Benjamin Mkapa: Natamani kuwe na Tume Huru ya Uchaguzi, Wapinzani wahusishwe kwenye kupiga na kuhesabu kura na kutangazwa mshindi

Benjamin Mkapa: Natamani kuwe na Tume Huru ya Uchaguzi, Wapinzani wahusishwe kwenye kupiga na kuhesabu kura na kutangazwa mshindi

Enzi hizo Ngangari vs Ngunguri.
Jino kwa Jino.
Ukiweka Ugoko naweka njumu.
Pembeni alikuwepo Mzee wa Nditta IGP MAHITA mzee wa FOUR FOUR TWO. ujambazi ukiwa kwenye Chati za juuu kabisa na Msemo MTAJI WA MASIKINI NI NGUVU ZAKE MWENYEWE. Mtutu nje nje daaaah
Tumetoka mbali
 
Aliyewaita wapinzani malofa ni nani,mbona anatonesha maumivu angetulia alee wajukuu ashatuletea majanga atuache tupambane nayo.
Sasa malofa wataruhusiwa vipi kukaa meza moja kuhesabu kura
Neno hilo alipenda kulitumia sana alipokuwa na hasira au kukerekwa na hoja za mtu/watu fulani.
Sio wapinzani tu bali akiwa Ikulu alishawafukuza viongozi wa UVccm akisema "ondokeni sina muda wa kuongea na malofa hapa".
 
Neno hilo alipenda kulitumia sana alipokuwa na hasira au kukerekwa na hoja za mtu/watu fulani.
Sio wapinzani tu bali akiwa Ikulu alishawafukuza viongozi wa UVccm akisema "ondokeni sina muda wa kuongea na malofa hapa".
Akiwa ana hasira hua anatumia neno gani?
 
Hapana tuangalie ukweli anaousema anausema kwa lengo gani.
Ni majuto na kujikosha tu, lakini unabaki kuwa ukweli kwamba tume huru inahitajika sasa na imechelewa sana, na hata kipindi cha uongozi wake ilihitajika pia.
 
Mkapa ni mwana Demokrasia, suala la Urais Zanzibar lina ugumu wake, haliamuriwi tu na Rais wa JMT aliyoko MADARAKANI ila kuna kitu kilichojificha nyuma ya pazia kwa nini Maalim Seif ananyimwa haki zake ....mwaka 2004 nilimskia Mkapa akiwa anahojiwa na DW akisema angefurahi sana kama vyama vya upinzani vingeongeza wabunge wengi katika uchaguzi wa 2005 ..

Pamoja na madoa doa yake katika usimamizi hafifu kwenye mashirika ya umma, lakini kwenye ushiriki kujenga vyama vya upinzani hakuvionea...kipind chake tulikuwa tunaona hata midahalo ya makatibu wakuu wa vyama vya kisiasa ...unafanyika live
Had nitafurahi....ni binadamu pia alifanya makosa mengi katika utawala wako ..
 
Alikukuwa ndani ya box. Ukiwa ndani ya box inje huoni. Unapokuwa nje ya box ndipo unaona.
P

Kwa hakika, ukiwa ndani nivigumu sana kutengenganisha yaliyo tofauti.

Ukitoka nje ndio akili inakuja, ufahamu na hekima.

Umri wa Mkapa umeenda
Hekima
Huruma
Ubabu
Hofu ya Mungu.... je yupo? Kama yupo nikimkuta nini kitanitokea mbele za Mungu?

Mungu anasema nanafsi yake, tuelewe unabii huu wa mzee mkapa

2. H
 
Mahita alimpiga mabomu Mrema pale Moshi wakati wa kampeni. Wakati huo akiwa RPC Kilimanjaro. Mkapa alipoupata Urais, akamzawadia Mahita u-IGP kwa kumpiga mabomu pale Moshi! Nyerere hakupenda kitendo cha Mrema kupigwa mabomu na wafuasi wake eti kwa vile walikuwa wanasukuma gari lake. Sasa hivi Mkapa anajifanya mlokole eti!
Kafika 80yr ndo umri wa kutafakari yote ya dunia ni ubatili, kuukimbiza upepo, yeye ndie aliyewaumiza Sana wapemba wakiwa na comandoo ambae nae Mungu kampiga upofu, kwa kushirikiana na Mahita ndio waliokuwa wakiifurumushia CUF mabomu kila siku
 
Bila shaka naamini kwa Mungu kuna moto na pepo katika madaraja tofauti ...

Kweli mimi ninadhambi na huenda nikaingia motoni ikiwa sinto samehewa na Baba muumba

Ila dhambi za huyu mzee ni za kiwango flani kiasi kwamba ikiwa Baba Mungu atamsamehe dhambi zake kwa kupitia hizi toba za kinafiki majukwaani basi mimi binafsi by default ntapelekwa Katika pepo ya daraja la juu kabisa

I mean by default ntakua nimekolifai Pepo ya festi klasi ase!!!

Huu ni unafiki wa kiwango cha kutokusamehewa dhambi kwakweli hata Utubu kwa kusali masaa 24
 
Back
Top Bottom