Biashara ya Nguo za Mtumba: Ushauri na Muongozo wa Kuifanya kwa Mafanikio


Kama wateja wanakua wengi basi baro ya kg 100 unaimaliza siku moja tu but wakiwa wachache unawezapiga nusu au robo tatu na nusu au robo inayobakia unamalizia siku inayofuata.

Hata hivyo experience hiyo nayokupatia ni huku kusini sijajua maeneo mengine na hasa hapo DAR biashara ipoje! so ni vema ukazingatia hali halisi ya mahala unapotaka ukafanyia biashara.
 

Asante sana kwa reply hii na nimekuwa inspired sana. sasa naomba kujua napataje hili baro? Nawezaje kupokea au kotoa oda ya huu mzigo?
 
Ha ha ha! Hapo ndo pagumu, anapataje hizo balo? Watu hawataki kusema wanapiga chenga tu.
 
Balo zipo sehemu nyingi

Changamoto ni iyo uchakachuzi wa mabalo, niliwai kwenda uganda balo hazifunguliwi.

Mara nyingi balo ikiwa na koa, imefungwa na yale mabati inakuwa haijafunguliwa, ila ikiwa na plastic mara nyingi izo ndizo zimefungwa upya, ila c lazima iwe ivo.

Haya ni jibu swali wanalokwepa wengi zinapatikana wap?

Ukifika mnazi mmoja dar, kama unatoka k.koo nyooka moja kwa moja kama unaenda mnara wa saa au stesheni, unapovuka tu makutano ya pili ya mataa, ya mnazi mmoja kuna maduka wanauza sana kanga na vitenge, kuanzia hapo, maduka ya mitumba nikibao, nenda mtaa wa pili kama sikosei unaitwa sofia, maduka kibao hapo mitumba tupu, yani zunguka eneo ilo utapata mitumba kibao.

Pili ukiwa congo, k.koo kituoni mkono wa kulia ukiwa unaelekea mnazi lipo duka moja hapo kwa mhind linapakana na duka la samsung.

Tatu Magomeni, ni eneo jipya hili, ofis za ttcl ukifika hapo upande wa pili utaona mitumba had ya viatu wholesale bales.

Hapa magomeni ni makutano ya mataa pale ukiuliza ofis za ttcl utaoneshwa.

Changamoto ni kupata bales nzuri, kama unaweza mtafute mteja wao mzoefu wanaempaga vitu bora, akuchukulie.

Au washikishe wale jamaa tingo wa dukani kitu kidogo, wambie nipe kitu cha maaana jifanye ni mzoefu ila unabadili duka tu.

Ukijifanya mzoefu usizubae, kwa mfano ukiuliza mixer ya nguo za kike, akikuuliza kg ngap unakuwa shapu kuonesha unajua, sio wanauliza Kg hujui kuwa balo zina kilogram

Au unaulizwa material inayotaka hukui, either cotton, nylon n.k

Nahs nimesema kidogo kitakachowasaidieni
 

Hii kitu ni common sana maeneo ya mtwara ukiwa mjanja inalipa sana.
 

Mkuu nimependa mchanganuo wako! Nisaidie naweza kuzipata wap hzo bila kuchakachuliwa na wajanja? Nina mtaji kidogo nataka nifanye biashara ya nguo za kike maana nasoma bado ila nataka niwe mjasilia mali.
 
Mkuu nimependa mchanganuo wako! Nisaidie naweza kuzipata wap hzo bila kuchakachuliwa na wajanja? Nina mtaji kidogo nataka nifanye biashara ya nguo za kike maana nasoma bado ila nataka niwe mjasilia mali
Naona kuna mtu kaeleza vizuri sana maduka yalipo.
 

Mkuu kama hautajari mimi mwenyewe nafanya shughuli ya mitumba ila kwa sasa soko siyo zuri huku dar na nina mzigo mwingi sana nisaidie kuutoa.
 
mkuu kama hautajari mimi mwenyewe nafanya shughuli ya mitumba ila kwa sasa soko siyo zuri huku dar na nina mzigo mwingi sana nisaidie kuutoa

niko tayari kukusaidia na kuutoa huo mzigo iwe kupitia mimi mwenyewe au kuwapa direction ndugu zangu/wafanya biashara wezangu so ni pm no yako tuunganishe nguvu!
 
Wakuu mimi nauza mitumba kwa rejareja bei poa kabisa nguo aina zote niko dsm, temeke,mbagala,kizuiani ila mwenye kuhitaji nguo kuanzia kumi tunampelekea mzigo anachagua baada ya kuthibitisha uhitaji wake
 
mkuu kama hautajari mimi mwenyewe nafanya shughuli ya mitumba ila kwa sasa soko siyo zuri huku dar na nina mzigo mwingi sana nisaidie kuutoa

Wakuu mimi nauza mitumba kwa rejareja bei poa kabisa nguo aina zote niko dsm, temeke,mbagala,kizuiani ila mwenye kuhitaji nguo kuanzia kumi tunampelekea mzigo anachagua baada ya kuthibitisha uhitaji wake

Mkitoa kwa bei ya jumla yan cheap, wasiluaneni nami private, niwachangie mzigo
 
Naomba waungwana ambao hata mwenyezi Mungu atawalipa. Nahitaji kufanya biashara ya mitumba ya kike, Je Inalipa? Nikipitisha ofisini, vyuoni, masaluni etc je itanilipa kwa mtaji wa 100,000/=?

Nipo Dar es Salaam ndugu zangum samahani kwa muda wenu jamani.
 
Kila biashara inalipa mkuu hakuna isiyolipa ndo maana wanafanya, kila la kheri.
 
Biashara ya mitumba inalipa tena ukengua wafungashia Kenya, kuna soko lamitumba tena mitumba first class.kama unahela ya kutosha hata kama laki 5 ivi kianzio, ila hii inataka uwe na sehemu waitundika au hata kijibanda chako cha kufanyia biashara.
 
Mafikizolo nipo njian kuelekea kenya kutafuta hii kitu grade one. Hebu nipe direction kidogo mkuu.
 
Mafikizolo nipo njian kuelekea kenya kutafuta hii kitu grade one..hebu nipe direction kidogo mkuu
Ntakupa link ya page fcbk ya wanaouza mitumba grade A pale gikomba kenya au waweza searh kama una fcbk account.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…