Bibi zake mke wangu wakikosa pesa ya kulipa ada wanaanza kutumia mabavu nilipe mahari

Kwanini wewe ukipewa zawadi unaipeleka wapi....??
Mahari sio zawadi, hakuna zawadi inayodaiwa au kuwa bargained/ kufanyiwa makubaliano kupitia mazungumzo ya mapatano kabla haijatolewa.
 
Nani kawaambia mahari haitakiwi kuisha ? Ni imani za mtaa au imani za kidini? Kama kwa upande wa Dini kwa waislam mahari ni deni inatakiwa ilipwe haraka sana kabla hujafa na ukifa ukiwa na deni hilo ndugu zako wanatakiwa wakulipie
Binadamu nwenzako sio kama furushi la viazi
 
Mahari sio zawadi, hakuna zawadi inayodaiwa au kuwa bargained/ kufanyiwa makubaliano kupitia mazungumzo ya mapatano kabla haijatolewa.
Huo ni mtazamo wako binafsi au umenukuu mahali....??
 
Nani kawaambia mahari haitakiwi kuisha ? Ni imani za mtaa au imani za kidini? Kama kwa upande wa Dini kwa waislam mahari ni deni inatakiwa ilipwe haraka sana kabla hujafa na ukifa ukiwa na deni hilo ndugu zako wanatakiwa wakulipie
👊👊
 
How can anyone seriously believe this kind of nonsense?!
 
How can anyone seriously believe this kind of nonsense?!
Tunaishi katika ulimwengu wa watu mbali mbali wenye maoni, mitazamo na mitindo ya maisha tofauti tofauti kulingana na jamii inayokuzunguka!!!

Msawazo na ustaarabu katika matumizi sahihi ya ufahamu ni kuchunga mipaka yako kwenye utaratibu wa watu wengine kwenye maisha yao!!!
 
Ulitaka ninukuu wapi?
Katika jamii zetu kuna watu wanayaendesha kufuatana na miongozo yao ya kiimani na kuna wengine huyaongoza maisha yao kulingana na utashi wao wenyewe.....

Sasa sijajua kwa upande wako tunayaongelea haya katika mlango upi wa muongozo wako wa maisha!!
 
Ushauri kwa Waislamu, nimetaja waislamu makusudi ili wapuuzi wengine wasiliingilie hili

Muislamu tambua mahari ndio inakupa uhalali wa kumuingilia huyo mke wako,kwahiyo ule ujinga wa kusema mahari haimaliziwi sio katika Uislamu

Ila unayo ruhusa ya kutoa kidogo kidogo kama hali sio nzuri,ila azimia kumaliza haraka iwezekanavyo

Pili mahari ni ya mke sio ya baba wala mama,kwahiyo wazazi wa kiislamu hiyo sio haki yenu hata kidogo

Na haya mambo sijui mkaja au koti la babu ni Mila tu lkn sio dini hiyo,kama mnataka kula hela basi ni hiyo ya Mila lkn sio mahari
 
Kama usumbufu wote huo unatokana na mahali iliyobaki, jikusanye malizia mahali yao halafu usiwe na muda nao.

Kata mazoea na wao.
Ni hii ndio njia pekee ya kufanya,kama alikubali hiyo mahari basi alikubali huo mkataba wa kimila,kwahiyo Aache kulialia Amalize deni la watu
 
Siku moja shem wenu kwenye stori aliniambia kwamba nikienda kwao kuoa dada zake wataniita na kuniambia kwamba nimemchukua mdogo wao akiwa mzuri, hana makovu, anan'gaa na kwamba kwao hajaua Nikimchoka nimrudishe hivyohivyo na kwamba wasisikie hata nimemuelewesha jambo kwa Makofi japo mara mojamoja kwa mwaka.
Nikamjibu kwamba atakaejaribu hayo maneno ya shombo hataamini dharau atakayoambulia palepale harusini na kwamba kejeli na majungu ni sumu kwangu Wala wasijaribu.
Mzee mzima nilioa mwaka 2020 Wala sijawah kusikia hizo habari.
Nb. Mkuu inaonekana umeachia gap kubwa sana la kuonekana mnyonge hivyo washaanza na wamekuzoea kwamba bila mwana wao hutaishi kwa Raha .
Walezi wenye adabu na fikra nzuri swala la kumtoa mtoto wao kwa mume kisa wamepishana nawewe Huwa ni kitu kisicho na maana na hawathubutu kufanya
 
Vipi hao mke na mume wakiachana? Undugu wa wa hizo familia bado utaendelea?
Ndiyo maana wana watoto tayari ambao watawaunganisha daima. Kama hakuna watoto bado ndoa katika familia hizo mbili haiwezi kutokea
 
Ni hii ndio njia pekee ya kufanya,kama alikubali hiyo mahari basi alikubali huo mkataba wa kimila,kwahiyo Aache kulialia Amalize deni la watu
Ni kweli mkuu.
Kama wana aibu nao watakata usumbufu. Lakini kama ni familia isiyo na aibu hata mahari ikimalizika watakuja na usumbufu wa kuomba huduma.

Kitakachomuokoa ni msimamo wake.
 
Endelea kulipa kidogo kidogo mpaka umalize deni
 
mpaka wanakufanyia hivyo walishakuona zuzu toka kipindi unaanza maswala ya kulipa mahari na mipango ya ndoa..... iko hivi pale unapokwenda kupiga ukwe ndipo wanapata naasi ya kukuona upoje kama ulienda kinyonge baaass umekwishaaa kama ulionyesha kumyenyekea sana umekwisha kiufupi pale ndipo wanapia hili jaba zima au tulichekeche kwa namna gani..... swala la mahari sio ishu kubwa sana na ukionaje warudishie mtoto wao kama naye yupo upande wa hao mabibi temana nae katafute mwingine asiena mabibi.... wakikuzoea zaidi tomber hadi hao mabibi
 
Uko sahihi kabisa ndo maana nikasema hiyo familia kwanzia jamaa,ndugu wa mke na mke mwenyewe wote wana matatizo kila mmoja kati yao ana mtizamo ambao siyo wa sawa, wangekua wana uelewa wa ulichoandika huo mgogoro usingekuwepo .

Tatizo jamaa nae kadhamiria kutokumaliza mahari, ndugu nao wanaamini mahari ni haki yao, mke nae kakaa kimya akiamini mahari yake inatakiwa ilipwe familia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…