Biashara ya ngono ndiyo biashara inayofanywa na Wanawake wengi zaidi

Genesis 38​

Yuda Na Tamari​

1Wakati ule, Yuda akawaacha ndugu zake akaenda kuishi na Hira Mwadulami. 2Huko Yuda akakutana na binti wa Kikanaani aitwaye Shua akamwoa na akakutana naye kimwili, 3akapata mimba akamzaa mwana, ambaye alimwita Eri. 4Akapata mimba tena, akamzaa mwana na kumwita Onani. 5Akamzaa mwana mwingine tena, akamwita Shela. Huyu alimzalia mahali paitwapo Kezibu.
6Yuda akampatia Eri, mzaliwa wake wa kwanza mke, aitwaye Tamari. 7Lakini Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda alikuwa mwovu machoni pa BWANA, kwa hiyo BWANA akamwua.
8Kisha Yuda akamwambia Onani, “Kutana kimwili na mke wa ndugu yako na utimize wajibu wako kwake kama mke wa ndugu yako ili umpatie ndugu yako uzao.” 9Lakini Onani alijua kwamba uzao haungekuwa wake, kwa hiyo kila alipokutana kimwili na mke wa ndugu yake, alimwaga chini mbegu za kiume ili asimpatie ndugu yake uzao. 10Alichofanya kilikuwa kiovu machoni pa BWANA, hivyo, pia BWANA akamwua Onani.
11Kisha Yuda akamwambia Tamari mkwewe, “Ishi kama mjane nyumbani mwa baba yako mpaka mwanangu Shela atakapokua.” Kwa maana alifikiri, “Angeweza kufa pia kama ndugu zake.” Kwa hiyo Tamari alikwenda kuishi nyumbani kwa baba yake.
12Baada ya muda mrefu mke wa Yuda binti wa Shua akafariki. Baada ya msiba, Yuda alikwenda Timna, kwa watu waliokuwa wakikata kondoo wake manyoya, naye alifuatana na rafiki yake Hira Mwadulami.
13Tamari alipoambiwa, “Baba mkwe wako yuko njiani kwenda Timna kukata kondoo wake manyoya,” 14alivua mavazi yake ya ujane, akajifunika kwa shela ili asifahamike, akaketi kwenye mlango wa Enaimu, ambao upo njiani kuelekea Timna. Akafanya hivyo kwa sababu aliona kwamba, ingawa Shela amekua, lakini alikuwa hajakabidhiwa kwake kuwa mkewe.
15Yuda alipomwona alifikiri ni kahaba, kwa sababu alikuwa amefunika uso wake. 16Pasipo kutambua kwamba alikuwa mkwe wake, akamwendea kando ya njia na kumwambia, “Njoo sasa, nikutane na wewe kimwili.”
Yule mkwewe akamwuliza, “Utanipa nini nikikutana nawe kimwili?”17Akamwambia, “Nitakutumia mwana-mbuzi kutoka kundi langu.”
Akamwuliza, “Utanipa kitu cho chote kama amana mpaka utakapompeleka?”18Akamwuliza, “Nikupe amana gani?”
Akamjibu, “Pete yako na kamba yake pamoja na fimbo iliyo mkononi mwako.” Kwa hiyo akampa vitu hivyo kisha akakutana naye kimwili, naye akapata mimba yake. 19Tamari akaondoka, akavua shela yake akavaa tena nguo zake za ujane.
20Wakati ule ule, Yuda akamtuma rafiki yake Mwadulami apeleke yule mwana-mbuzi ili arudishiwe amana yake kutoka kwa yule mwanamke, lakini yule rafiki yake hakumkuta yule mwanamke. 21Akawauliza watu wanaoishi mahali pale, “Yuko wapi yule kahaba wa mahali pa kuabudia miungu aliyekuwa kando ya barabara hapa Enaimu?”
Wakamjibu, “Hajawahi kuwepo mwanamke ye yote kahaba wa mahali pa kuabudia miungu hapa.”22Kwa hiyo akamrudia Yuda na kumwambia, “Sikumpata. Zaidi ya hayo, watu wanaoishi mahali pale walisema ‘Hapakuwahi kuwepo mwanamke ye yote kahaba wa mahali pa kuabudia miungu hapa.’ ”
23Kisha Yuda akasema, “Mwache avichukue vitu hivyo, ama sivyo tutakuwa kichekesho. Hata hivyo, nilimpelekea mwana-mbuzi, lakini hukumkuta.”
24Baada ya miezi mitatu Yuda akaambiwa, “Tamari mkweo ana hatia ya kuwa kahaba, na matokeo yake ana mimba.”
Yuda akasema, “Mtoeni nje na achomwe moto hadi afe!”25Alipokuwa akitolewa nje, akatuma ujumbe kwa baba mkwe wake kusema, “Nina mimba ya mtu mwenye vitu hivi.” Akaongeza kusema, “Angalia kama utatambua kwamba pete hii na kamba yake pamoja na fimbo hii ni vya nani.”
26Yuda akavitambua na kusema, “Yeye ana haki kuliko mimi, kwa kuwa sikumkabidhi kwa mwanangu Shela ili awe mkewe.” Tangu hapo hakukutana naye kimwili tena.
27Wakati ulipofika wa kujifungua, kukawa na wana mapacha tumboni mwake. 28Alipokuwa akijifungua, mmoja akatoa mkono wake nje, kwa hiyo muuguzi akachukua uzi mwekundu na kuufunga mkononi mwa yule mtoto akasema, “Huyu ametoka kwanza.” 29Lakini alipourudisha mkono wake ndugu yake akaanza kutoka naye akasema, “Hivi ndivyo ulivyotoka kwa nguvu!” Akaitwa Peresi. 30Kisha ndugu yake, aliyekuwa na uzi mwekundu mkononi, akatoka naye akaitwa Zera.
Copyright information for Neno
 
Guys,mimi naona sisi wanaume tunakuwa so biased kwa hii issue kwa kuwahusisha wanawake kuwa ndio wanaonekana waanga wa biashara hii. Mi naona mtoa mada kasahau kufanya uchunguzi kuwa ili biashara ionekane imefanyika nini kinatakiwa kuwepo. Mimi naona two sides must be present, meaning... where one sells, a buyer is there to buy.

Kwa mantiki hiyo 89% ya wanawake wanaofanya biashara ya ngono( kwa mujibu wa mtoa mada) ni sawa na asilimia hiyo hiyo ya wanaume wanaonunua bidhaa hiyo. Hapo mi naona ngoma droo.
 
Yeah inaanza uzinzi mwisho mnaenda kwenye ndoa ndio maana Kwa Sasa ndoa hazidumu kwasababu mlivyopatana mkikumbuka lawama zinaanza na kila mmoja anadhani yeye ni msafi.
Ukweli wadada wengi hufanya biashara ya ngono
Na wanajua kufanya BIASHARA sana... wapo vzr mnooo ktk customer CARE na kukwepa kuharibiwa BIASHARA zao
 
Si kweliiii WAUZAJI ni wengi kuliko WANUNUAJI
 
Kabisa naunga mkono hoja,serikali inakosa mapato,kwa kujiaminisha kwamba hakuna kitu kama hicho.
 
Miaka 10 ijayo ngono inaweza kuwa kitovu Cha mapato hapa kwetu bahati mbaya bandari huenda haitakuwepo tunaweza kutegemeza Kodi kwenye sekta hii yenye wateja wengi kuliko chochote.

Tatizo ni kuwabaini na mifumo yankuwalipisha Kodi.

Si rahisi. Maana hata mkeo unakuta anafanya BIASHARA na ww (LEGIT) wakat huo anafanya UHARAMIA wa kuuza bidhaa haramu, huko nje.
 
forceNi kweli kabisa, this is the oldest professional na the oldest business ambayo imeajiri watu wengi kuliko ajira nyingine zote!.
Mnanikumbusha mutual induction na induced electromotive force, (i.e.m.f), the direction of induce i.e.m.f is such to oppose a motion producing it (sitaki na taka) halafu baadae imooo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…