Biashara ya movies za nje ni 🔥 sana Kkoo, ni nini kiliua soko la filamu za Tanzania?

Mtu anayesema bora comedy hajaona comedy za kenya.Sisi mtu akikaza na style ya comedy basi atakaza nayo hadi izoeleke.mfano mkojani ingebid awe ashatafuta ubunifu mwingine zaidi ya lafudhi yake ya kipemba
Ubunifu hatuna
 

Kanumba mm sioni kama alikua na kitu cha ziada kwenye industry,ni vile alivuma wakati ambao kibongo bongo industry ya movie ndio ilikua Inaanza Na siyo kwamba alikua mzuri kiivo,movie ni technology na investment Na siyo mambo ya kanumba
 
Kuna movies za 1960 unazicheki za Mambele. Dah. Wale jamaa wametuacha mbali kingese.
 
Hata mambo ya kisayansi hawana, hawajui hata masuala ya carnivore au herbivore, hata kuclassifly wanyama ni hola, na wakiigiza scene za hospital hakuna technical ishu wanazo ongea . Bongo muvie madudu Sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mastermind wa bongo movie mwenye mission na vision just gone so wakina hemed ni kujilamba lamba tuu ni bora nirudie movie za kanumba za kitambo kuliko za leo nilikuwa super and number one fan's wa tamthilia ya mtungi sijui walistop vipi wale watu wakina cheche
 
Mtu anakuonyea bunduki afu anakwambia ntakuchinja,

Au mtu anaajisemesha eti ""naenda kunywa maji"" badala ya kwenda kunywa bila kuongea utafikili sisi hatuoni;

Kuna movie ya zaman kidogo ya yule demu Jennifer kyaka( odama) eti alikuwa na damu mguuni kigezo hicho Cha damu mguuni mamake akajua kuwa mtto wake ashatolewa bikra.. akati in reality hakuna kitu Kama hicho.
Nikaacha kuangalia upumbavu huo pamoja na za kihindi,
 
Mtu anayesema bora comedy hajaona comedy za kenya.Sisi mtu akikaza na style ya comedy basi atakaza nayo hadi izoeleke.mfano mkojani ingebid awe ashatafuta ubunifu mwingine zaidi ya lafudhi yake ya kipemba
Au bwana kidogo.
 

U think kanumba Kwa saa hii angeweza kufanya kitu gani ? Industry inahitaji zaidi watu walionyuma ya camera na siyo kweli kwamba hatuna watu wanaojua kuigiZa.tatizo ni technology na investment uyo kanumba alikua wa kawaida mnoo ,yani mm ukinitajia kanumba nakuona ww hata elimu ya diploma huna ,yani ww ni house boy uliyechangamka
 
Kuna movies za 1960 unazicheki za Mambele. Dah. Wale jamaa wametuacha mbali kingese.
Mkuu nahisi sisi Tanzania kwa ujumla (kila kitu) tuko nyuma mno yani miaka 100 nyuma,tuishi maisha waliokua wanaishi 1800 huko kasoro tu teknolojia
 
Huu ujivuni sasa mzee, hebu tutajie msanii wa bongo aliyekua na uwezo wa kutoa filamu kumzidi mwendazake Steven Charles Kanumba
 
Mimi
Haikufuma
Saluni ya mama kimbo
(hizi utafananisha na behind the enemy line)
Khaaaaa ,ertugul khaaah [emoji23]
 
Kuna movies za 1960 unazicheki za Mambele. Dah. Wale jamaa wametuacha mbali kingese.
Jumamosi nilikua nimekaa sehemu nikaona muvi ya Yesu (ya kibongo) inaonyeshwa TBC. Nikawa interested kuifatilia nione kinachoonyeshwa. Sijajua kama wale ni waigizaji rasmi au ni watu tu waliamua kuigiza, ila nilicheka sana.

Ile movie maarufu ya The Jesus Film ya kizungu, ukiambiwa bajeti yake tu ilikua Usd 6 million (Sawa na Tsh 13.5 billion) na ilitengenezwa mwaka 1979!

Matatizo makubwa mawili nayoyaona kwenye bongo movie ni:

1. Bajeti finyu
2. Weledi

Hivi vitu viwili ni kama havipo kabisa kwenye hii tasnia na matokeo yake ndio haya tunayoyaona. Mtu anataka atengeneze muvi kwa bajeti ya tsh milioni mbili, unategemea nini? Wangekua angalau na weledi, wangeweza kutumia ubunifu kama wanaofanya wenzetu kutengeneza low budget movies na zikawa nzuri. Kuna movies za wenzetu unakuta movie nzima ina watu watano tu na location imetumika moja, ila hubanduki kwenye kiti!
 
Boss hata ukiweka pesa yako hapo hakuna waigizaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…