Uchaguzi 2020 Bernard Membe: Watanzania mkae macho na mkae chonjo. Nafunga bao la Ushindi dakika ya 89 kwenye Uchaguzi huu 2020

Ukienda na nakala ya hii hotuba ya Kachero pale Finca, Bayport, Tunakopesha ltd etc unachukulia mkopo bila mizengwe!

Porojo zipo kiasi pia like hapo kwa wabunge 78, dakika ya 89 etc lakini madini ndio yametamalaki.

BTW: Mbona hawajamuuliza kuhusu wale maadui zake 12 alioahidi kuwahamishia Kenya?

Kwangu hii ni Hotuba bora kabisa kwa mwaka huu!

Ila inaonesha kuna shida ndani ya ACT likely "Mwanawachu"&Co wamemsusia mbobezi baada ya kukaidi kumuunga mkono wamtakaye wao.
 
Membe ni kiazi, tena kiazi mviringo
 
Ninachokiaona Membe amejaribu kukwepa mishale ya NEC, kama angesema anamuunga mkono Lissu huwezi kujua NEC wangesema nini. To me he is smart guy maana ni mgombea gani asiyefanya kampeni!!
Wewe uko njema upstairs
 
Kumekucha sasa. Wana ACT sijui washike lipi sasa!
"Hatufui nguo za ndani hadharani" hii lugha ni ngumu kuielewa. Membe anatumia lugha ngumu sana kueleweka. Wana ACT wakimsikiliza Zitto na Maalimu Seif watawaelewa. Msikilize Maalimu leo huko Hai utamuelewa.
 
Zitto ndiye alimshawishi Kachelo hadi kuhamia chama chake, na kumpa ridhaa ya kugombea.... iweje tena ahitaji ushawishi kumpigia kura?
Mambo yamebadilika. Zitto kasema anampigia kura Tundu Lissu.

Swali ninalouliza, kwa kuongezea maneno yako, linampa mzigo mkubwa zaidi Membe kujielezea.

Ikiwa Zitto Kabwe, mtu ambaye unasema alimshawishi Membe kugombea urais kwa tiketi ya ACT, anasema hatampigia kura Membe, sisi wengine ambao hatujui mambo ya ndani ya chama cha ACT tutapata vipi ujasiri wa kusema tumpigie kura Membe?

Membe kashindwa kumshawishi mtu aliyemuomba aingie ACT na kugombea urais, Zitto Kabwe.

Atatushawishi vipi sisi wengine ambao hata si wanachama wa ACT tumpigie yeye kura?
 
Nakuelewa saana dawa ya macho inakera always the same old story.... That's the huge mistake to date huyuu bwana lazma tu angetumika kushusha morali za watu but ni kama hana imapct kwasasa ila tuone 🇹🇿🇹🇿🇹🇿✌️✌️
 
Hata Mimi nimeusoma mchezo namna hiyo. Na kweli hilo litakuwa bao bora kabisa la mashindano la dakika ya 89.
Upinzani wa safari hii wamejipanga kisayansi au tuseme wameikuta timu ya CCM inayoongozwa na 3Zs (yaani zumbukuku watatu) imezubaa haijui kinacho endelea.
Kwa taarifa 3Zs ni;
Jiwe
Baa-shiru
Chakubanga.
Hebu sikia timu hiyo inaweza kuzungumza haya yafuatayo.


Your browser is not able to display this video.
 
Kazungumza mambo mengi lakini nilichokiona ni hatari ya kuwapandisha viongozi wa dini kwenye majukwaa ya kisiasa.

CHADEMA wanakosea Sana, hiyo ndio tunaita political immaturity.

..mbona magufuli amekuwa akifanya kampeni makanisani na misikitini tangu aingie madarakani?

..mbona ccm imekuwa ikipigiwa kampeni na viongozi wa dini na ktk kampeni hizi?

..kamati ya amani ya viongozi wa dini iko kwa ajili ya ccm, au kwa ajili ya nchi, na vyama vyote vya siasa?

..Watanzania tuache UNAFIKI. kuliko kuendelea kuwafanya viongozi wa dini kuwa miliki ya ccm, ni bora tukawapa uhuru kukampeni waziwazi kwa yeyote wanayemuunga mkono.
 
He is very strategic and few can understand this culculated move. What he did is to let them more confusing while things are already settled.
Nyie watu acheni kupotoshana eti Membe yuko strategic, wapi ninyi mnakwama, Membe kasema yeye ni mgombea halali na kakanusha kuwa hakuna vyama vimewahi kuungana vikakitoa chama tawala madarakani. Sasa ninyi mnajipa moyo eti kampigia kampeni huyo lopolopo wenu Lissu.

Believe me, Octoba 28 mtapigika sana hamtaaamini.
 
Bao la ushindi hilo analo zungumzia yeye ni lipi[emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787]embu aendelee kupumzika alale
 
Hii sasa ndio tafsiri ya mtu alievurugwa, spare a thought for Membe.
 
"Hatufui nguo za ndani hadharani" hii lugha ni ngumu kuielewa. Membe anatumia lugha ngumu sana kueleweka. Wana ACT wakimsikiliza Zitto na Maalimu Seif watawaelewa. Msikilize Maalimu leo huko Hai utamuelewa.
Tumwamini nani? Wee unayemlisha maneno au yeye.aliyetamka toka kinywani mwake?
 
Hana jipya huyo ni walewale
 
Huenda huu mchezo unaofanywa na vyama hivi viwili Chadema na ACT ni kupima upepo nani mwenye kuwa na watu wengi ili waungane mkono, na inavyo onyesha ACT wamekubali kuwa backing up team ya Chadema. Lakini kwa mwenendo wa uchaguzi huenda dakika za mwisho ikiwa Lissu atafanyiwa figisu yoyote ya kutomuwezesha kugombania na Membe asimame na Magufuli kwa kupata support ya Chadema. Siasa ni mchezo mchafu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…