Sangamwalogesha
JF-Expert Member
- Mar 10, 2025
- 2,153
- 1,419
Kuna taasisi ipo pale Kilombero jijini Arusha jengo la Summit Centre inaitwa IVOJ inatoa mikopo. Taasisi tajwa ni zaidi ya kausha damu, riba ni kubwa sana, ukichukua Milioni moja unarudisha zaidi ya Milioni moja na laki 8. Mbaya zaidi na kinachodhalilisha wamekusanya kadi za benki za hao wateja wao. Wanabadilisha namba za NMB Mobile au ya Simbamking. Mwisho wa mwezi wao ndio huenda ATM kudraw pesa zote za wateja wanajaza kwenye mabegi, wateja ndio hufuata pesa zao ofisini kwao. Kwenye akaunti ya mteja wanatoa hela yote siyo kwamba hutoa marejesho. Benki kuu muwaambie wananchi huu utaratibu ni sahihi na upo? Taasisi inachukua kadi za benki za wateja na kubadilisha namba za siri,
ndio iende benki kutoa hela kwenye akaunti za wateja na
wawagawie wateja. Kwanini watanzania wanyanyaswe na kudhalilishwa hivi? Nchi hii haina taratibu kwa mujibu wa sheria?
Halafu unaambiwa mwenye taasisi ni mtumishi wa umma anafanya kazi kule Monduli km siyo jeshini ni mwalimu. Ndio kusema na BOT mnahongwa? Akaunti ya benki ni mali binafsi ya mteja wa benki.