Biashara ya Stationery: Ushauri, Vifaa, Gharama na Mbinu za Uendeshaji

Kwa miji mipya ndio sehemu nzuri za kutokea,na utajikuta unapata fursa zingine
 
Bei ya katatasi,,counter books,mafaftari ya kawaida na pens kwa jumla zikoje kwa sasa dar,,nataka nijaribu na hizo bidhaa wadau

Nilikuwa namaanisha bei ya karatasi (rimu),peni,,counterbooks na madaftari ya kawida kwa bei ya jumla ipoje kwa sasa Dar naomba msaada wenu wadau.
 
Mwenye kujua tafadhali juu ya Skills anazotakiwa kuwa nazo mfanyabiashara wa stationery ili kuwashika wateja wake wote...... Plz naomba uniorodheshee........ Asante
Microsoft office word, excel, publisher na PowerPoint kama uko maeneo ya chuoni, pia graphic designing kwa ajili ya kudesign card (unaweza kutumia word na publisher au Photoshop).
 
Wakuu naomba mnipe elimu kidogo kuhusu biashara ya stationary

Jinsi ya uendeshaji wake,location nzuri ya kuianzisha,faida yake,hasara na changamoto nyingine

Asanteni
 
Nipo musoma ,nimepata sehemu machine ya kopy na kuprint kwa laki 7 ,computer ninayo laptop,so nia yangu nianze na kazi ya kutoa copy,kuprint na kutype
 
Itapendeza pia kama eneo hilo litakuwa na taasisi za serikali mf. shule msingi/sekondari,halmashauri au ofisi yyte ya serikali ambayo huduma zake zinatumiwa na wengi,hapa utaneemeka kwa kupata zabuni mbalimbali. Pia uchangamfu wa eneo,pilikapilika,na utumiaji mkubwa wa huduma za stationary mf. matumizi ya internet,kuchapa kadi,kupiga na kusafisha picha,kuandaa mikataba ya makampuni/vikundi,kutengeneza tiketi za mabasi,n.k n.k
Ila kama ni stationery kwa ajili ya kutoa photocopy/kuchapa ni heri ukaanzisha kilimo cha bustani maana huwezi kutengeneza pesa ya maana na huku gharama za pango,umeme na maisha mengine zinakusubiri..
 
Mkuu nimekuelewa sana lengo langu ni kubwa sana wala sitaishia kwenye copy na typing ,nitafanyia kazi hili wazo lako, na sehemu niliyopanga kufungua ofisi ni karibu na chuo cha maendeleo ya jamii
 
Habari za siku mingi wanaJf ni muda sasa sikuwa naposti wala kukoment ila mara mojamoja nilikuwa napita kama msomaji hii ni kutokana na majukumu.

Nilibahatika kupata ajila taasisi moja hivi ila pia ni mjasiriamali ambaye nimewekeza kwenye stationery mbili kubwa tu ila imefika muda napenda kuongeza ubunifu.

Nimevutiwa na biashara ya kuprint covers za simu (smartphones) ambapo nimekua nikiona baadhi ya watu wameprint picha zao kwenye covers za simu zao lakini nikiwauliza wengi husema waliprint Nairobi sasa nahitaji kujua ni mashine ipi na ina bei gani pia material zake na upatikanaji wake pia.

Naamini humu hawakosi wataalamu wa idara hiyo please tupeane mautundu si unajua tena mwanamke kujishughulisha.!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…