Pole sana Zitto kwa yanayokutokea. nadhani sasa umeamini kuwa hata ule mpango wa kutaka kukuwekea sumu ili ufe ulikuwa ni wa kweli. ingawa ulitumia nguvu nyingi sana kuukanusha lakini leo hii unatuthibitisha kuwa kuna wabaya ndani ya chama chako ambao kila kukicha wanakuandama. lengo lao si zuri hata kidogo na usipokuwa makini ujue ndiyo mwisho wako. najua harakati yao hiyo ni kutokana na dhamira yako ya kutaka kugombea urais wa nchi kwenye uchaguzi wa mwaka 2015. aidha hayo yanatokea huku chama kikiwa kinajiandaa kufanya uchaguzi wa viongozi ngazi ya taifa huku wewe ukitadhamiria kugombea nafasi ya uenyekiti. najua katika uchaguzi huo, mpango umeandaliwa ili wewe na ARFI muondolewe kabisa kwenye safu ya juu ya uongozi. najua nafasi zenu zitachukuliwa na KITILA MKUMBO na PR. ABDALLAH SAFARI. mipango hiyo imekamilika na kinachosubiriwa ni uchaguzi huo ufanyike. lengo kuu la mpango huo ni kutaka kukuondoa kabisa kwenye safu ya maamuzi ndani ya chama chako. hatua hiyo ilianza muda mrefu na Dr SLAA ndiyo anayeusimamia. ndiyo maana yeye anapokuwa nje ya nchi kikazi, majukumu yake anamwachia JOHN MNYIKA wakati wewe ndiye uliyekuwa unastahili. hata katika maamuzi mazito kama yale ya kuwafukuza akina MWAMPAMBA na SHONZA, mawazo yako yalipuuzwa.
ZITTO, nakushangaa sana unavyotumia nguvu nyingi na muda mwingi kuwatetea watu wasiokutakia mema. suala la lwakatare lipo bayana kabisa na ilipaswa chama kichukue hatua ili kisipakwe madoa. kitendo cha kukamatwa lwakatare kufuatia kashfa ya video ya kupanga njama za kigaidi ni aibu kubwa si tu kwa lwakatare mwenyewe bali ni kwa chama pia. kumbuka LWAKATARE ni Mkurugenzi wa ulinzi na usalama wa chama na ninaamini kuwa mipango hiyo kama si maelekezo ya Katibu Mkuu WILBROAD SLAA basi alimshirikisha katika hatua zote. nina hakika hata Mwenyekiti FREEMAN MBOWE mipango hiyo alikuwa haijui na ndiyo maana akakimbilia kusema kuwa kama LWAKATARE amehusika kwa makusudi au uzembe basi anatakiwa awajibishwe. kwa kuwa Dr Slaa anajua nini kinachoendelea katika sakata hilo, amefanikiwa kuwashawishi viongozi wote ili chama kiwe na msimamo mmoja wa kumtetea LWAKATARE kwa gharama zozote zile. tayari kiasi kikubwa cha fedha kimetengwa kwa ajili ya kumhonga JAJI aliyepangwa kusikiliza kesi hiyo na ndiyo maana kauli imetolewa kuwa CHAMA KINA IMANI NA JAJI HUYO. kama kweli chama kinaona kuwa LWAKATARE ameonewa, iweje watenge kiasi kikubwa zaidi ya shilingi milioni 100 kwa lengo tu la kuhakikisha ukweli unapindishwa? mikakati yote hiyo inafanyika bila ya wewe Naibu Katibu mkuu kushirikishwa na bila kuijua. ndiyo maana nikatangulia kusema kuwa unajaribu kuwatetea watu wasio na dhamira njema nawe.
ZITTO, hivi unajua ni kwa nini viongozi wenzako wa CHADEMA kupitia Kamati Kuu wameagiza JF kuondoa mijadala yote inayokielemea chama? ni kwamba wamebaini kuwa viongozi wa chama hawapo pamoja na matamshi yao yamekigawa chama. pia unajua ni kwa nini chama hakimtetei LUDOVICK JOSEPH wakati yeye ni mtu wa karibu sana na familia ya Dr Slaa? kama LUDOVICK amesalitiwa, je wewe ambaye ni kama damu ya kunguni kwa dr slaa utapendwa kwa lipi? ndugu yangu, nakupenda sana na najua una safari ndefu katika ukombozi wa taifa hili. wewe ni mzalendo halisi na hawa wengine wapo kwa maslahi yao tu.
zitto, tunakushukuru kwa kututhibitishia kuwa ile video ya LWAKATARE ni halisi kama alivyofanya LISSU. Ninaamini hata ule mjadala wa ama video ile ni halisi au feki umekufa baada ya kupata majawabu sahihi.
pamoja na hayo ZITTO, bado ninakushangaa kwa kwenda kinyume na matakwa ya Kamati Kuu ya CHADEMA. kama wamekubaliana kuwa msemaji mkuu katika sakata la LWAKATARE ni LISSU, iweje wewe unaongelea jambo hilo katika mitandao ya kijamii? mie ninaamini cha muhimu ujumbe kutolewa. aidha Kwa kuandika au kuongea lakini kote ni kutoa ujumbe. kitendo chako cha kuendelea kuongelea suala la LWAKATARE unashindwa kuficha hisia zako na matokeo yake unakiumbua chama. najua utaniuliza mbona jambo hilo lipo mahakamani na mbona viongozi wa CHADEMA akiwemo lissu anaongelea mara kwa mara ilhali anajua kuwa huko ni kuvunja sheria. jibu ni fupi sana. LISSU anajua kuwa LWAKATARE ana hatia hivyo anajaribu kuongea kwenye public kupotosha mawazo ya watu na kutaka huruma kwa jamii ili ikiamuliwa kuwa LWAKATARE ahukumiwe kifungo warudi mitaani kuandamana kwa madai kuwa CCM wanakidhoofisha shama
namalizia kwa msemo wa kiswahili kuwa NUNGUNUNGU HAKUMBATIWI