Baraza la Sanaa Zanzibar: Wanaume Wanaosukwa kama Wanawake kukamatwa, faini ni Tsh. Milioni 1 au kifungo cha Miezi 6
Wakimaliza hapo waje kwa watoboa pua, wavaa hereni na vikuku.
 
Hawajaishia kwenye kusuka tuu, kwenye muziki wa ufukweni pia, kwa kifupi Islamic State of Zanzibar haitaki mambo ya music urembo na sanaa za kisasa
 
Katibu Mtendaji Baraza la sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni, Dkt.Omar Adam leo kwenye Asubuhi Njema ya ZBC ameelezea mengi yanayohusu sekta ya sanaa, filamu na namna wanavyosimamia Mila, Desturi na Utamaduni wa Zanzibar.
Mtoa mada umepotosha "HAKUNA KIBALI CHA KUSUKA" nimemsikia mimi mwenyewe muhusika akihojiwa BBC swahili. Bali kuna faini ya 1M kwa atakaekamatwa kasuka au jela 6Month
 
Sasa hapo Kuna uzuri gani?

"Kibari kusuka milioni, lengo kulinda utamaduni"

Ina maana Nikilipa milioni Kisha nikasuka huo utamaduni utakuwa umelindwa? Hapo walichofanya ni kwamba Zanzibar kusuka ni ruksa ila Kuna gharama kubwa.

Bla bla za kuprotect vijana wasijiingize kwenye mambo ya hovyo wangepiga marufuku Kama hivi "Zanzibar mtoto wa kiume kusuka hairuhusiwi" FULL STOP.
Hakuna kibali bali kuna faini tu
 
Mtoa mada umepotosha "HAKUNA KIBALI CHA KUSUKA" nimemsikia mimi mwenyewe muhusika akihojiwa BBC swahili. Bali kuna faini ya 1M kwa atakaekamatwa kasuka au jela 6Month


Habari ilikuwa:

Tittle: Mwanaume atakayesuka nywele Zanzibar, faini milioni 1, jela miezi sita

Body:
Serikali ya Zanzibar imesema ni kosa kisheria mwanaume kuingia au kuishi viziwani Zanzibar akiwa amesuka nywele.

''Kwa mujibu wa sheria zetu ukikutwa utatozwa faini ya milioni moja za kitanzania ambayo ni zaidi ya dola 400 za kimarekani au kufungwa jela miezi sita au adhabu zote kwa pamoja,” imeeleza Serikali ya Zanzibar.

Akizungumza na BBC, Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni Zanzibar, Dkt Omar Adam amesema serikali kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi imeanza operesheni ya kukamata wanaume wote waliosuka nywele ikiwa ni utekelezaji wa sheria inayokataza wanaume kusuka nywele ili kulinda maadili na tamaduni za Zanzibar.

Dkt Omar amesema vijana wengi visiwani humo wamekuwa na hulka ya kusuka nywele kinyume na taratibu za wazanzibar.

Alisema,” Sifahamu kama kuna mzee yoyote hapa Zanzibar ambaye atamchukua mwanae wa kiume halafu ampeleke saluni kusuka nywele. Huu si utamaduni wa Zanzibar na sisi kama wasimamia sheria lazima tuzuie hili.”
 
Hawa watu hawajui kama Dunia sasa ni kijiji kimoja?upuuzi wowote unafika duniani huko na wote tunaonekana hatuna akili,

Karne hii ni ya kufatilia nani kasuka, nani kavaa hereni, nani kachora tattoo kweli!!!

Umeme na maji hapo Znz ni shida, Elimu ni kichefu chefu, Umaskini kama wote leo unakamata vijana wanaosuka ambao hata 2% hawafiki!

Hii ni laana sio bure.
 
“ Ni kosa kisheria mwanaume kuingia au kuishi viziwani Zanzibar akiwa amesuka nywele"

Serikali ya Zanzibar imesema ni kosa kisheria mwanaume kuingia au kuishi viziwani Zanzibar akiwa amesuka nywele.

''Kwa mujibu wa sheria zetu ukikutwa utatozwa faini ya milioni moja za kitanzania ambayo ni zaidi ya dola 400 za kimarekani au kufungwa jela miezi sita au adhabu zote kwa pamoja,”
 
Amelaaniwa mwanaume ajifananishae na mwanamke na amelaaniwa mwanamke ajifananishae na mwanaume.
 
Hakuna kitu kama hicho, na nchi haiongozwi Kwa hisia za watu, hata kama hupendi wanaume wanaosuka huwezi kuamka tuu na kutoa tamko kwa sababu wewe ni kiongozi au serikali, Sheria zifuatwe tuache ujinga
 
Back
Top Bottom