HOJA Benki ya CRDB inatuhumiwa kuibia watu hela kwenye akaunti zao. BoT ipo Kimya

HOJA Benki ya CRDB inatuhumiwa kuibia watu hela kwenye akaunti zao. BoT ipo Kimya

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Siyo kweli mimi hicho kitu hakijawahi kutokea na sometimes nakuaga na Balance hadi ya 100m hapo kuibiwa 70k si ndiyo rahisi zaidi? Tafuteni pesa jamani siyo kuangalia Salio kila sekunde 30
Hapo 100m tu unasema tutafute hela daah..
 
Sii kwamba watu hawazijui hzo foreign banks hapana ila watu wanataka assurance ya pesa zao in case anything happens. Mfano leo hii hyo equity ikatangaza kufirisika au ikafungwa gafla kama zilivofungwaga baadhi ya banks kipindi cha magufuli je ww mteja utaenda china kudai pesa zako?
Ni uoga tu usio na maana ,kwani unafikiri nmb au crdb hao vibAka wakifirisika mtalipwa pesa ? vibAka wanaoiba pesa za watu
 
CRDB kuna wafanyakazi wadokozi wengi wanaojichotea pesa kidogo kidogo zilizoko kwenye akaunti za watu, hasa zile zisizokuwa na miamala ya mara kwa mara.

Hii tabia niliiripoti miaka miwili iliyopita baada ya akaunti yangu kukatwa shs 15000 bila maelezo yoyote tena bila kuwa na deni.

Nadhani ujio wa ile falsafa ya Kizimkazi ya kuruhusu kula kwa urefu wa kamba imeeleweka vizuri CRDB.... Yoour berra woch uaar bak!! 😳
 
wanakupa kadi wapi
Ukiwa inafanya miamala wanakupigia simu kuuliza kama wakutengenezee kadi, ukikubali wanakutengenezea unaenda kuchukua kwenye moja ya vitu vyao. Ila mimi binafsi sina kadi, nikitaka kufanya miamala ya kawaida nanunua tu bundle lao la buku.
 
Pia ukiachana na bank charges kuna VAT na Service Levy kama deductions especially account za makampuni, na hizo VAT wamiliki wengi wa makampuni hawazi-claim kama inputs sababu ni amounts ndogo ndogo na wengine hawako makini nazo.
Nashangaa watu wanalialia,walifikiri bank ni vibubu vyao nyumbani?
 
Mimi wananikata Milioni 2 kila siku ila nimemuachia Mungu... Hawana huruma kabisa hela yenyewe naipata kwa kuchimba mitaro..
 
Pia ukiachana na bank charges kuna VAT na Service Levy kama deductions especially account za makampuni, na hizo VAT wamiliki wengi wa makampuni hawazi-claim kama inputs sababu ni amounts ndogo ndogo na wengine hawako makini nazo.
Mimi nilijua watu wanaweka hela bank ili bank izifanyie biashara na kupata faida ya uendeshaji
Nikimaanisha makato yapo ila yangetokana na faida wanayopata kwenye biashara ikiwepo ya kukopesha ambayo ina riba kubwa tu (kati ya 12%- 18% hivi)
Kwa maana hiyo; ukiweka milioni 20; baada ya miaka miwili nilitegemea ukute basi milioni 20 na sio 19 na laki kadhaa. Hii ndio inafanya watu wafikiri kuwa, matumizi yao ni makubwa kuliko biashara wanayofanya (WANAKULA MTAJI)
 
Mimi nilijua watu wanaweka hela bank ili bank izifanyie biashara na kupata faida ya uendeshaji
Nikimaanisha makato yapo ila yangetokana na faida wanayopata kwenye biashara ikiwepo ya kukopesha ambayo ina riba kubwa tu (kati ya 12%- 18% hivi)
Kwa maana hiyo; ukiweka milioni 20; baada ya miaka miwili nilitegemea ukute basi milioni 20 na sio 19 na laki kadhaa. Hii ndio inafanya watu wafikiri kuwa, matumizi yao ni makubwa kuliko biashara wanayofanya...
Hapo ni hadi iwe fixed account mkuu, ikiwa ni current account lazima zikatwe.
 
Kila bank ina makato ya mwezi, duniani kote
We unamiliki account kwenye kila benki duniani? ama ni assumptions? unajua madhara ya ku-assume? zipo benki hazina model ya kutengeneza revenues kupitia account fees. Tena zipo nyingi tu, tena ukianzia hapa Tanzania kabla hujaenda nchi kama India
 
Huu uzi umenifanya nifanye udadisi kidogo kwenye account yangu kuhusu makato mbalimbali ya transaction nilizofanya kwa mwaka mmoja yani Nov 2025 mpaka nov 2026....
Nadhani nikifanya tangu nimefungua account 2006 mpaka sasa naweza kupata kapresha kidogo😀

Kwa jumla ya miamala 80 kama wastani kuna makato 200+ ambayo yanakuja jumla ya Tshs. 454,103.42. Chini ni ambatanisho la screenshot iliyoniletea jumla.

Sasa nimejaribu kufanya comparison na ECObank ambayo huwa natumia mara kwa mara mfano ukituma hela kutoka ecobank kwenda bank nyingine makato ni 1,770 haijalishi kiwango. Ila jamaa zangu hawa ni ukituma mfano 5m jua utakatwa zaidi ya 7000 kuendelea.
Sasa sielewi hizi bank nyingine zinawezaje kuwa na makato madogo ila hawa wanashindwa....

Tatzo kubwa la mfano ecobank ni kutokua na option ya malipo ya serikali kwa baadhi ya sekta....

Anyway tuendelee kupenda vya nyumbani NMB! CRDB! NBC MCB n.k
 

Attachments

  • IMG-20261101-WA0016.jpg
    IMG-20261101-WA0016.jpg
    167.1 KB · Views: 1
  • IMG-20261101-WA0016.jpg
    IMG-20261101-WA0016.jpg
    167.3 KB · Views: 1
We unamiliki account kwenye kila benki duniani? ama ni assumptions? unajua madhara ya ku-assume? zipo benki hazina model ya kutengeneza revenues kupitia account fees. Tena zipo nyingi tu, tena ukianzia hapa Tanzania kabla hujaenda nchi kama India
Nina akaunti NBC na crdb tangu 2005 mbuzi wewe,na chuo nilisoma biashara
Bank gani hiyo tz haina makato ya mwezi?
 
Back
Top Bottom