Kwanza ningependa kuwakumbusha kama Zanzibar ni nchi ambayo ina raisi wake, ina Bandari yake na ina kila kkitu chake.
Nimekua sipati majibu kwa nini Watanzania bara walio wengi wao wekua na wivu na manung’uniko juu ya visiwa hivi vya Zanzibar mpaka kufikia kulalamika hadharani juu ya bei zetu kuwa chini.
Na pia utaona wanaanzisha thread katika majukwaa tofauti kuwadhihaki na kuwasimanga Wazanzibari mara utawaskia ooh Wanawake wa Zanzibar sijui hawana bikra sehem fulani, jitu linasema ivo ata halijawahi kumuona msichana wa kizanzibari, kwenye hili la mahusiano leo niwaweke wazi ni suala la aibu na fedheha sisi wasichana wa kizanzibari kuwa na mahusiano na wasiekua wazanzibari haswa Watanganyika, kwaio msijisumbue bure wakuu.
Na pia wengi wenu mnaomchukia Raisi aliepo sasa madarakani ni kwa Sababu ya Uzanzibari wake, amekua hana jema kwenu, maana itafika wakati mtu akinyimwa unyumba na mke wake atakuja majukwaaani kulalamika rais amesababisha hivo nawaomba ndugu zangu Watanganyika mpunguze makasiriko.
Mwisho kabisa ningewaomba watanzaania bara mupambane na hali zenu baadhi yenu chuki zenu zidi ya visiwa vya Zanzibar havitowasaidia kitu zaidi ya kuwaongezea maumivu ya moyo kwa sababu Wazanzibari tuna tamaduni zetu na silka zetu na tunajivunia Uzanzibari wetu
View attachment 2212197