Uchaguzi 2020 Bernard Membe: Nitagombea Urais Upinzani ukinipa ridhaa


Hata wangetaka kuungana, hilo kwa sasa haliwezekani maana muda wa kisheria umeshapita.
 
Nitashangaa sana endapo upinzani watamchukua Membe kama mgombea wao. Watakua hawakomi hawa. Wanasahau kuwa Membe ni shushushu mbobevu.
 
Siasa za bongo bwana" Nyumba ajenge Mbowe kuhamia ahamie Membe"
 
Eti vyama vikiungana kumpitisha atagombea, Chadema ingieni tena kwenye huu mtego halafu mtakipata fresh
 
CCM hawaminiki,,,mkijua Lowasa yupo wapi basi hamtafanya kosa tena,,Lissu Anatosha ,,,,Kama upinzani WA Nchi hii unategema Makapi ya CCM ndo yawe presidential material of all time basi tutasubiri Sana!.
 
Nilikuwa na mawazo haya 2015 na niliwachukia Sana Cdm na Lowasa na nilimpigia Magu kura lakini sasa naona nilikosea Sana.
Swala kuu 2015 lilikuwa mabadiliko ina maana tumeridhika? Nadhani issue ni kumchallenge Magu ambaye ameshajisahau sana tofauti na wakati anapiga kampeni 2015.
Kwa hiyo ni muhimu kumtumia mtu yeyote mwenye uwezo wa kuthubutu kung'oa huyu jamaa.
Kuna wale wanasema Lowasa alipandikizwa!!! Ina maana Lowasa alikuwa hautaki urais? Lowasa alikuwa serious kuchukua nchi. Kama ni makosa ya kumpokea Lowasa yalishafanyika hata kumkataa Membe haitasaidia.
 
Magu lazima awe challenged .
2015 alisimama kunadi ilani ya ccm na akashinda Hawa watu wote waliopotea na akina Lisu ni kwa kiasi gani walikuwa wanamnyima kutekeleza aliyoyaahidi?
Nchi hii tuna mifumo mtu akikosea tuna mahakama kwa Nini uumize watu kwa kudhani tu kwamba wametumwa na mabeberu.
Kama wanankosea tuna mahakama. Mimi hiki kitu Cha watu kupotea kimeniuma Sana. Huwa najaribu kukaa kwenye nafasi ya walioumia nasononeka Sana.
Lazima tujenge siasa za kujali utu hivi vitu tunavyojitamba vimefanyika havina dhamani ya Maisha ya watu.
 

Mkuu hakuna anayemkataa Membe kuja upinzani, ila aende TADEA achukue fomu. Hayo mambo ya wanaccm kusubiri miezi mitatu kabla ya uchaguzi kisha kuingia upinzani, na wao kutaka kugombea urais sisi sio wapinzani wajinga wa hivyo. Huyo Membe adai tume ya uchaguzi kwa nguvu zake zote, ila sio kutaka kugombea urais.
 
Hakika. Umenena maneno ya upako.
 
Tatizo hawataki kujitolea lakini ni upi uamuzi sahihi kwa awakati huu?
2015 ilibaki kidogo hii nchi ikombolewe japo Lowasa alipokewa kimakosa lakini ukombozi ni ukombozi.
Kwakweli Hawa wazee uzalendo hawana kabisa hawataki kujitolea hata kwa kuwa washauri wa kuweka mikakati.
 
Akiulizwa swali la kichokozi na muandishi wa BBC Ndugu Benard ameeleza wazi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi mkuu anayo haki ya kuamrisha vyombo vya ulinzi na Usalama ,kuelekeza na kuvitaka vifanye nini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…