Kosa ambalo unafanya wewe na alilofanya John Ussher ni kusoma Creation Accounts Chronologically. Kuelewa kwamba Biblia katika Kitabu cha Mwanzo inaelezea kwamba lilianza tukio hili na kisha likafuata hili na kisha lile. Unapokisoma Kitabu cha mwanzo kuna vitu lazima uvielewe kwanza. Mfano lazima uelewe Thinking ya Waebrania kuhusu Time and Space, uelewe Lugha yao na Culture yao.
Ukitaka kuelewa kwamba Kitabu cha Mwanzo hakitupatia uumbaji Chronologically,naomba ujiulize swali: Mwanga unatokana na Jua na kinyume. Je,kwa mjibu Wa Sura 1:3, mwanga ndio ulianza kuumbwa na kisha ndio Jua na Mwezi na Jua vikaumbwa( Mwa 1:16) . Je,kama mambo yalifanyika Chronologically, hali hiyo iliwezekana vipi? Kwamba Mwanga uanze na kisha ndio Jua liumbwe wakati Jua ndio linatoa Mwanga?
Kwanza:
" 3 Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.
4 Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza."
Kisha:
"16 Mungu akafanya mianga miwili mikubwa, ule mkubwa utawale mchana, na ule mdogo utawale usiku; akafanya na nyota pia. 17 Mungu akaiweka katika anga la mbingu, itie nuru juu ya nchi."
Kwa hiyo, kwa nukuu hizo hapo utagundua kwamba Kitabu cha Mwanzo hakitupatii maelezo ya kisayansi jinsi Ulimwengu na Dunia vilivyoumbwa Chronologically Bali Kitabu kitabu hicho kinaeleza na kujibu Maswali yafuatayo: Who, Why and What juu ya Uumbaji.
nakupata kwa uzuri, kuna mambo kadhaa kwenye maelezo yako haya mkuu.
1:Hiyo thinking ya waebrania ni siri au, maana hujaitumia kuthibitisha Mungu ambaye sehemu zote anasema ameumba kila kitu duniani. Na Mungu huyohuyo akasema Ameyafanya Yote kwa siku Sita na Saba akapumzika.
Nyoosha maelezo ukipinga na maelezo niliyokupa huko juu Kuhusu uumbaji.
2: Hao waebrania ambao hata leo wapo japo hawamuamini Yesu, Unauhakika wanaamini Mungu hakuumba dunia kwa siku sita au sisi waebrania wa kisasa huku bongo tunauelewa mkubwa kuliko walengwa?
3:Kuhusu Jua na Mwanga, Sioni sababu ya Kumpangia Mungu mkuu. IKiwa alikuwa Workshop anatengenza Dunia anauhuru wa kutengeneza Mwanga kisha aweke system ya mianga maana hata mwezi sio kila siku upo usiku. Hivyo Kusema chanzo cha mwanga kilibidi kiwe jua tu hata kama lilikiwa halijaumbwa ni kumfanya Mungu kuwa na uwezo finyu katika uumbaji wake.
4: Kama aliumba Nuru, Na licha ya Nuru kuwepo giza likawepo hadi alipotenganisha huoni kulikiwa na shughuli ambayo inayoendelea beyond our finite imagination. Hapo panahitaji kuchukua kauli za Mungu kama zilivyo kwa Mujibu wa Ufafanuzi wa Bibilia Yote. Ule mtiririko uko sawa kabisa, na ufafanuzi wa mwanzo 2 pia uko sawa.
Katika Mwanzo mkuu kuna 5W zote na 1H
who - Mungu, Yohana 1 pia ikatia Muhuli yote hayakufanyika bila Yesu pia
What - Dunia
When - Hapo mwanzo kwa siku sita mfurulizo.
Why - Ili Mwanadamu atawale na kuvitiisha vyote vilivyomo.
Where - Kutoka katika "SI KITU" hadi Vitu au Dunia na Vitu Vilivyomo.
How
Kwa Kutamka na Vitu vikawa. Katengeneza na interdependent and self supporting system, Mmiliki Mwanadamu akamfanya kwa mavumbi ya ardhi, na akatengeneza system ya kuendeleza kizazi.
Hiyo chronological ni scientific kabisa mkuu. Na wapo wanasayansi wengi wanaoamini huo uumbaji wa siku sita hata kama sio wakristo lkn wanauchambua scientifically hadi raha. Jaribu kujifunza katika stream zote sio kwa wapinga Mungu tu.
Chanzo cha migogoro unayojitengenezea kilianza Amri ya nne IlipoNYOFOLEWA katika Amri Kumi sasa inabidi itafutwe justification ya kuungaunga kupinga matukio halisi ya Mwanzo. Nimekuqmbiq Bibilia Yote, inapoquote matukio yq Mwanzo inayareferer kama matukio halisi. Yesu aliyeumba anarefer matukio hayo kama yalivyo.
Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke,
5 akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?
mathayo 19:4-5.
Leo wafuasi wa Yesu wa Kisasa tunataka kuyafanya siri, mara hoo hadi tukawahoji waebrania, mara hadi twende vyuoni.
Hujaonyesha pia mkuu Kuwa Mungu aliyesema Kaumba kila Kitu, alifanya yote kwa siku sita kuwa alidanganya au hao waebrania hawakumuelewa miaka yote na hawajamuelewa hadi kesho ila waebrania wa ulaya au italy wamemuelewa zaidi.
karibu kwa maoni mkuu