Beijing: China yaiwekea vikwazo kampuni ya utengenezaji wa chips ya Marekani (Micron)

Sababu kuu ni teknolojia ya uundaji, waalamu, malighafi zitakazo tumika, uwekezaji,R&D e.tc
Nafahamu hivyo ila sioni kama ni vigezo ambavyo nchi kama china, korea, urusi, na india kua vimewashinda! Malighafi hawawezi kukosa, wataalamu kama wote na hata technology ipo juu na inaweza kununuliwa ikibidi, kwenye uwekezaji ndio kabisaaa
 
Reactions: TPP
Hili tatizo limeanzishwa na US mwenyewe kwa ushirikiano na mataifa rafiki kutumia sanctions kama silaha zinapo geuka kwao inakuwa uvunjifu wa sheria.
 
Nafahamu hivyo ila sioni kama ni vigezo ambavyo nchi kama china, korea, urusi, na india kua vimewashinda! Malighafi hawawezi kukosa, wataalamu kama wote na hata technology ipo juu na inaweza kununuliwa ikibidi, kwenye uwekezaji ndio kabisaaa
Teknolojia ya utengenezaji wa Chips ina ugumu wake na inahitaji umakini sio rahisi kupata teknolojia bora ya utengenezaji wa chips bora duniani kwa sasa.
 
Micron wanatengeneza Storage ama Memory kwa ujumla. kuna alternative nyingi mno, Samsung, Sky Hynx, Kioskea (zamani Toshiba) na hata China wana local companies zinatengeneza sio Tech ambayo ni complicated sana kama Semiconductor nyengine.
 
Teknolojia ya utengenezaji wa Chips ina ugumu wake na inahitaji umakini sio rahisi kupata teknolojia bora ya utengenezaji wa chips bora duniani kwa sasa.
Sijaona ugumu wake ilihali kuna viwanda vipo hapahapa duniani na vinatengeneza! Hiyo technology huyo america kaitoa wapi ambapo dunia nzima kusiwe na yeyote atakae weza kuziunda!
 
Reactions: TPP
Unasema China iwape Morali wataalamu wake wakati huo huo wewe taifa lako linabakia kuwa la omba omba tu, himiza watu wa taifa lako kujikita kwenye STEM,
Sawa upo sahihi ila nlimjibu kwa hoja yake ya China kupiga ban km wamekosea au laah.
 
Hii imekuwa tabia ya US kutumia sanctions kama silaha kuliko kuacha ushindani kama ambavyo ana tangaza sera za kibepari na faida zake.
Na huo ujinga wake ndio unao sababisha mataifa mengine yanaendelea mpaka anashindwa kuyamiliki maana kwa huu upuuzi lazima kila mtu ajitafute tu hamna namna
 
Hii vita ya chips ni noma! Ila ninini kinacho sababisha nchi kama china mpaka leo kushindwa kuunda chips zake!!? Kuna india na korea, wanashindwa nini kuunda hivi vitu!!?
Chip zipo nyingi, na Zinatengenezwa maeneo mengi tu, kitu ambacho China wameshindwa ama atleast itawachukua miaka 20 kuweza kutengeneza ni issue za Semiconductor na kuna mambo mawili

1. EUV za ASML ya Mholanzi
2. Silicon za Mjapan

Hizo EUV ni machine complicated sana zinazotumika kutengeneza processor, Gpu na vitu vingine, ukisikia TSMC, sijui intel ama Samsung wanatengeneza Processor za kisasa ujue EUV inahusika. Ipo kama hivi


Hako kadude kanauzwa kama trilioni 1 hivi. Sasa hivi mchina anawekeza matrilioni ya Hela kuja na Alternative yake.

2. Mjapan ndio anasuply most purified Silicon ambazo zinatumika kwenye semiconductor. Ni crucial kutengeneza chip kwa manufacturing process ndogo mfano hizi 3nm ama 4nm etc.

Kifupi mkuu hata Marekani mwenyewe hii tech hana na hata hao Waholanzi wanamsaidia tu Marekani sababu hawana jinsi (Marekani ana wa Blackmail) ila Waholanzi kesho wakijitoa Mhanga na kuside na China kibao kinageuka.

Tech nyingi ngumu ngumu zinatoka Japan na Ulaya hasa Maeneo ya Nordic, Ujerumani, Uholanzi etc.
 
Sijaona ugumu wake ilihali kuna viwanda vipo hapahapa duniani na vinatengeneza! Hiyo technology huyo america kaitoa wapi ambapo dunia nzima kusiwe na yeyote atakae weza kuziunda!
Ni mataifa mangapi yana miliki teknolojia ya utengenezaji wa makombora ya kinyuklia bila usaidizi au wizi kwa mataifa ya nje ?

Teknolojia ya Chips ni mfano wa bomu la kinyuklia katika teknolojia dunia kwa sasa kwa hiyo inalindwa.

China anayo teknolojia ya kutengeneza Chips lakini sio za ubora wa juu zaidi kama U.S, Netherlands na Taiwan.
 
China ikipoteza soko la bidhaa la Marekani na Ulaya itakufa njaa. Hakuna nchi nyingine duniani zenye uwezo wa kuipa hizo pesa wanazopata huko. Mauzo ya China Marekani/ulaya/G7 ni zaidi ya theluthi na huko wanauza zile bidhaa za daraja la kwanza.
Lala naisi bado unaota aliyekwambia nani kuwa China ndyo inaitegemea tu west sema pia west wakikosa soko LA China watallala njaa west wanaitegemea China kikubwa zaidi siyo tu kama mletaji wa bidhaa nchini mwao ila kama mnunuzi mkubwa wa bidhaa zao, Tesla walifungua kiwanda kikubwa cha magari China siyo kwasababu ya nguvu kazi ila sababu ya uwitaji mkubwa na soko muhimu kwa bidhaa zake Tesla imepata faida kubwa sababu ya manunuzi makubwa ndani ya uchina, ivyoivyo kwa IPhone faida kubwa ya bidhaa zao inatoka China kampuni zote kubwa za magari ulaya zinaona China kama soko lao LA muhimu kwa bidhaa zao, kwaio kijana acha kuichukulia poa China kama nchi maskini kama zetu izi uchumi wa China ulipofika siyo wa kuufananisha nawa nchi yoyote pale ulaya
 
Kuhusu EUV lithography kuna baadhi ya vipande China imekwisha fanikiwa kutengeneza.

Huawei imesema mpaka sasa wapo katika hatua nzuri kuhusu EUV lithography katika vifaa mbalimbali.
 
Mfumuko wa bei Marekani na Ulaya huwa unasabaishwa na bei za mafuta na sera za kifedha/benki sio hizo bidhaa za mchina.
Ndyo maana nakwambia lala kipindi cha trump mfumuko wa bei ulipanda marekani sababu ya tarrif ya bidhaa za uchina haukuwa mkubwa kama huu ila ulipanda kwa kiasi chake yote sababu ya tarrif
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…