Mkuu Dada
Sky Eclat , kwavile wana jf tuko wengi na hakuna awezaye kusoma makala za wana jf wote, mimi ni miongoni mwa tulio andika sana kuhusu uchaguzi mkuu wa 2020, tena wengi wameanza kuandika kuhusu uchaguzi huu, wakati wa mchakato wa uchaguzi, mimi nilianza kuandika kuhusu uchaguzi huu mwaka 2015 baada tuu ya uchaguzi Mkuu wa 2015, wakati wengine wote wakisubiri matokeo kwa hamu kubwa wakiamini EL atashinda, tarehe 28 October 2015 nilipandisha bandiko hili humu jf na nilisema kila kitu kuhusu uchaguzi wa 2020!
Wanabodi, Dr. John Pombe Joseph Magufuli ndiye mshindi wa urais Tanzania kwa mwaka huu wa 2015-2025 and may be more!, anayesubiri tuu kutangazwa rasmi na kuapishwa. Nimesema 2015 -2025 sio kwa bahati mbaya as if hakuna uchaguzi 2020, no!, nimesema 2015-2025 kwa sababu huu ndio ukweli...
Baada ya JPM kuingia madarakani na kasi yake, November 2015 nikapanda tena
Wanabodi. Kwa Kasi Hii ya Rais Wetu Mpendwa, Dr. John Pombe Joseph Magufuli na Falsafa yake ya "Hapa Kazi Tu", na kama hiki tunachokiona sasa, sio nguvu ya soda tuu, yaani ataendelea kwa kasi hii hii hadi 2020, kuna haja kweli ya kufanya tena uchaguzi wa rais?. Kwa maoni yangu, uchaguzi wa...
Kwa miaka yote mitano nimekuwa nikiendesha darasa la bure kuhusu 2020
Wanabodi, Hili ni bandiko la swali, kwa uchaguzi wa 2020, kwa mujibu wa utaratibu wao CCM, tayari tunaye mgombea wa urais ni Dr. John Pombe Joseph Magufuli. Swali la kujiuliza kwa huu upinzani uliopo Tanzania kwa sasa, jee kwa uchaguzi wa 2020 mgombea wa CCM, Dr. John Pombe Joseph Magufuli ana...
Wanabodi, Hili ni bandiko la swali dogo tuu kuwa uchaguzi wa 2015 tulikuwa na chaguo, jee uchaguzi wa 2020 tutakuwa na chaguo?. Declaration of Interest: Mimi Pascal Mayalla ni mshirika mkubwa wa "Joni Mtembezi Lebo Nyeusi" na ninapoandika hapa, tayari niko under the influence of Joni Mtembezi...
Wanabodi, Kipenga cha kuanza kwa kampeni za Uchanguzi Mkuu ujao kimepulizwa leo na fungua dimba amekuwa Chadema. Nimeangalia kidogo kupitia live ya TBC, kiukweli nilichoshuhudia, ndicho kimenipelekea mimi kuanzisha huu uzi ambao ni swali. Je, Tanzania tuna upinzani wa kweli, upinzani makini...
Hata ugombea wa Tundu Lissu, mimi nimeshiriki kumchagiza, kabla za zile pyu pyu za Dodoma
Wanabodi, Hili ni bandiko la swali tuu, Ili uchaguzi wa 2020 usiwe ni igizo tuu la uchaguzi, Je tumchagize na kushinikiza Tundu Lissu ndiye asimamishwe na upinzani kumkabili John P. Magufuli? kwa sababu mpaka sasa, Tundu Lissu ndie mwanasiasa pekee wa upinzani ambaye so far, ameonyesha ana...
Wanabodi Declaration of Interest Naomba kuanza na ku declare interest kuwa mimi ni Kada wa Chama Cha Mapinduzi, CCM ambaye ni muumini wa haki na demokrasia ya kweli ndani ya Bunge. Nautoa ushauri huu kwa dhati ya moyo wangu, licha ya ukada wangu kwa chama changu, CCM. Asiyekubali Kushindwa Sio...
Wanabodi, Leo tena nimepata fursa ya kuwaletea makala hii ya "Kwa Maslahi ya Taifa". Hili ni bandiko la wito kwa Watanzania tuache kufanya mizaha kwenye kila kitu kama hali ilivyo sasa ya kufanya mizaha kwenye kugombea Urais wa JMT na Zanzibar, hata watu wasiostahili, wanapeleka majina yao...
Wanabodi, Hili ni bandiko la swali, ikitokea Tundu Lissu ameshindwa uchaguzi huu kihalali katika Uchaguzi Mkuu huru na wa haki, jee tumchagize JPM, for the the sake of national unity, and to heal the nation, amteue Tundu Lissu kuwa Mbunge wa kuteuliwa katika zile nafasi zake kumi za uteuzi as...
Wanabodi, Chadema kimekuwa kikishauriwa mambo mengi humu jukwaani, ila kimekuwa kichwa ngumu kupokea baadhi ya ushauri, kwa hoja kuwa unatoka kwa watu wasiokitakia mema, na wengine kufikia kiwango cha kuwaona kama ni shetani! Msemaji wa Chadema Tumaini Makene akakiri wazi kuwa Chadema inapuuza...
Tena licha ya mimi kuwa ni kada wa Chama Cha Mapinduzi, CCM, lakini nimepigania sana fair game hadi kutoa ushauri mahsus kwa watu mahsus
Wanabodi, Hili ni ombi maalum kwa watu maalum, hivyo hii thread sio thread ya watu wote bali ni thread maalum kwa watu maalum na lengo maalum la kutuma ujumbe maalum kabisa kwa watu maalum kabisa. Tanzania sio nchi ya watu fulani tuu au chama fulani tuu, Tanzania ni nchi ya Watanzania wote, wa...
Na baada ya chama changu CCM kushinda ushindi wa kishindo cha asilimia 99% kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa , nilipandisha bandiko hili la kizalendo sana
Wanabodi, Tangu kuanza kwa pilika pilika za uchaguzi wa Serikali za Mitaa, sijawahi kuzungumza lolote kuhusu uchaguzi huu kutokana na kuwa bize na shughuli za kitaifa, kwanza ni Wiki ya Msaada wa Kisheria iliyofanyika kitaifa mjini Bariadi Mkoani Simiyu na kufuatiwa na Wiki ya Azaki...
Watu wengi walikuwa na mategemeo makubwa na Chadema, niliwasaidia sana kuitathimini Chadema kama ina uwezo, the ability na capabilities
Wanabodi, Hili ni bandiko la swali la tathmini kuhusu upinzani kuweza kuchukua nchi uchaguzi wa 2020. Kwa upande wa huku Tanzania Bara, ulizungumzia upinzani ni unazungumzia Chadema, hivyo hili bandiko kuihusu Chadema, as a representative wa upinzani kwa huku Tanzania Bara, vipi kuhusu Chadema...
Wanabodi, Kwanza sote tunalaani kwa dhati kabisa, kitendo alichofanyiwa Mhe. Tundu Lissu cha kumiminiwa risasi 38 na watu wasiojulikana, kati ya hizo risasi 16 zikampata!, kitendo ambacho kimefanywa mchana kweupe, tena akiwa kwenye eneo ambalo ni secure area!, maeneo ya waheshimiwa, ambayo...
Wanabodi, Kichwa cha habari cha bandiko hili kinajieleza wazi, hili likiwa ni bandiko la swali, kuwa siku zote huwa nailaumu Chadema kuwa hawajitambui na hawajui wanataka nini!. sasa kesho Chadema wanafanya uchaguzi wa Mwenyekiti, swali ni jee sasa Chadema wanajitambua?, jee wanajua wanataka...
Mabandiko hayo matatu yalithibitisha Chadema hakuna kitu for 2020!. Ile nguvu na hamasa ya upinzani uchaguzi wa 2020, ni kutumia tuu upepo wa Tundu Lissu.
Kwa kifupi nilisema
Hivyo Dada yangu
Sky Eclat, and by the way mimi as a human being, nimetokea kukupenda fulani hivi japo sijakuambia...
Jumapili njema
P.