Balo zipo sehemu nyingi
Changamoto ni iyo uchakachuzi wa mabalo, niliwai kwenda uganda balo hazifunguliwi.
Mara nyingi balo ikiwa na koa, imefungwa na yale mabati inakuwa haijafunguliwa, ila ikiwa na plastic mara nyingi izo ndizo zimefungwa upya, ila c lazima iwe ivo.
Haya ni jibu swali wanalokwepa wengi zinapatikana wap?
Ukifika mnazi mmoja dar, kama unatoka k.koo nyooka moja kwa moja kama unaenda mnara wa saa au stesheni, unapovuka tu makutano ya pili ya mataa, ya mnazi mmoja kuna maduka wanauza sana kanga na vitenge, kuanzia hapo, maduka ya mitumba nikibao, nenda mtaa wa pili kama sikosei unaitwa sofia, maduka kibao hapo mitumba tupu, yani zunguka eneo ilo utapata mitumba kibao.
Pili ukiwa congo, k.koo kituoni mkono wa kulia ukiwa unaelekea mnazi lipo duka moja hapo kwa mhind linapakana na duka la samsung.
Tatu Magomeni, ni eneo jipya hili, ofis za ttcl ukifika hapo upande wa pili utaona mitumba had ya viatu wholesale bales.
Hapa magomeni ni makutano ya mataa pale ukiuliza ofis za ttcl utaoneshwa.
Changamoto ni kupata bales nzuri, kama unaweza mtafute mteja wao mzoefu wanaempaga vitu bora, akuchukulie.
Au washikishe wale jamaa tingo wa dukani kitu kidogo, wambie nipe kitu cha maaana jifanye ni mzoefu ila unabadili duka tu.
Ukijifanya mzoefu usizubae, kwa mfano ukiuliza mixer ya nguo za kike, akikuuliza kg ngap unakuwa shapu kuonesha unajua, sio wanauliza Kg hujui kuwa balo zina kilogram
Au unaulizwa material inayotaka hukui, either cotton, nylon n.k
Nahs nimesema kidogo kitakachowasaidieni