Chip zipo nyingi, na Zinatengenezwa maeneo mengi tu, kitu ambacho China wameshindwa ama atleast itawachukua miaka 20 kuweza kutengeneza ni issue za Semiconductor na kuna mambo mawili
1. EUV za ASML ya Mholanzi
2. Silicon za Mjapan
Hizo EUV ni machine complicated sana zinazotumika kutengeneza processor, Gpu na vitu vingine, ukisikia TSMC, sijui intel ama Samsung wanatengeneza Processor za kisasa ujue EUV inahusika. Ipo kama hivi
View attachment 2632839
Hako kadude kanauzwa kama trilioni 1 hivi. Sasa hivi mchina anawekeza matrilioni ya Hela kuja na Alternative yake.
2. Mjapan ndio anasuply most purified Silicon ambazo zinatumika kwenye semiconductor. Ni crucial kutengeneza chip kwa manufacturing process ndogo mfano hizi 3nm ama 4nm etc.
Kifupi mkuu hata Marekani mwenyewe hii tech hana na hata hao Waholanzi wanamsaidia tu Marekani sababu hawana jinsi (Marekani ana wa Blackmail) ila Waholanzi kesho wakijitoa Mhanga na kuside na China kibao kinageuka.
Tech nyingi ngumu ngumu zinatoka Japan na Ulaya hasa Maeneo ya Nordic, Ujerumani, Uholanzi etc.