Biashara ya Nguo za Mtumba: Ushauri na Muongozo wa Kuifanya kwa Mafanikio

Biashara ya Nguo za Mtumba: Ushauri na Muongozo wa Kuifanya kwa Mafanikio

Owk Mr.Mtimbo hongera kwa hapo ulipofikia, tuendelee hiyo biashara ya jumla ya mabaro imekaa vp? Na kwa upande wa mnada ilikuwa inakuchukua mda gani kumaliza baro moja na kutia sokoni lingine...big up sana mkuu kwa kututiaa moyo wajasiriamali wenzako nasi pia tutaleta mrejesho hapa hapa jamvini ili wengine pia waendelee kujifunza hii fursa

Kama wateja wanakua wengi basi baro ya kg 100 unaimaliza siku moja tu but wakiwa wachache unawezapiga nusu au robo tatu na nusu au robo inayobakia unamalizia siku inayofuata.

Hata hivyo experience hiyo nayokupatia ni huku kusini sijajua maeneo mengine na hasa hapo DAR biashara ipoje! so ni vema ukazingatia hali halisi ya mahala unapotaka ukafanyia biashara.
 
Nimeiona mkuu text yako!
Ila biashara ipo hivi:

Kila baro inavyotoka nje inakua na mchanganyiko wa nguo zote yaani grade A, B,C na zinginezo na haswa kwa zile mixture kinachosumbua kuna aina fulani ya baro huwa wabongo huzifungua na kuchukua nguo nzuri then huzipack tena
sasa hukikumbana nazo hizo zilizofunguliwa unaweza ukakata mtaji

Kuna aina kama tatu hivi za baro ambazo ni nzuri kwa mnada kwani zenyewe ni mixture

Aina ya kwanza ambazo zenyewe hutoa nguo nyingi ambazo ni grade one ni Australia ambazo zinapatikana ktika uzito wa kg 100 na bei yake ina range Tsh 450000 hadi 500000,hizi ni nzuri na ndio ninazoziuza Mimi nawe nakushauri uzipate hizo kwani si rahisi kukata pesa yako ,umeanguka sana unarudisha pesa yako

Za pili ni baro za kichina nazo ni nzuri na hata bei yake ni affordable kg 100 @ Tsh 370000 hadi Tsh 420000

Na za tatu ni za kimarekani maarufa kama SUMMER, zinapatikana katika uzito wa kg 50 na 80 na bei zake Tsh 250000 hadi Tsh280000 kwa za kg 50 na Tsh 320000 hadi Tsh370000
ndio hivyo mkuu jipange kachukue mzigo huo

Asante sana kwa reply hii na nimekuwa inspired sana. sasa naomba kujua napataje hili baro? Nawezaje kupokea au kotoa oda ya huu mzigo?
 
Ha ha ha! Hapo ndo pagumu, anapataje hizo balo? Watu hawataki kusema wanapiga chenga tu.
 
Balo zipo sehemu nyingi

Changamoto ni iyo uchakachuzi wa mabalo, niliwai kwenda uganda balo hazifunguliwi.

Mara nyingi balo ikiwa na koa, imefungwa na yale mabati inakuwa haijafunguliwa, ila ikiwa na plastic mara nyingi izo ndizo zimefungwa upya, ila c lazima iwe ivo.

Haya ni jibu swali wanalokwepa wengi zinapatikana wap?

Ukifika mnazi mmoja dar, kama unatoka k.koo nyooka moja kwa moja kama unaenda mnara wa saa au stesheni, unapovuka tu makutano ya pili ya mataa, ya mnazi mmoja kuna maduka wanauza sana kanga na vitenge, kuanzia hapo, maduka ya mitumba nikibao, nenda mtaa wa pili kama sikosei unaitwa sofia, maduka kibao hapo mitumba tupu, yani zunguka eneo ilo utapata mitumba kibao.

Pili ukiwa congo, k.koo kituoni mkono wa kulia ukiwa unaelekea mnazi lipo duka moja hapo kwa mhind linapakana na duka la samsung.

Tatu Magomeni, ni eneo jipya hili, ofis za ttcl ukifika hapo upande wa pili utaona mitumba had ya viatu wholesale bales.

Hapa magomeni ni makutano ya mataa pale ukiuliza ofis za ttcl utaoneshwa.

Changamoto ni kupata bales nzuri, kama unaweza mtafute mteja wao mzoefu wanaempaga vitu bora, akuchukulie.

Au washikishe wale jamaa tingo wa dukani kitu kidogo, wambie nipe kitu cha maaana jifanye ni mzoefu ila unabadili duka tu.

Ukijifanya mzoefu usizubae, kwa mfano ukiuliza mixer ya nguo za kike, akikuuliza kg ngap unakuwa shapu kuonesha unajua, sio wanauliza Kg hujui kuwa balo zina kilogram

Au unaulizwa material inayotaka hukui, either cotton, nylon n.k

Nahs nimesema kidogo kitakachowasaidieni
 
Ni biashara nzuri sana mkuu na hasa kama ulivyosema unataka kuuza kwa njia ya mnada Mimi mwenyewe naifanya iyo shughuri nilianza just mwezi 1 uliopita na baro moja na sasa ninauwezo wa kuagizia baro 5 na malengo yangu niwe nauza kwa jumla na lengo hilo litafanikiwa kwani msimu wa korosho ndo unaanza huku kusini. kwa Maelezo zaidi ni PM namba zako tuone kama tunaweza kushirikana kwa hilo

Hii kitu ni common sana maeneo ya mtwara ukiwa mjanja inalipa sana.
 
Nimeiona mkuu text yako!
Ila biashara ipo hivi:

Kila baro inavyotoka nje inakua na mchanganyiko wa nguo zote yaani grade A, B,C na zinginezo na haswa kwa zile mixture kinachosumbua kuna aina fulani ya baro huwa wabongo huzifungua na kuchukua nguo nzuri then huzipack tena
sasa hukikumbana nazo hizo zilizofunguliwa unaweza ukakata mtaji

Kuna aina kama tatu hivi za baro ambazo ni nzuri kwa mnada kwani zenyewe ni mixture

Aina ya kwanza ambazo zenyewe hutoa nguo nyingi ambazo ni grade one ni Australia ambazo zinapatikana ktika uzito wa kg 100 na bei yake ina range Tsh 450000 hadi 500000,hizi ni nzuri na ndio ninazoziuza Mimi nawe nakushauri uzipate hizo kwani si rahisi kukata pesa yako ,umeanguka sana unarudisha pesa yako

Za pili ni baro za kichina nazo ni nzuri na hata bei yake ni affordable kg 100 @ Tsh 370000 hadi Tsh 420000

Na za tatu ni za kimarekani maarufa kama SUMMER, zinapatikana katika uzito wa kg 50 na 80 na bei zake Tsh 250000 hadi Tsh280000 kwa za kg 50 na Tsh 320000 hadi Tsh370000
ndio hivyo mkuu jipange kachukue mzigo huo

Mkuu nimependa mchanganuo wako! Nisaidie naweza kuzipata wap hzo bila kuchakachuliwa na wajanja? Nina mtaji kidogo nataka nifanye biashara ya nguo za kike maana nasoma bado ila nataka niwe mjasilia mali.
 
Mkuu nimependa mchanganuo wako! Nisaidie naweza kuzipata wap hzo bila kuchakachuliwa na wajanja? Nina mtaji kidogo nataka nifanye biashara ya nguo za kike maana nasoma bado ila nataka niwe mjasilia mali
Naona kuna mtu kaeleza vizuri sana maduka yalipo.
 
Sijajua Dar biashara ya mnada ipoje/ inalipaje lakini kwa huku kusini mtwara/ lindi biashara ni nzuri sana na kama nilivyokudokezea pale awali sasa hivi no msimu wa korosho so wakulima wanakua na pesa na biashara hufanyika poa tu.

Kuhusu faida, biashara ikiwa nzuri baro 1 hununua baro lezange na kwa upande wangu imenisaidia sana kuinuka haraka haraka name ndio maana naanza kua hats name kibur cha kutaka kuanza na mimi kuanza kuuza kwa jumla

Mkuu kama hautajari mimi mwenyewe nafanya shughuli ya mitumba ila kwa sasa soko siyo zuri huku dar na nina mzigo mwingi sana nisaidie kuutoa.
 
mkuu kama hautajari mimi mwenyewe nafanya shughuli ya mitumba ila kwa sasa soko siyo zuri huku dar na nina mzigo mwingi sana nisaidie kuutoa

niko tayari kukusaidia na kuutoa huo mzigo iwe kupitia mimi mwenyewe au kuwapa direction ndugu zangu/wafanya biashara wezangu so ni pm no yako tuunganishe nguvu!
 
Wakuu mimi nauza mitumba kwa rejareja bei poa kabisa nguo aina zote niko dsm, temeke,mbagala,kizuiani ila mwenye kuhitaji nguo kuanzia kumi tunampelekea mzigo anachagua baada ya kuthibitisha uhitaji wake
 
mkuu kama hautajari mimi mwenyewe nafanya shughuli ya mitumba ila kwa sasa soko siyo zuri huku dar na nina mzigo mwingi sana nisaidie kuutoa

Wakuu mimi nauza mitumba kwa rejareja bei poa kabisa nguo aina zote niko dsm, temeke,mbagala,kizuiani ila mwenye kuhitaji nguo kuanzia kumi tunampelekea mzigo anachagua baada ya kuthibitisha uhitaji wake

Mkitoa kwa bei ya jumla yan cheap, wasiluaneni nami private, niwachangie mzigo
 
Naomba waungwana ambao hata mwenyezi Mungu atawalipa. Nahitaji kufanya biashara ya mitumba ya kike, Je Inalipa? Nikipitisha ofisini, vyuoni, masaluni etc je itanilipa kwa mtaji wa 100,000/=?

Nipo Dar es Salaam ndugu zangum samahani kwa muda wenu jamani.
 
Kila biashara inalipa mkuu hakuna isiyolipa ndo maana wanafanya, kila la kheri.
 
Biashara ya mitumba inalipa tena ukengua wafungashia Kenya, kuna soko lamitumba tena mitumba first class.kama unahela ya kutosha hata kama laki 5 ivi kianzio, ila hii inataka uwe na sehemu waitundika au hata kijibanda chako cha kufanyia biashara.
 
Mafikizolo nipo njian kuelekea kenya kutafuta hii kitu grade one. Hebu nipe direction kidogo mkuu.
 
Mafikizolo nipo njian kuelekea kenya kutafuta hii kitu grade one..hebu nipe direction kidogo mkuu
Ntakupa link ya page fcbk ya wanaouza mitumba grade A pale gikomba kenya au waweza searh kama una fcbk account.
 
Back
Top Bottom