Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Salaam Wakuu,
Leo Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Ndugu Bernard Membe anaongea na Wahariri wa Vyombo vya habari Jijini Dar.
Nipo hapa City Lodge Mjini kati kusikiliza kile atakachoongea niwajuze.
Taarifa zote zitapatikana kwenye hii thread.
Stay tuned.
=====
UPDATES: 1048HRS
Wanahabari Washafika eneo la tukio
UPDATES: 1100HRS
MEMBE ANASEMA:
Nimewaita kupitia ninyi niongee na Watanzania.
Wengi wameuliza Membe yupo wapi? Au kaunga mkono Juhudi, au kaondoka chama?
Mimi Membe ni Mgombea Halali wa ACT Wazalendo. Ni chama chetu kizuri na nitakipeleka kwenye Uchaguzi wa Mwaka huu kama Mgombea wa Urais.
Kuna watu walikuwa wanasubiri nitamke tu neno ila mambo yatimie.
Mimi hupenda kujibu Maswali.
Hapa nimekuja na Omary Faki Mgombea Mwezi kutoka zanzibar na Meneja Kampeni wa Urais wa ACT.
Ipo nadharia kwamba Vyama vikiungana vinaweza kushinda. Lakini katika bala la Africa, nadhalia hii haijawahi kufanikiwa.
Madikiteta wote wameangushwa na vyama binafsi. Afrika chama kimoja ndo huwa kinashinda sio vilivyoungana.
Vyama 19 bara la afrika vya Ukombozi, vyama 13 vimeshaondoka. Vimeondolewa baada ya vyama vyenyewe kujitafuna na kuwa na mpasuko na vyama vya upinzani vikachukua advantage.
Ili chama Tawala kife, kinatakiwa kipasuke kwanza.
Nadharia ya chama Tawala kupasuka, imeshakomaa Tanzania.
Chama Tawala cha CCM tunakiangusha Mwaka huu kama tutafanya haya nitakayoyasema.
Nini maana ya kupasuka kwa chama. Ni hadi wanachama waseme tumechoka. Angalieni wakati wa kura za maoni za CCM,watu walienguliwa. Sisi ACT tulipokea Applications 42 za kuomba kujiunga na sisi. Sijui walioenda vyama vingine.
Baada ya kura za maoni Bashiru akaanza kuwaahidi kwamba watapewa vyeo watatumbuliwa.
Mimi nlikuwa na wabunge 78 wa CCM, 46 Wamefyekwa na 23 bado wamo CCM. Siwapi majina
Mimi nlijipanga na wenzangu sita ili kushindana na Magufuli, mimi nlikuwa tayari kumkabiri kwenye Uchaguzi na bahati yao walinifukuza.
Hata chama Tawala mambo yanapoharibika wanakimbia. Lazima wapewe sehemu ya kutokea. Anaweza akachagua chama cha kujiunga.
Tunachotaka sisi ni kukipasua chama cha CCM na kimeshapasuka. Sasa aje mtu mwenye nguvu aingie madarakani.
KUSUDIO LANGU
Ndugu zangu watanzania, tumepata tabu sana. Tumepiga kwelikweli. Sasa hivi Tanzania ni Fukara, Watanzania hawana fedha. Dunia haiishi hivi. Dunia ina fedha. Sisi tumerudi miaka ya 80. Serikali haitumii fedha sababu haina kwasababu imekopa sana.
Dunia nzima Serikali ndo tajiri wa kwanza na kuzisambaza. Ukiona nchi haina fedha wa kuajibishwa ni serikali. Serikali ndo mwajiri Mkuu.
Mtu mmoja anasema sasa kama mimi nina fedha kwaninii nikope?
Kopa ulipe kidogo kidogo. Ukienda kununu vitu kwa fedha yako ili uonekane una hela jua unafukarisha Serikali yetu.
Rais aje awe Mimi au Tundu, kazi kubwa itakuwa ni kulipa Madeni. Na mashitaka yote tutakayodaiwa itabidi tulipe.
Tusidanganyane, Serikali hii haona fedha. Tuna ufukara. Na ufukara huu ndo unaofanya watu wakati wa Uchaguzi, Ukichanganya ufukara huu na hasira wakati wa Uchaguzi ndo unawasha moto.
Mimi nmesimamia uchaguzi 19.
Ukichanganya hasira ya kunyimwa haki ukajumlisha na Ufukara walionao ni fujo. Na haya mazingira tumeyatengeneza.
Kwani hatuna njaa? Siku hizi chakula chetu ni mihogo na madafu.
Pale kariakoo unakuta asubuhi anakunywa kahawa, mchana hadi jioni.
Watu wanakula mihogo mibichi na iliyoiva. Wanasisinzia hovyo hovyo
Jana saa nne usiku nimetembelea hotel za dar. Zote ni kiza, hakuna watu.
Jana nmeenda kariakoo nikiwa nmevaa kanzu. Zamani tulikuwa tunaingiza 90 bilioni kwa wiki. Nenda sasa hivi, inatisha. Fremu nyingi sana zimefungwa.
Mtu anasema ukiingia kariakoo na vazi la CCM hawakufanyi kitu kama zamani.
Hawafanyi hivyo sababu wanakuoenda bali ni uoga. Watu hawapo huru.
Uchaguzi huu tuwe na haki. Waangalizi kutoka nje watakuwa wachache. Wale wakubwa wakubwa hawaji. Hawaji sababu wanajua bado kuna COVID-19. Pia UNDP haijatoa fedha sababu Serikali ilikataa fedha za uchaguzi na kwanini walikataa? Muwaulize nyinyi.
Ila wanatakataa sababu ukipokea fedha za UNDP shariti namba moja ni lazima walete international observers. Hawa waliokuja ni Mabalozi na Wafanyabiashara.
Tutakuwa na observers.
Uchaguzi huu lazima itendeke haki.
Pale Zanzibar wanachodai ni haki.
Zanzibar wapo laki nne na sitini elfu tunapiga siku mbili lakini wenzetu wapo Milioni 29 wanapiga siku moja.
ACT wanalalamika kwanini tunaoewa tarehe mbili za Uchaguzi? Ndo maana Maalim seif akafungiwa.
Hatujachelewa kuepusha maafa Zanzibar. Mimi nliona maafa mbele ya Macho yangu Zimbabwe. Ilikuwa hivi hivi kupiga kura mara mbili.
Zimbabwe 2013 walipiga siku mbili ikatokea vita, mwaka 2018 wakapiga kura mara moja.
Zanzibar wameiga hii ya kupiga kura mara Mbili Zimbabwe.
Mimi kama mwanasiasa mbobezi, nawashauri Zanzibar kura ipigwe mara moja.
Wanasema tarehe 27 ni ZEC na tarehe 28 NEC. watu wanahoji, mbona zamani tulikuwa tunapiga kura siku moja?
Ili kukwepa fujo, tuache kupiga kura mara mbili.
Hakuna kitu kibaya kwenye Uchaguzi kama Ukabila na dini.
Nawaomba sana viongozi wetu wa dini, watuunge mkono kimya kimya, wakiendelea kutangaza hadharani, wataingiza nchi kwenye Vita za kidini.
Kama mwanasiasa mbobezi, nawaomba Viongozi wa dini msituongize kwenye vita ya Ukabila na udini.
Kazi ya Viongozi wa dini ni kuhubiri haki amani na Utulivu. Kazi yao ya pili ni kuombea Taifa.
Viongozi wa dini tusiaidieni kuliombea Taifa. Tusihubiri amani na Utulivu bali tuhubiri haki.
Nmefanya utafiti na wenzangu, tumeviona viashiria vya kuwepo machafuko.
Sasa sisikii ile lugha ya tunatest mitambo, mitambo gani? Mitambo yenyewe ishaharibika.
Sisikii ile lugha eti tutashinda asubuhi. Watu wapo kimya kama vile hakuna uchaguzi. Kule mikoani wapo kimya kabisa.
Chama cha mapinduzi hakina fedha. Ndio maana wanaahirisha kampeni. Hivi hamjui kwamba kuna watu wanakidai chama cha mapinduzi tangu 2015? Na hawa wasanii Uchaguzi ukiisha utaanza kusikia naidai CCM.
Nawaomba viongozi wa Dini msiingie kwemye mitego. Tupigieni michepuo chini chini mkienda huko juu mtachafua hali ya hewa
Tulipokonywa Uhuru miaka mitano iliyopita. Jana nlikuwa na sikiliza rais kwenye taarifa yake kwa vyombo vya habari. Clip ya kwanza inazema Waandishi wa habari nipo na ninyi mtakuwa na uhuru clip ya pili inasema Ole wenu.
Wandishi wa habari Mkiogopa mumekwenda na Maji. Unganeni muwe kitu kimoja kuisemea Nchi
Katika Serikali yetu hatuingilia vyombo vya habari.
Sasa hata mabaya yakitokea nchini vyombo vipo kimya.
Wafanyabiasha wakubwa zaidi ya 100 wamefunga biashara. Sasa hivi wafanyabiashara wapo India Mombasa, Lusaka afrika kusini. Kinaniuma ninavyoona hela zilizokuwa zinakuja Kariakoo zipo Lusaka.
Tukiingia Madarakani tutawashawishi warudi nchini.
Wale sio watu wa kudhalilishwa. Ila ni kukaa nao na kuongea
1. Uhuru, Biashara, Kilimo.
Bei ya korosho pamba tumbaku mbaazi sio serikali kuingilia bali iamuliwe na Soko.
Wananchi waambie Bei elekezi ya duniani.
Sisi swala la ajira tunalipa kipaumbele..
ACT tumeweka mbele mambo ya afya. Bima ya afya ya sasa ina ubaguzi
Sisi ACT theluthi mbili itatoka serikalini. Kila watu walipo elfu moja tutajenga Zahanati
Sasa Tanzania imekuwa kisiwa cha mafukara. Haina mahusiano mazuri na Dunia na jumuiya ya kimataifa sababu tumejitenga.
Sisi nchi yetu bado ni fukara. Tuna utajiri ambao upo Kilometa sita kwenda chini ya ardhi.
Tulileta uwekezaji wa bandari ya Bagamoyo, Serikali ya awamu ya tano ikakataa eti ni ina Mkataba mbaya..
Bagamoyo inaleta meli kubwa inabeba makontena milioni moja na laki nane.
Anadai eti watu wakubwa wamegawana.
Stiegler's gorge sasa kimyaaa.. Wakati zile hela tungezipeleka kwenye gesi.
Sio vibaya kujenga miundombinu. Lakini wewe usiwe rais wa miundombinu kama nyuki. Nyuki ndo kila siku asali.
Rais anataka azitendee Wizara zote 27 sawa. Sio kwenye miundo mbinu tu
Nyuki angegombea urais kwenye animals kingdom tusingemchagua. Nikuchague wewe unatengeneza asali asubuhi hadi jioni? Hapana.
Watanzania mkae macho na mkae chonjo. Nafunga bao la Ushindi dakika ya 89. Hiki ndicho kitakachotokea.
Huku chini tumeshamaliza tunakuja huku juu sasa.
Bao la dakika 89 linakataliwa? Kutoka benchi hadi bao dakika ya 89.haya ndo maajabu ya Uchaguzi wa Mwaka huu.
Ndani ya ACT WAZALENDO hatuna ugomvi. Nawaombea kur Wagombea Ubunge na Madiwani. Tunamuunga Mkono Maalim Seif.
Siku ya tarehe 29 Maalim Seif atakaa chini huku anakunywa dafu halafu afungulie radio asikilize ushindi wake unavyo tangazwa.
Hatuwezi kufua nguo za ndani mbele za watu.
Nitajitahidi kufanya kila linalowezekana kuishauri nchi tusiingie kwenye majanga na udini.
Watanzania wote twendeni tukapoge kura.
Naiomba Serikali itumie haki. CCM itumie haki, pale inapoona imeshindwa wasimame pembeni.
Tukishindwa mwaka huu kubadilisha uongozi wa CCM ni kwa sababau hatukujiandikisha au kwenda kupiga kura.
Msikubali kuuza vitambulisho vyenu.
Msikubali kuharibu kura zenu.
Sisi ni watanzania. Haki ikitendeka amani na utulivu vitakuwepo. Tusilofikishe taifa letu mahali pabaya. Haki itawale. Kura zihesabiwe wazi wazi na matangazo yatolewe kwa haki ya Mungu.
Sisi ni Watanzania. Watu wa dini watuunge mkono chini chini na kimya kimya ili Nchi yetu isimeguke
=====
ANAJIBU MASWALI
Kwanini hamtaki Zanzibar ipige kura mara mbili?
Membe: Mwenyekiti wa ZEC alisema ikitokea aliyetakiwa kupiga kura tarehe 27 akashindwa, anaweza kupiga kura tarehe 28. Hii ndo inaleta utata. Kuna uwezekano wale walioshiriki uchaguzi wa ZEC tarehe 27 akafanya Uchaguzi wa NEC tarehe 28.
Kwani kuna utafiti ulifanyika kwamba watu wanachoka kuoiga kura siku moja?
UNDP inasiaidia Uchaguzi Marekani? Kwani tukifanya kwa hela yetu kuna kosa?
Membe: UNDP ipo kwaajili ya nchi zinazoendelea. Tunachangia sababu sisi ni wajumbe na wanachama. Ni haki yetu kupata hela ya UNDP. Tume ya Uchaguzi ina ukata. Nchi zote zinapata hela za UNDP.
Mbona umejificha?
Nmejificha Rondo toka mwezi Machi baadae nikaja Dar.
ACT haina Ruzuku, ni chama kipya. Kwanza tuwapongeze. Nina uhakika uchaguzi ujao titavuna viti vingi. Kunakiwa na matatizo ya kiutawala, logistics, matatizo nk. Tumesimamisha Wabunge 120, walikuwa 140 wakang'olewa. Sikuishiwa sababu ya familia yangu bali nmeishiwa sababu ya chama tunachokipenda. Tupo tayari tuuze miwani ili wagombea wetu washinde. Vyama vingine visione aibu kisema vyama havina hela.
Bora ufanye Uchaguzi nanufukara kuliko mabilioni ambayo huna taarifa ya ulipo yatoa. Kilicho kizuri kwenye uchaguzi ni Afya na Sera.
Msione haya kusema hamna fedha. Sababu nchi hii hata makampuni hayana fedha sembuse Membe, sembuse ACT.
Hapa tunakula mihogo, senene au kahawa asubuhi na jioni.
Zitto na Seif wamesema watampigia kura Tundu Lissu, wewe unagombea ACT. Unasimamia miguu ipi?
Membe. Sisi tupo wamoja hatuna mgawanyiko. Chama cha ACT kina mgombea anaitwa Bernard Membe. Mimi nipo namba tisa kwenye karatasi ya kura. Waliosema ni individuals sio chama. Wqpo watu ndani ya ACT hawatampigia kura membe na Wawili wameshasema na wanaweza kubadili gia angani.
Kura za Wananchi ndo tunazozitafuta
Mgombea mwenza: ACT tunalalamika kura ya mara mbili sababu hao wanaopiga kura tarehe 27 watatakiwa kurudi kupiga kura ya NEC tarehe 28. Ndo maana tunasema waje tu tarehe 28. Sababu yarehe 27 watapiga kura za ZEC tu. Watu wanaotegemewa kupiga kura tarehe 27 ni kama elfu saba. Wanaopigwa kura tarehe 27 ni wale wasimamizi wa Uchaguzi na vyombo vya Ulinzi wa Usalama.
Hii pia inaongeza Usumbufu kwa wapiga kura. Sababu anapiga mara mbili
Hadi leo daftari la wapiga kura halijatoka.
Wanasema masanduku yatahifadhiwa halafu kura zitaxhanganywa na kura za tarehe 28. Sisi hatuamini
Na sisi tumewaambia Wanachama wetu waende kupiga kura tarehe 27.
Ulivyotoka Dubai Ulitaanza kuunguruma kutokea Tabora. Tarehe 15. Ilikuwaje?
Nlipotoka Dubai, Msaidizi wangu alikamatwa. Nlisubiri kimaliza shughuliza za msaidizi wangu ziishe na kusawazisha kauli tata.
Unaposema tumekopa sana una maanisha nini? Tafiti za IMF zinasema tunafanya vizuri Afrika mashariki.
Membe: Je, wewe unasemaje, Tanzania ina fedha?
PORTFOLIO ni fedha zinazotolewa Tanzania. IMF inaangalia ulipaji wako.
BoT ripoti ndo inaonesha kipato chako kwa mwezi.
Serikali haina fedha sababu ina mikopo mingi.
Watu hawapewi fedha za likizo, watu hawaongezewi mishahara kwanini? Sababu Serikali haina fedha
Swali: Tutarajiwe kukuona kwenye majukwaa?
Swali: Ni muujiza gani utaufanya dakika ya 89?
Wakati ukitangaza Kujiunga upinzani ulisema utakuwa tayari kumuunga mkononMgombea wa upinzani atakayekuwa na nguvu. Je wewe una nguvu kuliko Lissu?
Madeni ambayo yameongezeka ulikuwa huko, je Ulishauri nini?
Umefanya mikitano mingapi hadi sasa?
Unawasemaje Magufuli na Lissu?
Umeapa hurudi CCM je wakikuofa utakataa?
Wewe kama kachero Mbobezi, una viapo. Je umevikiuka?
Membe: Nikiambiwa nirudi CCM siwezi kurudi. Mimi nlikuwa nimkabiri rais huyu ndani ya chama wakanifukuza. Wangeona vumbi lenyewe.
- Kama kachero mbobezi nina viapo ambavyo sijavivunja. Nikivunja hapatakalika.
- Nmefanya Mikutano Majimbo, kitaifa, kimya kimya, sina idadi. Ya majukwaani nmefanya sita ya Public.
- Sio Lissu na Magufuli tu. Tupo 15.
- Mimi nIlikuwa Waziri wa mambo ya nje. Baraza la Mawaziri linajadili. Ni mgawanyo wa kazi. Rais, waziri wa fedha, na waziri wa mambo ya nje. Waziri akisaini Mkopo sio Membe tena bali Serikali. Madeni yanarithishwa.
- Nlitangaza nimeingia ACT Wazalendo. Sasa ni mshauri mkuu wa CHAMA. Ukishakuwa mteule wa Urais, kisheria hairuhusiwi kuseme unamuunga mkono rais fulani wakati na wewe ni mgombea wa huo urais. Ukisema hivyo unatakiwa upelekwe Milembe
Leo nitatweet kueleza jinsi nitakavyorudi kwenye majukwaa.