Biashara ya Daladala: Ushauri na Mbinu za Uendeshaji Wake

asante mkuu,hili la kuweka record sheet,ntalifanyia kazi,
 
Dar express wana system inayotambulika na hao walio ktk bariers /traffic points.hawatakiwi wala kuruhusiwa kulisimamisha basi la dar express na endapo ukakiuka jua kuwa unaamishwa na kupelekwa ukae police counter ukisubiri matukio tu,au worse ukae kuongoza msafara wa wahesihimiwa.= unakufa njaa.

Ndugu do a simple math, mshahara wa traffic coplo ukoje na anamiliki gari nzuri.e.g Mark II bei ya mafuta lita 1900, anampeleka mtoto wake shule ya private and ananyumba or anajenga nyumba nzuri.hana mkopo mkubwa,kwanza ha-qualify kupata mkopo mkubwa kufuatana na mshahara wake.

So hizo pesa zinatoka ktk ubunifu wao wa kutengeneza makosa barabarani na kutoa fine/notifications fake
 
SHAPU....kwanza kabisa nikupongeze kwa kuichukia na kuikataa rushwa....kwani rushwa hupotosha hukumu na na rushwa hudanganya.....nina ujumbe kwako..(SOMA MESEJI YANGU HAPO CHINI INAHUSU NINI)!
NINA USHAURI KWAKO KUTAKA KUJUA KIWANGO CHA RUSHWA NA HATA NAMNA AMBAVYO WEWE MWENYEWE UNAWEZA KUTOA...!

1. UNAENDESHA PRIVATE CAR......umewahi pata ajali ambayo ilibidi traffick afike?
2. Umewahi kupelekwa mahakamani kwa trfick case ama kesi yeyote ambayo wewe ni mtuhumiwa?
3. Umewahi kukamatwa na polisi na kupelekwa kituoni kwa kosa lolote

SAMAHANI ....KAMA HAYO HAYAJAKUKUTA HUWEZI KUJUA RUSHWA NI NINI! NA UKIKAZA INAKULA KWAKO!
 
bila rushwa..haki haipatikani....toa rushwa upate haki.....(?)
rushwa na tanzania dam-dam.....!
taasisi ipi rushwa kwao mwiko?
nasema kwa kuwa yamenikuta......!
 
Wana jf.ningependa kujua kipata cha daladala kwa siku kwa mikoa ya Dar na arusha kwa makisio inaweza kuwa tsh ngapi?
 
eleza ukubwa wa gari,kama ni hiace,Toyota DCM,au coaster.or yale makubwa ya miliango miwili.kuna wataalam watakujuvya
 
Naombeni msaada kwa hili. Nimefanikiwa kupata mtaji sehemu, nikaamua nifanye investment kwenye daladala na sehemu kununua shamba Visiga. Katika pilikapilika za kuitafuta gari inayomudu mazingira ya daladala nikakutana na jamaa mmoja ambaye amenidiscourage kabisa kuhusu hiyo biashara kwamba kama nataka kufa kwa presha basi niingie huko! Jamani kama kuna anaufahamu na hii biashara naomba msaada japo imeshaniingia akilini kabisa kuwa lazima niifanye.
 
Biashara ya daladala ni nzuri tuu iwapo utapata dereva mzuri/mwaminifu. Lakini na wewe pia inabidi uwe mfuatiliaji wa karibu. Pili, ni vyema ukahakikisha unapata njia nzuri ( I mean njia yenye barabara nzuri ambazo haziumizi gari mf Mwenge- Posta, Mwenge - Kariakoo etc) hapo utakula kuku kiaina.

Kila laheri na usijali watakaokukatisha tamaa coz kama ingekuwa ni biashara isiyolipa kusingekuwa na daladala hata moja barabarani
 

Thanks mkuu, maana jamaa alinitisha hadi nikapoteza confidence. Na hapo kwenye ufuatiliaji, kwamba niwe nawapiga surprise visit?
 
MESTOD,
-Nakutahadharisha tu mkuu kama unakaa stuli ndefu unajiingiza kwenye biashara
ya daladala moja ujue imekula kwako.
-Biashara ya Daladala ni biashara ya watu wavivu wa kufikiri,inafaida kubwa sana
ambayo inaishia kuwaneemesha makondakta na dereva kama nae anaakili.
Faida kubwa anabaki nayo kondacta kwasababu ndiye accounts clerck.
na yeye hana matumizi yoyote ya hiyo fedha zaidi ya kupeleka kwa mama ntilie na
masharobaro mtaani.
-Kabla hujaanza biashara tafuta kondacta umpe kazi kama yake usimhusishe dereva,
mwambie atafute dereva wake wa kuendesha gari,hapo wataiba lakini kidogo watakuletea
hesabu inayolingana.
-Wafumanie wakati fulani fulani ili wajue uko karibu.wasijue nyendo zako.
mara huku mara kule.utapata hesabu nzuri.
-Usifanye makosa ya kusamehe mara kwa mara.kianzio unaweza kufukuza kondacta ukaingiza
mwingine iwe fundisho.
 
<br />
<br />


Mkuu fafanua kidogo,nipo interested na namna ya usimamizi wa hii biashara,kumkabidhi Konda na yeye kuwa ndiye wa kumtafuta Dereva kunasaidiaje kupunguza wizi wao?
 

Hii ni moja kati ya precaution ambayo nilipewa mwanzoni. Sasa issue ipo kwenye kuwabana hao. Nimbanaje konda? Nimwambie hesabu kubwa?
 
MESTOD

Uzuri wa biashara ya daladala unategemea vitu vikuu vifuatavyo

1. Gari ya biashara inabidi iwe katika hali nzuri, kama unanunua basi atleast iwe used from Japan na siyo second hand za bongo, mana hapo kila siku itakua unapata mzozo na dereva.
2.Wewe mmiliki inabidi uwe na source nyingine kwamaana mapato yanayopatikana kwenye biasahara yawepo kwa ajili ya kuendeleza biashara.
3. Mmiliki inabidi uwe unaijali gari kwa kuhakikisha unafanya service za mara kwa mara chini ya usimamizi wako, maana wengine hua wanawapa madereva hela waende garage hili ni tatizo sana

Mie nlianza biashara hiyo Feb mwaka 2009 kwa kununua Coaster moja, then by July ni kachop in loan ya Tshs. 20m nikanunua ya pili...

Kuanzia hapo nikaanza kufanya savings, by Dec 2010 nimerudisha mtaji nloweka na kurecover ile loan nlochop in..now nimefanikiwa open a new line of business nauza used Toyota Coasters directly imported from Japan...kwa hili weza kuwa mteja wangu nikakupa abc zaidi mana pia aina ya engine inamatter sana kwenye hiyo biashara...

Kama vp tuwasiliane
 


Thats good idea mkuu. Mengine tutaongea kwa pm.
 
Usijidanganye kufanya biashara ya Daladala ,wewe kama siyo dereva wa hilo dala dala,basi uwe inspecta wake,ukae kituo cha basi linalopita ili uwe unawaona na kuhesabu tripu zake.
kama unapesa bora ununue canter/fuso ndogo ili ufanye biashara ya shamba na ukodishe hilo gari lako.

mimi namiliki daladala najua wizi wake ,hvi sasa nataka kuziuza niwe mfugaji fulltime
 
Wakuu naomba ushauri wenu kati ya nissan caravan na toyota hiace zote diesel ipi nzuri kwa kuanzia biashara ya daladala? naanza kwa kujaribu na kutake risk na mda mwingi naweza simamia kwa asilimia 65. Vipi uzoefu wa hii biasharana pia nani dealer wa uhakika wa hizi gari hapa bongo na japan. Nawaombeni ushauri wakuu. Pia nipeni bei zake kwa yule anaejua.
 
Unataka kufanyia mji gani hiyo biashara? Nissan ni nzuri kwenye maeneo yenye hali ya hewa ya baridi kama Arusha, mbeya, Knjaro na Iringa. Sehemu zenye joto haifai. Pia kama unategemea kwenda route zenye milima na miinuko ya mara kwa mara, diesel ingine haziwezi mzigo na zinawahi kuchoka. Ntarudi baadae
 
Sasa sinasikia mabasi ya kasi yanakuja bongo watu wa biashara ya daladala nasikia wanaanza kuziuza kiaina zikiwa zinalipa sasa angalia usiigie mkenge
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…