Nentanyau leo kasema ni siku nzito sana leo kwani wamepoteza askari 14 na mapigano makali. Ila kasema hawana budi lazima waendelee tu mpaka wakomboe mateka wote, sasa kweli akili za kawaida tu unataka kukomboa watu 200 sijui lakini umepoteza askari 153 na vita bado na hujui lini utafikia target. Ila nilivomuona leo akiongea unaona mtu ana stress mimi nadhani ali underestimate hii kazi. Vita vya siku hizi vigumu sana maana silaha ndogo bei rahisi zinaleta maafa makubwa. Hawa Houthi wanatumia drone za alfu 2 ma USA kuzitungia anatumia kombora la mil 2 bado gharama za patrol, hivi hawa jamaa wana akili kweli? sawa na kuuza mbuzi ushinde kesi ya Kuku.