Biashara ya ukahaba imekithiri Sinza na kusababisha wakazi kuhama nyumba zao

Biashara ya ukahaba imekithiri Sinza na kusababisha wakazi kuhama nyumba zao

images (39) (11).jpeg
Biashara ya ukahaba imevamia kwa kasi baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam, na kusababisha kero na adha kubwa katika makazi ya watu, hasa eneo la Sinza kiasi cha kuzifanya baadhi ya familia kuhama nyumba, Mwananchi limebaini.

Wazazi na walezi wanasema hali hiyo pamoja na kelele zinazosababishwa na muziki unaopigwa kwenye baa kubwa vimewasababishia ugumu usizoelezeka wa malezi ya watoto.

Uchunguzi wa Mwananchi umebaini biashara hiyo imekithiri katika mitaa mingi ya Sinza, hasa ile inayozunguka kumbi maarufu za starehe na hoteli kubwa.

Hali hiyo inayomulikwa kwa Sinza, ipo pia maeneo mengine kama Tabata, Ubungo, Kindondoni Buguruni na kwingineko, japokuwa ni kwa viwango tofauti.

Kutokana na hali ilivyo, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe hivi karibuni alikutana na watendaji na wenyeviti wa mitaa ili kujadili mambo mbalimbali, likiwemo la biashara hiyo huku akiwataka viongozi wa dini kulikemea suala hilo akisema utamaduni huo si wa Tanzania.

Wakazi wa maeneo husika wanasema mbali na kuwaletea changamoto ya malezi, hali hiyo imewalazimisha kubadili mifumo ya maisha ili kuzilinda familia zao.


“Nimelazimika kuhamia Goba kuwakwepa ‘madada poa’ na kelele za usiku kucha. Jirani na nyumba niliyokuwa naishi na familia yangu kuna gesti wanayotumia hao madada poa. Wanavuta bangi usiku kucha na asubuhi tunapotoka tunakuta kondomu zimetapakaa hadi magetini kwetu.

“Wakati mwingine wateja wao wanapaki magari yao kwenye uzio wa nyumba zetu na kuyatumia kufanya mapenzi badala ya kwenda gesti. Tumeripoti sana polisi hatuoni nafuu yoyote,” anasema Ally Mohamed aliyekuwa akiishi katika nyumba moja, nyuma ya baa ya Meeda, maarufu kama Kitambaa Cheupe.

Anaongeza kuwa “changamoto ya kulea watoto kule ilikuwa kubwa kwa kuwa akirudi saa moja usiku anakuta tayari (madada poa) wamejipanga mtaani, wakiona gari wanajiachia uchi, kumbe mtu unakwenda nyumbani akiwa na watoto.”

Mohamed anasema baadhi ya familia, kama ilivyo kwake, zimehama kuepuka kero na adha za ukahaba pamoja na kelele zinazotoka kwenye kumbi za starehe.

“Kuna wengine wameacha nyumba na kuzipangisha. Zimekuwa ‘gesti bubu’ (nyumba za kulala wageni zisizo rasmi) zinazotumiwa na machangudoa (makahaba),” anasema.

Mkazi mwingine wa Sinza A, Eva Selasini anasema makahaba hao wamewaweka katika wakati mgumu kutokana vitendo wanavyofanya usiku na mchana.

“Ni changamoto kubwa. Giza linapoingia huwezi kumtuma mtoto dukani, kama basi la shule limechelewa mzazi unapata wasiwasi kuwa mwanao ataona vitu asivyostahili kuviona kwa umri wake,” anasema mama huyo wa watoto wawili.

Kwa mujibu wa Eva, hofu ya wanaye kuona matukio yanayoendana ya biashara ya ukahaba haipati usiku pekee, bali hata asubuhi wakati mtoto wake akielekea shuleni.

“Mwanangu anapitiwa na basi saa 11:40 asubuhi, muda huu akina dada wanaojiuza wanakuwa bado wametanda mitaani, hivyo wanatuweka kwenye wakati mgumu kulea watoto wetu katika mazingira haya,” anaongeza.



Serikali za mitaa zaelemewa
Viongozi wa Serikali za mitaa Sinza wamekiri biashara ya ukahaba imekithiri katika baadhi ya maeneo yao ya utawala na kuongeza ugumu katika kazi yao.

Mwananchi limebaini kuwa makahaba wameteka kando eneo la kando ya Barabara ya Sam Nujoma kuanzia Mlimani City hadi katika baa maarufu ya 5N Pub & Night Club.

Eneo lingine ambalo biashara hiyo imekithiri ni eneo la Sinza Mori karibu na Corner Bar na klabu ya usiku ya Boardroom pamona na eneo la Meeda Bar maarufu kwa sasa kama Kitambaa Cheupe.

Baadhi ya wakazi wamehama na kugeuza nyumba zao gesti kisha kuzipangisha kwa wamiliki wa kumbi za starehe ili kujiepusha na adha walizokuwa wakizipata.

Uchunguzi wa Mwananchi onaonyesha pia kuwa makahaba wengi wanaojiuza usiku wamepanga katika nyumba zilizo katika makazi ya watu na wateja wanaowapata hulazimika kwanza kulipia chumba anachopelekwa na kahaba kabla ya kulipia huduma nyingine.

Wapo pia waliopanga vyumba katika nyumba za wageni zilizopo katika eneo hilo, hawa huwalipisha wateja wao kulingana na hadhi na gharama ya gesti husika.

“Tatizo hili lipo na nimekuwa nikipokea malalamiko ya wananchi ofisini na kwenye mikutano ya wananchi. Lalamiko lao kubwa ni kwamba biashara ya ukahaba inafanyika hadi asubuhi na baadhi yao huonekana wakifanya mapenzi pembezoni mwa nyumba zao,” anasema Ally Mgaya, mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Sinza A wenye wakazi zaidi ya 6,000.

Mgaya pia anasema makahaba wamesababisha changamoto kubwa za malezi ya watoto wa eneo lake.

“Katika mazingira ya kawaida hali hii inasababisha ugumu katika malezi ya watoto,” alisema.

Eneo lingine lililokumbwa na madhila ya biashara ya ukahaba ni Mtaa wa Nzasa, wenye wakazi zaidi ya 6,600.

Makahaba pia wamevamia maeneo ya Sinza Mori na mitaa iliyopo jirani na baa ya Meeda (Kitambaa Cheupe) na pembezoni mwa Shule ya Msingi Mapambano.

“Tatizo linakuwa kwa sababu ya uwepo wa baa na baada ya kufunguliwa baa ya B Max na Boardroom kumesababisha kuongezeka kwa hao watu ambao hufuata maeneo wanayoweza kufanya biashara kwa urahisi,” anasema Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Nzasa, Edwin Mfanga.

Anasema kumekuwa na malalamiko ya makahaba kufanya mapenzi na wateja wao katika magari na vichochoro vilivyo kwenye makazi ya watu.

“Mara nyingi tunawakamata kwenye vichochoro kwenye giza. Unakuta gari kichochoroni unadhani limepaki kumbe watu wanafanya vitu vyao,” anasema kiongozi huyo.

Hata hivyo, anasema makahaba wengi si wakazi wa Sinza. “Wengi tuliowahi kuwakamata wanatokea Manzese, Mbagala, Tandale na Mlalakuwa, wachache sana ni wakazi wa Sinza.”

Anakiri kupokea malalamiko ya wazazi kuhusu changamoto ya kulea watoto katika mazingira hayo.

“Malalamiko yamekuwa mengi sana. Asubuhi watoto wakitoka wanawaona ‘dada poa’ wametanda mitaani, wananchi wanakuta kondomu zilizotumika nje ya mageti yao na wakati mwingine watu wanajisaidia karibu na nyumba zao.


Hakuna sheria
Kukosekana kwa sheria mahususi ya kupambana na biashara ya ukahaba kumeelezwa kukwamisha jitihada za kukomsha tatizo hilo.

Operesheni nyingi za kuwakamata zimefanywa na polisi na viongozi wa Serikali za mitaa lakini wameishia kukamatwa na kushtakiwa kwa kosa la uzururaji na kuachiwa baada ya kulipa faini

“Kosa pekee wanaloweza kushitakiwa nalo ni uzururaji, kwa hiyo tumeishia kufanya operesheni za kuwakamata lakini haupiti muda wanarudi mtaani,” anasema Mgaya, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Sinza A.

Kiongozi mwenzake wa Mtaa wa Nzasa, Mfanga, anasema kukosekana kwa sheria yenye nguvu ya kuwatia hatiani makahaba na kumewapa changamoto kupambana na tatizo.

Ugumu kutunga sheria dhidi yao

Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho katika Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, Fulgence Massawe ansema Tanzania haina sheria ya kupambana na ukahaba moja kwa moja na kwamba ni vigumu kutunga sheria ya kuwatia watu hatiani kwa ukahaba.

“Mimi nikisema wewe ni mwizi lazima nionyeshe umeiba nini na ndio maana unapomkamata mtu kwa ukahaba lazima uonyesha alikuwa anafanya kitendo gani cha kuthibitisha ukahaba.

“Kuthibitisha ukahaba lazima uende zaidi ya kukamata mtu anayesimama pembezoni mwa barabara. Huo ndio ugumu na ndio maana wanaishia Mahakama ya Jiji. Kinachofanyika pale hakiwasaidii zaidi ya kuwadhalilisha tu,” anasema.

Massawe anaona kuongezeka kwa biashara ya ukahaba ni kielelezo cha kuongezeka kwa mmomonyoko wa maadili na ugumu wa maisha.

“Maadili hayalazimishwi kwa kutungiwa sheria na hata ukitunga sheria ni vigumu kuitekeleza kwa sababu anayetenda na anayetendewa wanakuwa wamekubaliana, sasa wewe unaanzia wapi kuwashtaki?” anahoji.

Anasisitiza kuwa njia pekee ya kupambana na tatizo hilo ni kuwafanya wasichana wajitambue, kupunguza ugumu wa maisha na taifa lijue lilikosea wapi kiasi cha maadili kuharibika ili hali hiyo ianze kurekebishwa.

Mkazi mwingine wa Mtaa wa Nzasa anasema kuna kila dalili kuwa kufurika kwa makahaba kumewaelemea viongozi wa serikali za mitaa.

“Maeneo yanayozunguka baa ya Meeda (Kitambaa Cheupe) ni balaa! Ukiripoti Serikali ya Mtaa utaona madada poa wanapotea wiki halafu wanarudi tena. Mume wangu anachukuaga hadi fimbo anakwenda kuwachapa.

“Asubuhi watoto wanapokwenda shule yaani ni aibu, kondomu zimetupwa hadi mlangoni. Kuna Jumamosi moja wanajumuiya walikuja kusali hapa kwangu wakakuta kondomu getini,” anasema dada mmoja anayeishi nyuma ya baa maarufu ya Meeda.

Mkazi mwingine wa Sinza A, Theodora Aloyce, 48, anasema hali hiyo imetokana na mamlaka kuruhusu kuwepo kwa baa kubwa na kumbi za starehe kwenye makazi ya watu.

“Inaleta ugumu sana kulea, watoto wetu wanatamani kuiga, wanadhani hayo ndiyo maisha, kuweka mabaa makubwa kwenye makazi ya watu ni shida! Kelele usiku kucha,“ analalamika.

Florence Mapigano, mjane wa aliyewahi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu, Dan Mapigano analalamika kuwa watu wasiowajua huegesha magari nje ya mageti yao usiku na kufanya vitendo vichafu.

“Magari yanapaki nje ya mageti yetu, wanalewa, wanafanya uchafu, asubuhi utakuta chupa za mikojo, za bia na kondomu. Hali hii imetuathiri sana sisi tunaotaka kukaa katika nyumba zetu kwa amani. Sinza sasa imeanza kuwa kitovu cha mambo haya ya machangudoa,” anasema Bi Florence.

Mkazi wa Mtaa wa Arusha, Sinza A, Lilian Urio naye anaeleza kukithiri kwa biashara ya ukahaba Sinza kuwa kumewafanya wazazi wengi kuhama.

“Kama wewe ni mzazi na uko responsible (unawajibika) ku-protect (kuwalinda) watoto wako utafanyaje katika hali hii, zaidi ya kuhama? Ama uhame au ujue kuongea na watoto wako vizuri,” anasema.

Anasema kufunguliwa kwa baa nyingi kubwa na ndogo kumewavutia makahaba kutoka sehemu mbali mbali kuja Sinza.

“Wamiliki wengine wa baa wanawaita (makahaba) ili wavutie wateja, muda wote hawa dada poa wako barabarani hadi muda wa saa 1 asubuhi. Yaani kusema ukweli watu wa maeneo haya tuko katika wakati mgumu sana,” anasema.

Mwananchi limebaini pia kuwa makahaba wengi huamua kumalizana na wateja wao kwenye vichochoroni vilivyopo kwenye mitaa ya makazi ya watu.

“Utakuta kondomu zimetapakaa mitaani. Yote hii ni kwa sababu ya kuongezeka kwa baa na majumba ya starehe za usiku. Maeneo yetu malezi yamekuwa magumu sana,” anasema Urio.

Urio na mkazi mwingine wa eneo hilo, Mohamed Mauj wanasema kwa nyakato tofauti kuwa eneo linalozunguka baa ya Kitambaa Cheupe biashara hiyo hufanyika mpaka saa 1:30 asubuhi siku za mwisho wa wiki.

“Usiku barabara zote hazina ustaarabu, huwezi kupita na watoto. Mbali na makahaba, kelele pia ni kubwa mno. Baa zinapiga muziki mkubwa hadi saa 1 asubuhi. Unatupigia kelele wakati sisi hatuna shida ya kelele, hizo kelele ni za wateja wako kwa nini unataka na sisi majirani tusilale?

Polisi wafuatilia
Alipotafutwa kueleza ni hatua gani wanazochukua kupambana na hali hiyo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro alisema wanafuatilia suala hilo.

“Tutafuatilia suala hilo, asante kwa taarifa,” alisema alipozungumza na Mwananchi kwa njia ya simu.
 
Eti biashara ya ukahaba imevamia Dar!
Ni lini kulikuwa hamna ukahaba?
Ukahaba ni the most oldest profession in the world
 
Hii biashara inatakiwa iwe regulated
 
Lazima uwe na mipango mbadala ya miongo mitatu au minne katika eneo unaloishi, maana yake ni kuwa eneo lako la kuishi kwa sasa hata kama umejenga miaka thelathini ijayo halitakuwa lina kufaa tena, kama kinakufaa aidha ni kwa ajili ya biashara na sio kuishi mwenyewe.

Tunashauriwa pia kuwa na mashamba pamoja na makazi yenye miundombinu bora pembezoni mwa miji mikubwa, hii itatusaidia kwenda kuishi huko baadae umri unaposogea.

Somo hili nilijifunza kutoka kwa mzee wangu, miaka ya themanini tulihamia mikocheni ilikuwa ni mashambani ila baada ya miongo mitatu, wazee hawakutamani tena kuishi pale wakahamia pembezoni.

Jiulize mahali unapo ishi leo baada ya miaka ishirini au thelathini patakufaa? utakuwa umejiandaa kwa ustaarabu wa kizazi kingine kipya?

Usisubiri kustaafu au kuchoka, watu wenye akili hupanga maisha yao ya baadae kwa kufanya maandalizi ya sehemu watakazo ishi umri ukisogea.

Maisha ni kupanga na kupanga ni kuchagua, tusikubali kuishi kama miti mikubwa ya mibuyu.
 
wakazi wa Dar bwana kwa kiki,

Washindwe kuhama kule Jangwani kwenye mafuriko waje kuhama sababu ya wauza Utamu?[emoji23][emoji23][emoji23]

wanaume wa Dar ni hopless kabisa
Wakati huko mikoani watu wanakaa karibu na mbuga ya wanyama pori wanaume wa dar wanakimbia kisa kelele kweli dar ni majanga.
 
wakazi wa Dar bwana kwa kiki,

Washindwe kuhama kule Jangwani kwenye mafuriko waje kuhama sababu ya wauza Utamu?[emoji23][emoji23][emoji23]

wanaume wa Dar ni hopless kabisa

[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]aiseeeeeee
 
wakazi wa Dar bwana kwa kiki,

Washindwe kuhama kule Jangwani kwenye mafuriko waje kuhama sababu ya wauza Utamu?[emoji23][emoji23][emoji23]

wanaume wa Dar ni hopless kabisa
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] shangaa nawee
 
Back
Top Bottom