Barua ya Zitto kuhusu Lwakatare: Maelezo yangu

Status
Not open for further replies.
Nimefatilia Majibu/Maelezo ya Zitto
kiukweli naona kuna mapungufu makubwa kwenye Uongozi wa juu wa Chadema, nilikuwa najaribu kujiuliza maswali yafuatayo
1) Hivi Zitto hiyo barua alimkabidhi nani pale ofisini?, Secretari au Katibu mwenyewe (Dr Slaa)?
2) Kwa mtazamo wangu Barua haiwezi kukidhi haja sana ya maswali, maoni pamoja na majibu yenye kushiba, kama Zitto na @Dr Slaa wapo ofisi moja ilikuwa kuna ugumu gani wa Zitto na Slaa kukutana ofisini na kuongea 'fizically' nadhani yangeongelewa mengi zaidi ya yaliyokuwepo kwenye hiyo barua.
3) Nadhani kuna kutoaminiana,kuogopana au kuviziana kwa kiasi kikubwa baina ya viongozi wa Chadema,
Maana halisi ya kuandika barua ni kupeleka ujumbe na kisha kuwa na kumbukumbu na pia ushahidi, kwa mtazamo wangu Zitto aliandika barua ili iwe kumbukumbu na pia ushahidi kuwa alishauri ama alionya kuhusu hilo swala,

Swali ngumu ni nani alivujisha hiyo barua? na kwa nini?
kimtazamo:
labda nianzie hapa, Hiyo barua haina faida kwa Chadema kama Chama, Bali ina faida kwa Zitto kisiasa,
Kichama wameonyesha misimamo yao kuwa wapo bega kwa bega na Lwakatare, Sijasikia kiongozi wa juu wa Chama akiongea against na hiyo case, inaonekana Slaa, Mbowe pamoja na Lissu wanamuunga mkono Lwakatare, Misimamo ya hao viongozi niliowataja ndio ulikuwa unaonekana kana kwamba ndio msimamo wa Chama,

Zitto ana haki kabisa ya kutokubaliana na misimamo ya hao viongozi wenzie, na ana haki ya kutoa maoni yake na kukishauri chama, na kwa 'mtazamo wake' ilikuwa ni muhimu kukishauri chama kwa ushahidi (Barua).
--------------------------
--------------------------
--------------------------

Kulingana na muonekano wa kesi ya Lwakatare, Hiyo Barua ni muhimu sana kwa Zitto kisiasa kuliko Chadema kama Chama
 
Last edited by a moderator:
Mmh siasa za vijana! Kumbe Zitto anamfahamu Ben! du Ukistaajabu ya Zitto utayaona ya Ben.
wapi imesemwa ZZK anamfahamu BEN?Huyu Ben ndo alikuwa anaomba akutanishwe na zitto.
 

umesema kweli kabisa yaani huyo Zitto anataka kuonyesha kwamba kwenye chama chake hakuna utaratibu wa mawasiliano anashangaza sana huyo mdudu
 
wapi imesemwa ZZK anamfahamu BEN?Huyu Ben ndo alikuwa anaomba akutanishwe na zitto.

Juliana Shonza na Mtela Mwampamba wamethibitisha Ben na Zitto kukutana mara nyingi japo Zitto anakataa kwa sababu ambazo hawezi kuzielezea
 
THE TEAM
Zitto Kabwe,Shibuda,Shonza,Mwampamba,mtera,Ludovick,Habib Mchange,Mwigulu,nape,Riz1
 
Juliana Shonza na Mtela Mwampamba wamethibitisha Ben na Zitto kukutana mara nyingi japo Zitto anakataa kwa sababu ambazo hawezi kuzielezea

Taratibu wanajianika tena hiyo post no. "703" nafikiri ni kati ya hayo MP7.
 




Afanye maamuzi hayo
Submitted by Mwandishi wetu (not verified) on Tue, 14/12/2010 - 4:42pm.
Afanye maamuzi hayo anayoyataka. Anamtisha nani bwana? Huo ni utoto na naanza kuamini kuwa alivamia siasa hali yakuwa hakuwa na mvuto nayo. Kwa mwenendo huu, Zito hafai hata kuwa mjumbe wa nyumba kumi (Kama zipo) maana anaonyesha yeye kuwasaidia mafisadi. Halafu watu wanaoona kuwa Mwanahalisi (Kubenea) anazusha mambo maana ninasoma Comment za watu mbalimbali na story mbalimbali napata wazimu fulani. Wanasema eti kubenea unachonganisha watu kwa story hizi. Kama wanaona si za kweli, wakupatie ushahidi utakaotofautisha hayo yote; na si kubwabwaja tu. La hawataki, waende mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake. Kama Zito anaulizwa na Mnyika juu ya ujumbe, hajibu maana yake nini?? Ni kuonyesha jinsi gani yuko "guilty" kwa hilo. Chadema mfukuzeni huyo; asiwacheleweshe na wala asiwatishe. Inachekesha kweli, kwamba atatoa maamuzi ambayo hayategemewi na watanzania?? Ajabu kweli. Mwalimu JK alivyong'atuka, watanzania tulijiuliza tutaongozwa na nani. Leo nchi ina awamu tatu zaidi za uongozi na nchi ipo; hata kama haiendi vizuri sana. Lakini ipo na itaendelea kuwepo. Yeye anatishia watu nyau? Thats being stupid tena a high degree of stupidity. Kama una mawazo ya kutofautiana na wenzako, unasema ukiwa kifua wazi na watu wanasonga mbele. Zito hujawa LULU kiasi hicho, kwamba kutokuwepo kwako kutaifanya nchi itetereke. Rais angesema atachukua uamuzi mgumu, watu mnatishika maana ana dola na sheria inampa uwezo wakati mwingine hata kuamuru mtu kufa (Kunyonga). Itakuwa wewe bwana??? Acha hizo. Tumia usomi wako vizuri bro.

Source:
http://www.mwanahalisi.co.tz/siri_za_zitto_nje

 

That's my sentiments, exactly. I'm anti ZZK but truth be told, Ben used to belong to ZZK camp that time when he blindly supported Malema. I told you both that Malema was an opportunist and the ANC was going to fix him. I'm baffled now to see Ben waging a war against his fellow hypocrite, ZZK
 
nashukuru kiongozi wangu penye nia pana njia.kufikia mafanikio lazima kuwe na vikwazo vingi.Mungu ibariki CHADEMA.Hakika tutashinda
 
zitto mwenyewe anakanusha uwepo wa njama hizi lakini we bi mdogo umeng'ang'ania!!!huku nkama sio kujipendekeza in first degree tukuiteje?
 

Oh really?

Malema is a force to be reckoned with.The really enemy of ANC is not Julius Malema

Ironically, Mr Malema and supporters are trying to do what the league's founders, including the country's former President Nelson Mandela, did beginning in 1944.



By being mildly militant-calling for civil disobedience against the apartheid rule-they had taken control of the ANC by the end of the decade.


Sijui unamuweka wapi Jacob Zuma ambaye ni mwanasiasa msaliti na asiyeaminika.Ni fedheha sana kwa Rais wa taifa kubwa Afrika Kiuchumi na katika nguvu za kijeshi (super power) kushiriki katika mbinu za mabeberu kuidhinisha no-Fly Zone Kule Libwa kumuondoa Muammar Ghaddafi kwa kushirikiana na waasi.Hakukitendea haki kiti cha Afrika kwenye UN Security Council(non permanent members)

Wanasiasa vigeu geu na wabinafsi ni hatari sana maana wakipata madaraka watakua hawana tofauti na wakoloni wanaotakiwa kuondolewa.Leo utawala wa ANC umeshindwa kujitofautisha na Makaburu kwa kuwa tu Zuma anapenda kubeba populist agenda.Wanasiasa wanaopenda kubeba ajenda maarufu za muda huo ni wabinafsi wa kupindukia na hawafai kuchukua uongozi wa juu wa taifa lenye ndoto kubwa za miaka 50 au 100 ijayo

Juzi wanajeshi wengi wa South Africa wameuawa huko Jamhuri ya Afrika ya Kati wakati waasi(Mashujaa) wa SELEKA walipokua wakipambana kuipundua serikali iliyoshirikiana na mabeberu kupora raslimali za nchi hiyo.Ni aibu kwa SA kutuma majeshi kuulinda utawala corrupt unaohujumu wananchi wake na kuwa dalali wa raslimali za nchi kwa mataifa ya mabeberu.Jacob Zuma amezoea tabia hii maana hata alipokua akijaribu kumpindua Thabo mbeki ndani ya ANC alikua akipata sapoti kutoka kwa serikali ya vibaraka ya Botswana na Uholanzi.Tabia hiyo ameiendeleza baada ya kutwaa madaraka ya ANC na ukuu wa nchi.Hata Ghaddafi alimfadhili kumng'oa thabo Mbeki kwa kuwa yeye na mbeki walikua na power struggle kuhusu PAN AFRICANISM.Leo amekuja kumsaliti kwa ubinafsi na uroho wake.Huyu ni adui wa South Africa na Afrika kwa ujumla

Kama ni opportunist basi Jacob Zuma ndiye opportunist namba moja,a toothless president wa super power.Ameshindwa hata kubadili economic policies na foreign policy to suit SA's Role katika mataifa ya BRICS.Ni fedheha ya Africa
 

Unaweza kutusibitishia hapo? ama alishindwa kwako? Wanafiki wote na Zitto wako, anajiandikia barua mwenyewe, anaiweka kwenye mtandao mwenyewe anaanza kulia mwenyewe, Sishangai ni sifa za Mnafiki hizo! kutafuta huruma
 
Last edited by a moderator:
kwa upande mwingine ngoma ni drow kwani chedema imepandikiza mamluki ccm na usalama wa taifa,na ccm pia wamepandikiza kwa chadema[/QUO

Muosha naye anapooshwa....tehe...tehe....tehe.......

Mkuu.
Mchango wako umefanana na jina lako! No facts no right to speak.
 
well said mkuu zito.

ZK haya mapandikizi yanayonyemelea kila jambo hapo kinondoni lazima yaangaliwe sana ama sivyo yatakuwa kama NCCR mageuzi enzi ya mwanzo wa Demokrasia ya vyama vingi inaanza. Ushauri wangu ni kuwa Watanzania siasa za vyama vingi sio dhambi na watawala wakubali kila jambo wanoloshindwa nawaomba CDM zidisheni nguvu ipo siku YES
 
naona dogo zitto anaendeleza mind game, barua kaandika yeye kaipelelka kwa katibu baadae amee-upload the same letter mtandaoni anakuja na gia eti nimeombwa na watu wa jamiiforums nitoe maelezo, yuko kama kingwangalla anaanzisha thread kisha anaichangia yeye mwenyewe kwa ID tofauti tofauti.

hiyo barua uliiandika ukiwa mezani kwa katibu mkuu au uliandikia uswahilini ndo ukaipeleka? kama hukuiandikia mezani kwa katibu mkuu ebu tupe chain of custody ya barua yako kabla ya kufika kwa katibu mkuu? acha utoto dogo, try to grow a bit.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…