BBC yarusha habari kuhusu wakosoaji wa Serikali wanaotekwa, kupotea au kuuawa

BBC yarusha habari kuhusu wakosoaji wa Serikali wanaotekwa, kupotea au kuuawa

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
27,843
Reaction score
29,350
Katika amka na BBC leo asubuhi tarehe 03/09/2025, shirika la utangazi la BBC limejaribu kuwataja watu wanaowaua wakosoaji wa serikali, akiwemo Shadrack Chaula (Car of God) kutoka mkoa wa Mbeya aliyetekwa mwezi mmoja baada ya kunusurika kifungo cha miaka miwili kwa kosa la kuchoma picha ya Samia.

WATUHUMIWA WANASEMAJE?
Viongozi wa serikali walipotakiwa kutoa ufafanuzi, wamekimbia na kuingia mitini. Mbali na kamanda wa polisi aliyesema uchunguzi bado unaendelea, hadi sasa kuna wakosoaji wengi wa serikali wameuawa, akiwemo Tundu Lissu aliyeponea chupuchupu kuuawa kwa risasi.

Watetezi wa haki za binadamu wamekuwa wakikemea vikali mauaji haya na kusema ikiwa watu wana makosa ni afadhali wafungwe jela badala ya kuuawa ovyo kama umbwa. Wametolea mfano wa Car of God ambaye alifungwa kihalali kwa kuchoma picha ya rais na kulipa faini halali ya kisheria lakini baadaye wauaji wakaja kuchukua. Haipendezi.

MAONI YANGU
Nakemea kwa nguvu zote haya mauaji ya wakosoaji wa serikali. Kama wana makosa ni vizuri wafungwe badala ya kuuawa.


View: https://www.youtube.com/watch?v=dpelpum5ecU
​
 
Kuna vitu vingine huwa nashindwa kuelewa. Inawezekana watz wengi wana tatizobla changamoto ya afya ya akili. Sasa mleta habari anasema bbc imelitaja genge watu wanategemea umewaletea taarifa ukiwaweka wazi hao waliotajwa ili kila mtu awajue. Sasa wewe unachofanya kinamsaidia mtu kivipi anayesoma uzi huu?

Maana hayo majina hawajayaona. Au unatafuta tu validation kwamba na wewe uliwahi andikaga kitu humu.

Huu muda uliotumia kuandika huu uzi si ungekuwa unafanya kazi inayokupatia kipato baadae watoto wako angalau wapate chochote kitu tumboni. Aisee kweli changamoto ya afya ya akili ni kubwa tz
 
Kuna vitu vingine huwa nashindwa kuelewa. Inawezekana watz wengi wana tatizobla changamoto ya afya ya akili.
Uko sahihi taifa lina wajinga wengi

USSR
 
Mimi nafkiri hao watekaji waongeze kasi ili watu wengi waweze kutekwa na kuuliwa


Kauli hii labda kuna watu inawapa faraja hasa wale wanaowatetea hao watekaji
 
Walipoulizwa waliingia mtini nani hao serikali kwahyo wauaji ninani ni serikali
 
Katika amka na BBC leo asubuhi tarehe 03/09/2025, shirika la utangazi la BBC limejaribu kuwataja watu wanaowaua wakosoaji wa serikali, akiwemo Shadrack Chaula (Car of God) kutoka mkoa wa Mbeya aliyetekwa mwezi mmoja baada ya kunusurika kifungo cha miaka miwili kwa kosa la kuchoma picha ya Samia.

WATUHUMIWA WANASEMAJE?
Viongozi wa serikali walipotakiwa kutoa ufafanuzi, wamekimbia na kuingia mitini. Mbali na kamanda wa polisi aliyesema uchunguzi bado unaendelea, hadi sasa kuna wakosoaji wengi wa serikali wameuawa, akiwemo Tundu Lissu aliyeponea chupuchupu kuuawa kwa risasi.

Watetezi wa haki za binadamu wamekuwa wakikemea vikali mauaji haya na kusema ikiwa wtu wana makosa ni afadhali wafungwe jela badala ya kuuawa ovyo kama umbwa. Wametolea mfano wa Car of God ambaye alifungwa kihalali kwa kuchoma picha ya rais na kulipa faini halali ya kisheria lakini baadaye wauaji wakaja kuchukua. Haipendezi.

MAONI YANGU
Nakemea kwa nguvu zote haya mauaji ya wakosoaji wa serikali. Kama wana makosa ni vizuri wafungwe badala ya kuuawa.

Chanzo
Mbona hakuna genge limetajwa
 

Hatimaye documentary ya Utekaji na Upotezaji wa Wakosoaji wa Serikali imerushwa rasmi na Chombo cha habari cha Kimataifa cha BBC

Kurushwa kwa habari hii rasmi na Chombo rasmi cha habari cha Kimataifa ni uthibitisho rasmi kuwa masuala ya utekwaji na upotezwaji wa Watanzania wasio na hatia umefika rasmi Kimataifa.

Huu ni mwanzo mzuri kwenye shauri atakalofunguliwa Samia, Mtoto wake Abdul, Mkwe wake Mchengerwa na Wasaidizi wao wote akiwemo SACP Mafwele, CP Awadhi, Juma Homera, IGP Wambura na Wengineo wengi katika Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai ( ICC) wakati wowote ule kuanzia sasa.

Tunashukuru BBC. Tunategemea Makala ile kurushwa zaidi hadi kwenye Channel yenu ya Kiingereza ikiwemo kwenye Program ya Focus on Africa.

No Reform No Election ✊️ ✌️
 
Mleta mada kasema kwamba kwenye hiyo taarifa eti genge limetajwa. Ukiisikiliza hiyo taarifa genge halijatajwa. Sasa hadi hapo kila mtu anajua kuwa mleta mada ana changamoto ya afya ya akili. Hawezi sema genge limetajwa wakati genge halijatajwa.

Nadhani watu kama hawa huyu mleta mada maisha yashamshinda hajafanya chochote katika maisha yake sasa hasira alizonazo anajaribu tupa lawama kwa na kutengeneza stori kulaumu kuwa watu wengine wanaangusha maisha ya wengine ikiwamo ya kwake. Kaka fanya kazi upate pesa
 
Back
Top Bottom