HOJA Benki ya CRDB inatuhumiwa kuibia watu hela kwenye akaunti zao. BoT ipo Kimya

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Andikeni barua Kwa waziri wa fedha,gavana wa benki kuu na kama watakaa kimya fanyeni press conference ya vyombo vya habari vya kimataifa
 
Njia nzuri ya kutambua kama kuna mapungufu kwenye akaunti yako ni kufuatilia bank Statements kama anavyosema huyo dada wa mwisho.

Mimi pia nina akaunti CRDB ile ya Tanzanite na huwa wanatuma statements za kila mwezi kupitia email.

Ninachoelewa ni kwamba yapo makato ya aina tatu kwenye akaunti yangu ambayo ni :

1. Maintenance fee Schedule 1,800tshs
2. Makato ya muamala pale unapomtumia mtu pesa. 1,500 tshs
3. Tax 350tshs

Ambazo jumla kwa mwezi ili kuendesha akaunti ni 3,650tshs

Kwa mie wa Ughaibuni naelewa kuwa hizi ni aina ya njia za bank kutengeneza pesa za kujiendesha.

Sasa, kama kuna makato ya zaidi ya hayo hapo juu ni kweli kwahitajika CRDB kutoa maelezo.

Kama yapo makato mengine yalo nje ya mfumo wake wa kawaida zaidi ya makato hayo hapo juu, ni budi yakawekwa hapa kisha CRDB wakajibu tuhuma hizi.

Ushauri.

Jaribu sana kutotumia PIN pale ambapo watambua kuwa una changamoto ya kumbukumbu maana ukifanya jumamosi au jumapili au siku ya sikukuu tambua kuwa kadi yako itamezwa na utaipata jumatatu.

Ukiona kama kuna changamoto bas jaribu mara kwa mara kutumia njia ya wakala au kuingia bank mwenyewe utoe pesa.

Hata hivyo kuhusu wizi hilo ni jukumu la CRDB kuja hapa kutolea ufafanuzi kuhusu hlo.
 
Nina akaunti NBC na crdb tangu 2005 mbuzi wewe,na chuo nilisoma biashara
Bank gani hiyo tz haina makato ya mwezi?
Sasa ukiwa na accout NBC na CRDB ndo inakufanya una-draw conclusion dunia nzima kwamba: kila benki inakata monthly maintenance fee? Kama chuo ulisoma biashara na hauelewi 'freemium business model ni nini?' basi rudi kusoma chuo upya, kwa sababu elimu bado hajakupa maarifa ya kutosha.
 
1. Maintenance fee Schedule 1,800tshs
2. Makato ya muamala pale unapomtumia mtu pesa. 1,500 tshs
3. Tax 350tshs
Sasa hivi watu wameongezeka. Gharama inatakiwa zipungue. Halafu fee ya kila mwaka inafanya kazi gani hadi tukatwe kila mwezi.

Hayo makato wamekubaliana na nani?

Wanipigie simu niangalie kama naweza, kama siwezi nifunge account.
 
Siyo kweli mimi hicho kitu hakijawahi kutokea na sometimes nakuaga na Balance hadi ya 100m hapo kuibiwa 70k si ndiyo rahisi zaidi? Tafuteni pesa jamani siyo kuangalia Salio kila sekunde 30
Wewe account yako haina kitu bwabwa Wewe endelea kukata viuno CCM kwa buku 7
 
Sasa hivi watu wameongezeka. Gharama inatakiwa zipungue. Halafu fee ya kila mwaka inafanya kazi gani hadi tukatwe kila mwezi.

Hayo makato wamekubaliana na nani?

Wanipigie simu niangalie kama naweza, kama siwezi nifunge account.
Mkuu, mie sitabisha sana maana kila mtu ana madai yake lakini baada ya malalamiko kama haya, itabidi kila mteja arudi tena kwenye ile T&C alosaini wakati wa kufungua akaunti.

Kama hayo makato hayamo humo au kuelezwa yatatokea basi hiyo itakuwa dhahiri kuwa ni wizi.
 
Wewe account yako haina kitu bwabwa Wewe endelea kukata viuno CCM kwa buku 7
Najaribu kuscreen shoot inashindikana siku hizi Simbanking wameboresha nilitaka nikulize japo nimeingiza kwenye mzunguko kama 70m lakini si haba
 
Siku niliyoona hako ka-CEO kao kafupi fupi kanahudhuria mikutano ya chama Dodoma nilijua tu hiyo benki haipo salama. Benki kuu siku hizi pana vibaraka wengi sana na watu wenye uwezo mdogo sana sidhani kama wanaweza kufanya chochote.
 
itabidi kila mteja arudi tena kwenye ile T&C alosaini wakati wa kufungua akaunti.
Kutokurudi kusoma sio sababu ya kukatwa hela. Mfano mimi nimejiunga CRDB 2002 hata sikua na simu, ila sjawahi kuisoma hiyo T and C.

Wao walitakiwa wawe wanatujulsha kwa meseji miezi 6 kabla ili kama mtu hutaki ufunge account.

Kwani Anuani, Email na Namba za simu tunawapa za kazi gani? Kwanini wasitumie kutujulisha makato kabla.

Mimi wanajulishe kwa barua ili niweze kuwashitaki.

Kwahiyo wamekuambia watatoa ufafanuzi au hawatoi?
 
Bank bhana nilipokua nafanya biashara ya mitumba nilikua napeleka hela bank ya nyumba niliona kama bank ya posta na wengine ni waogo aisee kuna siku naenda pale Bank ilikua ipo Forest ya zamani Mbeya hapo naambiwa bank imefirisika kinachotokea hapa hatuwezi kukupa hii pesa tutakupa wateja wakija kuweka ndio upewe na za kwako watu walipogundua bank ni wahuni wakaacha kupeleka pesa nikawa naenda kila siku kuuliza kama nataka kukopa jamaa walinichanganya sana baadae wakaja kutulipa kwenye jengo iliyopo TRA Mbeya tena nilimuagiza Mama nenda kachukue maana nilikua nishaikatia tamaa na mimi nishaanza mishe zingine toka hapo haya Ma bank naona kama wahuni wahuni fulani tu ingawaje nafanya nao kazi sana maana hakuna namna kipindi hicho nipo shule huku nauza nguo Docks Mwanjelwa hapo ilikua Tsh 750,000 siji kusahau ila ilinitesa sana na kubadili mfumo wangu wa kazi kabisaa..
 
Hii bank ni changamoto nakumbuka mwaka 2016 walinikata kama laki3 pasipo msingi wowote na nilikuta natoa Hela bila kucheki balance siku nacheki balance ndio mzozo binafsi ulianza.

Nilifika geto nikarecall miamala yote niliofanya nikapiga total nikafananisha na balance nikaiona hiyo loss. Nikarudi branch pale mbezi mwisho nikatoa maelezo wakaniambia hela imekatwa kwasababu nilifanya malipo ya online.

Ni kweli nilishawahi kuomba kadi yangu iwezeshwe kufanya miamala ya online lakini walinigomea na ilishapita miezi kama mi3. Niliwaka sana pale mapokezi yule dada akaniambia niandike barua, nikaandika palepale lakini ile barua haikufanyiwa kazi kwa zaidi ya wiki3. Kuna siku nikaenda akanijibu bado halijafanyiwa kazi, nikamuuliza nije lini mtakua mmelifanyia kazi? Akaniambia siku Fulani. Nikaenda kurudi hiyo siku bado halijafanyiwa kazi nikamuuliza meneja yupo nimuone? Dada akapata kigugumizi akaniuliza unataka Nini? Nikamjibu namtaka mtu anayeweza kunipa majibu ya Hela yangu imeenda wapi.

Bhasi yule dada bila hiyana akaniandikia barua nifike main branch Azikiwe, nikaenda kule nikamfuata meneja directly na issue yangu ikawa solved ndani ya nusu saa.

Niliamua kufunga akaunti 2017 baada ya kuona Kila nikifanya miamala wananikata 20k mpaka 30k alafu Haina sababu yoyote.
 
Mkuu, mie sitabisha sana maana kila mtu ana madai yake lakini baada ya malalamiko kama haya, itabidi kila mteja arudi tena kwenye ile T&C alosaini wakati wa kufungua akaunti.
Kipindi kile unaleta hapa Jamiiforums mamalamiko yako kuhusu CRDB tulibeba jambo lako kama jambo letu. Leo hii wenzako wanapata shida unawaambia warudi kusoma T&C. Je, wewe ulipoleta mjadala hiyo T&C ulosaini hukuiona?
 
Kipindi kile unaleta hapa Jamiiforums mamalamiko yako kuhusu CRDB tulibeba jambo lako kama jambo letu. Leo hii wenzako wanapata shida unawaambia warudi kusoma T&C. Je, wewe ulipoleta mjadala hiyo T&C ulosaini hukuiona?
Na mie wakati ule sikusoma uzuri hizi T&C lakini baada ya kurudi na kuzisoma nikaona kwamba ni kweli nilihitaji kusoma T&C.

Hata nilipofuatilia hizo 400 nikaambiwa nifungue akaunti ingine kwani ile ilikuwa dormant kwa muda fulani.

Hivyo tokea pale nafuatilia makato kwa kusoma bank stetements na pia nina online access na hakuna shida.

Lakini kiukweli pia nina akaunti Stanbic ambayo ni ya fedha za kigeni tu.

CRDB ni tanzanite kutoka ile waloimeza na 400
 
Siyo wewe tu maandishi huwa ni Madogo halafu mengi ukisoma mstari mmoja tuu una sign
 
Taja bank Tanzania ambayo haina makato ya mwezi nikaweke hela
 
Taja bank Tanzania ambayo haina makato ya mwezi nikaweke hela
Wadau wamezitaja hapo. Halafu haya mambo ni uelewa tu. Account zipo za aina nyingi, kuna account ambazo mandate zake zimeelekeza kwamba hazina makato ya mwezi. Chunguza vizuri, kwa sababu we ndo unabisha. Ukipata majibu rudi hapa.
 
Wadau wamezitaja hapo. Halafu haya mambo ni uelewa tu. Account zipo za aina nyingi, kuna account ambazo mandate zake zimeelekeza kwamba hazina makato ya mwezi. Chunguza vizuri, kwa sababu we ndo unabisha. Ukipata majibu rudi hapa.
Akaunti maalum siyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…