Biashara niliyofungua Aprili 2022 nimeifunga Agosti 2024

Maoni yako binafsi,kununua goods to sale(merchandise) au kua na products zako mwenyewe, ipi njia ya uhakika kusimama???
Kusimama katika zote
Unahitaji uwepo wako kwa kiwango kikubwa sana
Wewe ndo una maono ya unachotaka hutakiwi kumpa mtu ayaendeshe maono yako
Kutengeneza product zako nahisi kama kuna asilimia 500 basi ni zaidi ya hapo uwepo wako
Kuanzia production mpaka mali kuwa sokoni
Kwa mfano unataka kuzalisha biscuits
Wewe upo moshi kikazi uendeshaji na uzalishaji wa kiwandani kwa ajili ya hizo biscuts upo ARUSHA
kuna kufata malighafi
Packages
Kuzalisha na kuingiza sokoni
Hizo zote anafanya nani wewe ukiwa mbali???
Ni wazi unatakiwa uwe na mtaji mkubwa wa kuweka wafanyakazi wengi sana wa kusimamia na hili linategemea na scale ya uzalishaji wako
Ila mimi kwa ufatiliaji wa mambo ya production KWA MWANZO KAMA SIO KWA kipindi kikubwa cha uzalishaji unahitaji uwepo wako wewe
Na ukiwaajiri watu bila mfumo dhabiti wa kuwabana lazima utayumbishwa sana

Kwenye buy and sell (HAPA MIMI NI EXPERT)🥹🥹🥹
Mchuuzi mzuri
Bidhaa nyingi nanunua in bulk
Natakiwa kuwepo wakati wa kuzigawa in retail and in wholesale
Bidhaa ambazo naziuza kama zilivyo
Natakiwa kuzifata,kusafiri(mara chache) kuzileta kutoka godwn mwenyewe kuja kuziuza,kuzipigia promo mitandaoni
Kukusanya order za wateja ,kufunga mizigo yao
ni wazi siwezi mpa hayo majukumu kijana pekee au vijana pekeee
Nahitaji pale
Napost mitandao yote maarufu hii na ku update status kila siku
Hayo mkuu ni ngumu kuyafanya ukiwa uneajiriwa
Kwa wastani kwa siku napokea simu sio chini ya 30-50
Hiyo ni full time kaka, ni uachw kazi ufanye kazi

Kila la heri
 
Biashara boss pasua kichwa,inahitaji ufatiliaji, seriousness,na ujasiri..
 
Nimejifunza vitu mkuu asante sana, maani mi visioj yangu ni kuwa na viwanda vya kuproduce bidhaa mbali mbali hapa nchini, ila umenipa mwangaza.🙏
Mambo yanawezekana kumbe, maana nilikuwa najikuta nakata tamaa kwakuwa ndo naend kuanza.
 
Kabla ya kufungua biashara, kuna mambo muhimu ya kuzingatia ili kuhakikisha mafanikio na kuepuka baadhi ya matatizo.

UTAFITI WA MASOKO: Fanya utafiti wa kina kuhusu soko lako linalokusudia, wateja, na washindani. Tambua mahitaji ya wateja na jinsi biashara yako itakavyojitoa kwenye soko.

MPANGO WA BIASHARA:Andaa mpango wa biashara ulio kamili unaojumuisha malengo, mkakati wa soko, bajeti, na makadirio ya mapato na matumizi. Mpango huu utasaidia kuweka dira na kubaini mahitaji ya kifedha.

RASILIMALI ZA FEDHA:Hakikisha una mtaji wa kutosha kuanzisha na kuendesha biashara yako hadi itakapokuwa na uwezo wa kujitegemea. Fikiria kuhusu vyanzo vya fedha, kama vile mikopo au uwekezaji kutoka kwa watu wengine.

SHERIA NA KANUNI: Jua na elewa sheria na kanuni zinazohusu biashara yako, ikiwa ni pamoja na usajili wa biashara, leseni, na kodi. Hii ni muhimu kwa kuzuia matatizo ya kisheria baadaye.

MPANGILIO WA MAHALI: Chagua mahali panapofaa kwa biashara yako. Mahali panahitaji kuwa rahisi kufikika kwa wateja na wafanyakazi, na kuhakikisha kwamba ni sehemu yenye shughuli za biashara zinazofaa.

MKAKATI WA UUZAJI NA KUONGEZA WATEJA: Fikiria jinsi utakavyowafikia wateja wako, ni mbinu gani za uuzaji zitakazotumika, na jinsi utavyoshindana na washindani wako.

HUDUMA BORA:Jipange kutoa huduma bora kwa wateja na kuwa na mfumo mzuri wa kutatua malalamiko na kutoa huduma ya baada ya mauzo.

MIPANGO YA DHARURA: Kuwa na mipango ya dharura kwa matatizo yanayoweza kutokea, kama vile majanga ya asili, matatizo ya kifedha, au upungufu wa rasilimali.

UJUZI NA UZOEFU: Hakikisha una maarifa na ujuzi wa kutosha katika sekta au biashara unayopanga kuanzisha. Uzoefu na elimu ya kina yatakusaidia kufanya maamuzi bora.

Kwa kufuata baadhi ya hatua hizi, unaweza kuongeza ufanisi kwenye biashara.
 
Nimejifunza vitu mkuu asante sana, maani mi visioj yangu ni kuwa na viwanda vya kuproduce bidhaa mbali mbali hapa nchini, ila umenipa mwangaza.🙏
Mambo yanawezekana kumbe, maana nilikuwa najikuta nakata tamaa kwakuwa ndo naend kuanza.
Mungu akuangazie nuru za uso wake na akubariki
Tia juhudi
Soma sana
Juu ya jambo unalotaka kufanya
Kama ni kiwanda cha maziwa soma kuhusu viwanda vya hapa bongo na nje ikiwezekana
Pia nenda kaangalie ile interview ya mlokozi
Ingia you tube nae alikua muajiriwa akaanzisha kiwanda chake
Nenda kaichek yote upate hasira mkuuu
Hakuna jambo linaloshindikana duniani you can learn anything and you can do anything
Weka nia tu
Good night
 
Asante sana , nilishamuangalia muda mrefu.
 
Vijana wa kikristo wametajwa wapi kwenye huu uzi? Mbona kwa miaka mingi nimekuwa nikiamini wewe ni mtu mwenye akili halafu unataka kuni-prove wrong?
 
Uzi hauna tija kama umeshindwa kutaja aina ya biashara uliyokuwa ukiifanya ili tujue tukupe ushauri gani wa kusimama tena, au liwe kama angalizo wa kufanya biashara kama uliyokuwa ukiifanya wewe
.
Sijataja aina ya biashara kwasababu ya watu kama nyie ambao mpo specific, Binafsi nipo General ndio maana nimepata ushauri Kwa watu wengi Sana na umenijenga.
Ningetaja aina ya Biashara nisingepata ushauri Kwa Kila mtu kwasababu watu wangekua specific kwenye Biashara husika na sio general.
 
Sijataja sababu Moja tu ya make ndio chanzo Cha kufunga ila zipo kadhaa. Lakini sabubu kubwa iliyopelekea kufunga ni hasara ,nilikosa pesa ya kuendesha , lkn kumbuka Bado nilikua mbali na eneo la biashara Kwaio usimamizi ingekua changamoto.
 
Asante Sanaa mkuu
 

Hapa umeeleweka, nimejifunza kitu mkuu
 
Mkuu umetoa nondo za maana ingekuwa poa ukatuambia biashara unayofanya tujifunze
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…