Bible Vs Science: Je ulimwengu una umri gani?

Yes, Maana Neno linasema Mwanzo: 1:14 : Mungu akasema, na iwe mianga katika anga la Mbingu, ili itenge kat ya Mchana na Usiku, Nayo ndiyo iwe dalili na Majira na Siku na Miaka.
Hivyo basi, With this ni kwamba,Hapa ndipo tunaweza kuanza kuhesabia hizo siku, Miaka Etc, maana Ndiyo dalili ya Majira, Siku na Miaka.
Kwa kusema hivyo basi Umri wa Dunia, unachezea kwenye hiyo 6000 hapo.

Samahani: Naomba UfafanUzi kidogo kuhusu kutofautisha EARTH, WORLD and UNIVERSE
 
mkuu unamaoni gani juu ya Kauli ya Bibilia kuwa Mungu mwenyewe anasema alifanya Yote kwa siku sita na siku ya saba akapumzika.
Je hapa alikuwa anawaficha nini waisrael?
Je hakujua kuwa vingine aliviumba kwa mamilioni ya miaka?
Je kuna code yoyote nyuma ya kauli hiyo ya moja kwa moja na iliyohitaji Practical obedience kwa wale jamaa huku akijua kabisa sio kweli wanachokifanya kuhusu siku sita za uumbaji.
Kumbuka tukio la uumbaji ndio lilimtenganisha Mungu wao na miungu mingine. Nadhani ni eneo ambalo Mungu Muumbaji aliwafunda vizuri wale jamaa ili wahifadhi hizo habari hadi kizazi hiki cha neema kwa wote waisrael wa kimwili na wakiroho.

unaweza kutia maarifa kidogo hapo mkuu.
 
Natamani Kiranga angekuwa japo na busara ndogo ya kuwa realistic kama wewe angepata heshima humu jamvini.
Lakini ukimchunguza Akili yake iko below reasoning level.
Nadhani kaka Sanctus ulipitia kwenye Theolojia yenye kukupelekea kuwa gnostic bila kujitambua. Polepole u-gnostic utatoweka muda wa kuwa na Sisi tumo humu Jamvini.
 
Wamepima kuanzia Adam alipoumbwa!
Mbona tunasoma humu ndani Kuwa Dunia ilikuwa ina watu kabla ya Ujio wa Adamu?

Samahani kama nitakuwa sijaeleweka maana sipo vizuri kwenye hizi mambo.


Upo sahihi kabisa kuwa watu walikuwepo kabla ya Adam.
 

ni kweli tunaanza kuhesabu siku, majira na Miaka baada ya uboreshaji wa Dunia kuwa sehemu sahihi ya kuishi, baada ya Dunia kupewa uhai na inawezekana ndio Hesabu ya hizo siku 6000 za uhai wa Dunia unapotoka, lakini Dunia bila uhai ilikuwepo kadiri ya Mwanzo 1:1-2
 

Dunia haikuumbwa kwa siku sita, Dunia ilikuwepo, ila ilikuwa Giza, Utupu na ukiwa, Yaani ilikuwa haina uhai Mwanzo 1:1-2, Mungu kwa muda wa siku sita akaitransform Dunia na kuiwekea mazingira ya kuweza kufanyika maisha kwa viumbe hai
Ukiangalia hakuna hata sehemu moja kwenye Biblia inapoonyesha kuwa Mungu anaumba maji, au Miamba, bali tunaona katika hizo siku sita anaitenga miamba na maji, yaani anavitenga vitu vilivyokuwepo, vitu alivyoviumba katika Mwanzo 1:1-2
 
Mjadala mzito huu ila mi najuwa kunamiaka mingi hata hiyo million inaweza kuwa ndogo kwani sisi tumetokea wapi tukijuwa mwanzo wetu tunaweza juwa kuwa Ulimwengu na Mtoto wake dunia waliumbwa miaka mingapi iliyopita.
 
Idea kama zile licha kuwa na mapungufu, zipingwe kwa maandiko aliyotumia, au wanayotumia pro-creation scientists kwamba dunia haina miaka mamilioni bali miaka kama angalau elfu sita based to biblical genealogy ya Adam.

Kosa ambalo unafanya wewe na alilofanya John Ussher ni kusoma Creation Accounts Chronologically. Kuelewa kwamba Biblia katika Kitabu cha Mwanzo inaelezea kwamba lilianza tukio hili na kisha likafuata hili na kisha lile. Unapokisoma Kitabu cha mwanzo kuna vitu lazima uvielewe kwanza. Mfano lazima uelewe Thinking ya Waebrania kuhusu Time and Space, uelewe Lugha yao na Culture yao.

Ukitaka kuelewa kwamba Kitabu cha Mwanzo hakitupatia uumbaji Chronologically,naomba ujiulize swali: Mwanga unatokana na Jua na kinyume. Je,kwa mjibu Wa Sura 1:3, mwanga ndio ulianza kuumbwa na kisha ndio Jua na Mwezi na Jua vikaumbwa( Mwa 1:16) . Je,kama mambo yalifanyika Chronologically, hali hiyo iliwezekana vipi? Kwamba Mwanga uanze na kisha ndio Jua liumbwe wakati Jua ndio linatoa Mwanga?

Kwanza:

" 3 Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.
4 Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza."

Kisha:

"16 Mungu akafanya mianga miwili mikubwa, ule mkubwa utawale mchana, na ule mdogo utawale usiku; akafanya na nyota pia. 17 Mungu akaiweka katika anga la mbingu, itie nuru juu ya nchi."

Kwa hiyo, kwa nukuu hizo hapo utagundua kwamba Kitabu cha Mwanzo hakitupatii maelezo ya kisayansi jinsi Ulimwengu na Dunia vilivyoumbwa Chronologically Bali Kitabu kitabu hicho kinaeleza na kujibu Maswali yafuatayo: Who, Why and What juu ya Uumbaji.
 
jamvini.
Lakini ukimchunguza Akili yake iko below reasoning level.
Nadhani kaka Sanctus ulipitia kwenye Theolojia yenye kukupelekea kuwa gnostic bila kujitambua. Polepole u-gnostic utatoweka muda wa kuwa na Sisi tumo humu Jamvini

Usiwe na haraka ya kunihukumu hivyo. Mimi nitakuwa nawapeni Maswali ya kujiuliza na ukiona jibu au uelewa ulio nao una-contradict Facts za Kisayansi,Historia, Culture au thinking ya waandishi au audience kwa muda huo basi ujue hicho ulicho nacho ndio matangopori.

Hebu soma Mwa 1:3 na Mwa 1:16 halafu rudi hapa uniambie kama Logically inawezekana. Kama haiwezekani ndio ugutuke kwamba kumbe Kitabu cha Mwanzo hakielezi Uumbaji Chronologically.
 
Kaka mkubwa nakuelewa haya majibu yangemfikia pia

Cc@Nyabhingi
 

Ina maama Adamu aliumbwa wakati mmoja au muda sawa na ilivyoumbwa dunia au wewe una maanisha nini ?
 
umri wa dunia probably wanasayansi wako sawa 4.5 b years,vile vile hata upande wa bible maana kuna FUMBO KUBWA SANA KATIKA KITABU KINACHOELEZEA creations ya ulimwengu hasa MW 1:1 na Mw1;2 hizi ni dunia mbili tofauti,wachambuzi wanasema ile dunia ya MWZ 1:1 ilifall to entropy baada ya shetani kumuasi MUNGU,hivyo ya kwenye Mwz 1;2 ni matokeo ya ile ya kwanza kufa nahivyo basi kilichofanyika katika hii sio creation ni regenetions.
SOMA HAPA KUHUSU CREATIONS UTAELEWA MENGI www.kjvbibl The Bible, Genesis and Geology
 

Tatizo wanasayansi kuna mambo wanashindwa kuyathibitisha juu ya suala la uumbaji.
 
wakolosai 1:16
Yeye ndiye ali yeumba vitu vyote mbinguni na duniani; vitu vinavyoonekana na visivyoonekana; kama ni viti vya enzi au nguvu, au watawala au milki na mamlaka: vyote viliumbwa na yeye kwa ajili yake .

yohana 1:3
Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.

isaya 66: 2
For My hand made all these things, Thus all these things came into being," declares the LORD "But to this one I will look, To him who is humble and contrite of spirit, and who trembles at My word.
waefeso 3:9 Mungu aliumba kila kitu.

Ukiona hapo kwa mujibu wa bibilia bila kujali mchanganyiko wowote unaoweza kujitokeza mwanzo 1/2
Mungu kaumba kila kitu hadi maji ambayo hayajatamkwa.

Oanisha ni Kauli ya Mungu akirefer matukio ya Mwanzo 1 na 2

Kutoka 20:11
For in six days the Lord made the heavens and the earth, the sea, and all that is in them, but he rested on the seventh day. Therefore the Lord blessed the Sabbath day and made it holy.

sasa naomba maoni yako hapa. Je Tupingeje hii kauli ya Mungu na bibilia au uchambuzi gani wa siri unabatilisha hili mkuu.

cc SANCTUS ANACLETUS
 
Hii mada mbona imekuwa mpya sana kichwani kwangu?sijawahi kufikiri hata siku moja kuhusu umri wa Dunia.......ila leo nimeanza rasmi japo sio kwa umuhimu lakini huu uzi iko siku ntaleta majibu sahihi hapa(mwaka wowote)nikifanikiwa kupa jibu
 
nakupata kwa uzuri, kuna mambo kadhaa kwenye maelezo yako haya mkuu.

1:Hiyo thinking ya waebrania ni siri au, maana hujaitumia kuthibitisha Mungu ambaye sehemu zote anasema ameumba kila kitu duniani. Na Mungu huyohuyo akasema Ameyafanya Yote kwa siku Sita na Saba akapumzika.
Nyoosha maelezo ukipinga na maelezo niliyokupa huko juu Kuhusu uumbaji.

2: Hao waebrania ambao hata leo wapo japo hawamuamini Yesu, Unauhakika wanaamini Mungu hakuumba dunia kwa siku sita au sisi waebrania wa kisasa huku bongo tunauelewa mkubwa kuliko walengwa?

3:Kuhusu Jua na Mwanga, Sioni sababu ya Kumpangia Mungu mkuu. IKiwa alikuwa Workshop anatengenza Dunia anauhuru wa kutengeneza Mwanga kisha aweke system ya mianga maana hata mwezi sio kila siku upo usiku. Hivyo Kusema chanzo cha mwanga kilibidi kiwe jua tu hata kama lilikiwa halijaumbwa ni kumfanya Mungu kuwa na uwezo finyu katika uumbaji wake.

4: Kama aliumba Nuru, Na licha ya Nuru kuwepo giza likawepo hadi alipotenganisha huoni kulikiwa na shughuli ambayo inayoendelea beyond our finite imagination. Hapo panahitaji kuchukua kauli za Mungu kama zilivyo kwa Mujibu wa Ufafanuzi wa Bibilia Yote. Ule mtiririko uko sawa kabisa, na ufafanuzi wa mwanzo 2 pia uko sawa.

Katika Mwanzo mkuu kuna 5W zote na 1H
who - Mungu, Yohana 1 pia ikatia Muhuli yote hayakufanyika bila Yesu pia
What - Dunia
When - Hapo mwanzo kwa siku sita mfurulizo.
Why - Ili Mwanadamu atawale na kuvitiisha vyote vilivyomo.
Where - Kutoka katika "SI KITU" hadi Vitu au Dunia na Vitu Vilivyomo.

How
Kwa Kutamka na Vitu vikawa. Katengeneza na interdependent and self supporting system, Mmiliki Mwanadamu akamfanya kwa mavumbi ya ardhi, na akatengeneza system ya kuendeleza kizazi.
Hiyo chronological ni scientific kabisa mkuu. Na wapo wanasayansi wengi wanaoamini huo uumbaji wa siku sita hata kama sio wakristo lkn wanauchambua scientifically hadi raha. Jaribu kujifunza katika stream zote sio kwa wapinga Mungu tu.

Chanzo cha migogoro unayojitengenezea kilianza Amri ya nne IlipoNYOFOLEWA katika Amri Kumi sasa inabidi itafutwe justification ya kuungaunga kupinga matukio halisi ya Mwanzo. Nimekuqmbiq Bibilia Yote, inapoquote matukio yq Mwanzo inayareferer kama matukio halisi. Yesu aliyeumba anarefer matukio hayo kama yalivyo.
Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke,

5 akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?
mathayo 19:4-5.
Leo wafuasi wa Yesu wa Kisasa tunataka kuyafanya siri, mara hoo hadi tukawahoji waebrania, mara hadi twende vyuoni.

Hujaonyesha pia mkuu Kuwa Mungu aliyesema Kaumba kila Kitu, alifanya yote kwa siku sita kuwa alidanganya au hao waebrania hawakumuelewa miaka yote na hawajamuelewa hadi kesho ila waebrania wa ulaya au italy wamemuelewa zaidi.

karibu kwa maoni mkuu
 
For in six days the Lord made the heavens and the earth, the sea, and all that is in them, but he rested on the seventh day. Therefore the Lord blessed the Sabbath day and made it holy.

Hiyo bold siyo ushahidi kwamba kweli Dunia iliumbwa kwa siku Sita. Ulichofanya kuendelea tu kulieza wazo lako la uumbaji kwa muda Wa Siku. Hebu unaweza kurejea kwenye la Kiebrania "Yom" lenye maana ya siku uone lilipotumika muda ule lilimaanisha nini na " Bara" lenye maana ya Create lilikuwa na maana gani? Haya yatakusaidia kuanza kuelewa Ninachokiongelea.
 
Pia kama mkuu Sala na Kazi alivyotoa hoja, kwa sababu science ni progressive kila siku wanavumbua mapya wanaweza kuvumbua kile ambacho tunakisema pia, ingawa trend haionyeshi hilo.
mkuu mitale na midimu binafsi nimejaribu kusoma post zako kwa umakini. kuna baadhi ya maelezo yako nilitaka kukukanusha na pia nimefikiria kukuuliza maswali kadhaa kuhusu hoja na misimamo yako hasa juu matumizi ya sayansi, roho mtakatifu na biblia. lakini nimeona haina haja kwa sasa sababu post zako nyingi zinaonesha ni namna gani unavochanganya TAFITI ZA KISAYANSI NA BIBLIA. zinaonesha ni namna gani unavolazimisha TAFITI ZA KISAYANSI, ziwe poved na BIBLIA ilihali sayansi ina principle zake na bihlia ina principle zake kama kitabu cha KIIMANI na sio kitabu cha sayansi au philosophy. ndio maana kuna msemo unaosema kuwa "inapoishia sayansi ndipo imani inapoanzia"

kiujumla unalazimisha BIBLIA ithibitishe mambo ya kisayansi jambo ambalo nisawa na kulazimisha SAYANSI ithibishe mambo ya KIIMANI, imani na sayansi wapi na wapi mkuu.

kwenye sayansi na falsafa.hakuna neno IMANI/KUAMINI huko wanaongozwa na REASONING AND PRINCIPLES TU. hivyo mkuu kudai uthibitishoa wa masuala ya sayansi kwa kutumia biblia huko ni kuionea sayansi kwani sio kazi yake.

hivyo kwa muktadha huo niliokuonesha hapo juu binafsi ninaona huu mjadala unakuwa mgumu na haufiki mwisho zaidi ya kuzungukana tu. ndio maana kuna mchangiaji mmoja hapo juu unamdai uthibitisho wa mistari ya biblia katika hoja za kisayansi kitu ambacho kiukweli huwezi kikupata popote pale yaani kuprove hoja za kisayansi kwa mistari ya biblia hii haiwezani mkuu. uthibitisho wa kisayansi una formula na principle zake mkuu na sio mistari ya biblia.

mpendwa mitale na midimu binafsi ninafikiri kama Mungu angekusudia biblia kutufundisha sayansi/kutueleza kweli za kisayansi kinagaubaga kusingekuwa na haja ya wanasayansi, tafiti za kisayansi na sidhani kama Mungu angetuagiza tumpende kwa AKILI yetu yote nk kwani kila kitu, kila fomula na kila aina ya sayansi angetuwekea kwenye biblia na pia tusingekuwa tuna haja ya kusoma sayansi mashuleni nk cha msingi tunapaswa kumwomba roho mtakatifu atuongoze na kutusaidia kutambua pande POSITIVE na NEGATIVE za sayansi ilikulinda Imani yetu na mwisho kuufikia uzima wa milele.

wapendwa @zito junior SANCTUS ANACLETUS na mitale na midimu mtizamo wangu ni huu masuala mazima ya sayansi naamini katika tafiti za kisayansi na majibu ya kisayansi iwapo hayapingani na imani. na masuala mazima ya kiimani kuhusu Mungu na ulimwengu wa roho naamini katika biblia neno la Mungu. mapokeo matakatifu na mamlaka rasmi ya ufundishaji ya kanisa

vinginevyo kuendelea kuchanganya sayansi na biblia kitabu kielezeacho kweli za kiimani sidhani kama tunaweza kufika mwisho wa mjadala zaidi kulumbana.

hayo ni maoni yangu wapendwa.
 
Ina maama Adamu aliumbwa wakati mmoja au muda sawa na ilivyoumbwa dunia au wewe una maanisha nini ?
Hapana nachomaanisha je Dunia hii ina umri gani na sio VIUMBE vina umri gani maana obvious Dunia lazima iliumbwa kwanza kabla ya mwanadamu hivyo natamani nifahamu upi ni umri sahihi wa Dunia ni ipi maana Ussher alichosema ni kwamba Dunia iliumbwa siku sita kabla ya Adam kuletwa duniani na ndio maana nikaona nilete hii mada humu tusaidiane kujua nani mkweli kuhusu suala hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…