Bashe: Kuna kikundi ndani ya Idara ya Usalama (TISS) kinahusika na utekaji. Wabunge 11 wapo kwenye orodha ya kutekwa

Bashe: Kuna kikundi ndani ya Idara ya Usalama (TISS) kinahusika na utekaji. Wabunge 11 wapo kwenye orodha ya kutekwa

Usalama wa Taifa wapo kwa maslahi taifa.
Sure but they have to be smart kwa kila walitendalo.... Too much alcohol can course harmful to the society... na hakuna kilichofia kuhatarisha Taifa upande wa wananchi mpaka ifikie watu kutolewa roho kilazima... cha zaidi wao ndio sasa inakuwa wanaleta khofu kwa Taifa... Watu wanatakiwa wafanye kazi kwa ueredi wao na sio kulazimishwa wafanye cha anayetaka... Trust me zogo litatokea siku si nyingi Ukila sana utavimbiwa
 
Bashe yalimkuta wakati wa mkutano mkuu wa CCM.alikamatwa akawekwa kusikojulikana,akaachwa bila kupewa sababu yoyote.
 
Akili ya Bashe sio nzuri kabisa,aache kujihami kama anafanya mabaya aache. Usimseme mzee Magu pasipo kuwa na ulazima angalia watekaji wanaweza kuwa wengi hata kama unatembea na mke wa mtu ukitekwa utasema serikali?, waache utoto kuisingizia kila kitu serikali wafuatilie route course analysis ndo waje huku, japo JF ni jukwaa huru asituimanishe ujinga sisi bado tunaipenda serikali yetu. Amani kwanza-taifa lenye amani hili bhana
sasa si kasema katumiwa ujumbe mnaogopa nni kma siri imevuja??? hvi wwe kweli roma atekwe baada ya watu kupiga kelele ndio eti makonda anasema atampata kabla ya junatatau we huoni kma kuna movie flani inaendelea hapa nchini???? badala ya kumuunga mkono bunge huyu ili tabia hii ya watu kupotea kma alivyodai bashe na nape pia litokonezwe nyie mnakuja hapa mnaanza kumtetea magufuli!!!!! kwahyo unataka kusema magufuli is perfect?? akikosea asikosolewe ???
 
kosa kubwa la wengi wetu ni kujaribu kuchokonoa mambo yasiyochokonoleka..

kujifanya much know kwenye masuala muhimu ya usalama wa Taifa letu ambayo hata utaalamu wake hatuna.

usalama wa Taifa hili hauhitaji kuwa compromised na siasa.

ukitafuta kiki kupitia interest za kiusalama lazima upotee..

I love my country Tanzania wanasiasa wapotoshaji na wenye uchu ni wa kuogopwa kama ukoma.
 
Bashe anatengeza bifu na TISS na anachokitafuta atakipata
 
Huyu ndo aisaidie polisi na TISS awataje hao mawaziri na aonyeshe hizo meseji.
Ujinga gani huu wa kuchafuana bila ushahidi?
Wasigeuze Bunge kichaka cha porojo
 
Huyu Bashe anajistukia tu, kwanini asijilipue kabsa kwa kutaja wahusika maana anajijua kabsa hayupo CCM tokea kipindi kile lowassa amekatwa hivyo nafsi yake haina amani kabsa kuendelea kuwepo CCM ila tu anajilazimisha, kujilazimisha huko kuna mkuta anazungumza mambo ya ajabu kabsa ya kumchafua Rais. Chunguzeni kwanini wale team Lowassa wote kama bashe,msukuma,malima ndio wapiga kelele kila siku? Kwanini Wao tu?

Hivi usalama gani wa taifa ukawa na kikundi cha utekaji na tena utekaji wa kipuuzi kabsa kama tunaouona sasa? System ikitaka kukuua inakuondoa tu haisubiri kukuteka.

Hizi ni chuki tu za baadhi wa wabaya wa Magufuli maana kama kuyabana majizi ni kweli kayabana kwa hiyo tusitegemee mteremko kwa Magufuli hata siku moja.Watu wenye pesa chafu watahonga sana hawa whistleblower kumchafua Magufuli.

Watamsingizia mengi mno huyu mzee na ndio kwanza picha inaanza.
kuna MAJITU MENGINE HUMU wao chuki zao ni mbele tu HATA KWENYE UWONGO YANAKUBALI TU.....utasikia mtu anasema ETI MAGUFULI nchi imemshinda....SASA hao ambao nchi haikuwashinda walitufikisha wapi???mbna still mlikuwa mna piga kelele???
Afadhali ya huyu amabaye nchi imemshinda lakini pesa za walipa kodi zipo salama si kwenye mikono ya wachache.......
ACHA TU atunyooshe HII MIAKA 10 AKILI ZIKAE vizuri kichwani......
Tudhibitishie haya yanayoendelea hayana mkono wa kikundi flani cha kimafia ndani ya nchi hii kwa concrete evidence
 
bungeni hawajatumwa na JPM, bungeni wametumwa na watu waliowapa kura na kuwaamini, hawakuteuliwa kama dada zako ambao hawajui shida za wananchi,

Haya, waambie basi wawakilishe wananchi , na kama wameshindwa basi waachie ngazi siyo kupeleka kelele bungeni.

Kama hakuna hela, usalama wao unatishiwa basi, wakalime kwani mapori si yapo yakutosha??
 
MARA NYINGI SIWAAMINI WABUNGE WA CCM. KWANI MWISHO WA SIKU HAWASITI KUKATAA WANAYOYASIMAMIA.
BAJETI YA 2016/17 IMESHINDWA KWA KIASI KIKUBWA LAKINI UTASHANGAA INAYOKUJA WATAIPITISHA KWA KISHINDO.
Wangekuwa na ushirikiano na wabunge wa upinzani rais na hao wasaidizi wake wangeliheshimu bunge.
 
Idara ya usalama wa taifa kuteka ni moja ya majukumu yao, ila ni nani anaetekwa??? ni yule anaeonekana kuhatarisha usalama wa taifa. Sasa Bashe jipime kama unahatarisha usalama wa taifa unaeza ukawa miongoni. To me bashe bado hujafikia kiasi hicho cha wewe kutekwa, wewe ni wa kuvuliwa tu uanachama uka ungane na Lowassa wako. Usilete unazi wako.
Kwa hiyo TISS sasa inafanya kazi za kuitumikia ccm . . . ?

Kwani ktk chama chenu hamna namna ya kuwashughulikia wanachama mliowachoka mpaka mtumie TISS kuwateka au kuwanyamazisha . . ?!
 
Back
Top Bottom