ila ni taifa moja.
Tungekuwa wote ni kabila moja tunalounda taifa moja hiyo sheria ingefanya kazi
PhD aliipataje huyu? Au Ni daktari wa wanyama pori?Katibu Mtendaji Baraza la sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni, Dkt.Omar Adam leo kwenye Asubuhi Njema ya ZBC ameelezea mengi yanayohusu sekta ya sanaa, filamu na namna wanavyosimamia Mila, Desturi na Utamaduni wa Zanzibar.
Amesema "Moja ya kazi kubwa ya Baraza la sanaa Zanzibar ni kulinda Mila, Siha, desturi na Utamaduni wa Zanzibar, Baraza hili la sanaa pia lina minasaba na wananchi wote wa Zanzibar katika sekta ya filamu, sanaa na Utamaduni"
Ameongeza "Sisi kama Baraza hatufurahishwi kabisa na watu wanaoiga utamaduni wa nje ya Zanzibar kwasababu watu wengi wa nje wanakuja Zanzibar kujifunza kwasababu wanavutiwa na utamaduni, taratibu na desturi za Zanzibar"
Aidha, amebainisha "Askari wanakamata wanaume wote wanaosuka nywele kama za wasichana, Baraza la sanaa hatupendelei hilo na kuna kibali maalumu cha kusuka nywele ambacho ni milioni 1 na tumeweka bei hiyo ili kuwakomoa, sasa utachagua mwenyewe utoe milioni usuke au ununue kiwembe chako unyoe"
Akili za kijinga kabisa,unasema unalinda utamaduni wa zenj,lakini upo tayari kulipwa hera ili utamaduni uvunjwe!!wanaume walipie kibari cha kusuka!!Katibu Mtendaji Baraza la sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni, Dkt.Omar Adam leo kwenye Asubuhi Njema ya ZBC ameelezea mengi yanayohusu sekta ya sanaa, filamu na namna wanavyosimamia Mila, Desturi na Utamaduni wa Zanzibar.