Biblia wanayotumia Wakotoliki na wanayotumia Walutheri pamoja na madhehebu mengine ni tofauti?

Biblia wanayotumia Wakotoliki na wanayotumia Walutheri pamoja na madhehebu mengine ni tofauti?

“Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda. ”
— Mathayo 16:18 (Biblia Takatifu)
Ndiyo hapo Yesu alipomkabidhi kanisa Mtume Petro
 
  • Thanks
Reactions: 511
Yesu hakuwa na dini. Dini imeanza siku ya Pentekoste pale waliponena kwa lugha (Matendo: 2) ndipo kanisa lilipoanza
Kanisa lilianza siku ya pentekost
Dini zilikuwepo kabla ya yesu

Dhehebu la kwanza lilianza vatican
 
  • Thanks
Reactions: 511
Yani Yesu akajiambia mwenyewe kua yeye ni mwamba na juu yake atajenga kanisa lake? Kama wewe ni mkristo, Soma biblia ukiwa umemuomba Roho Mtakatifu ili akufunulie uielewe

Mathayo 16 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁷ Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.

Kufuatia andiko hilo mwamba unaozungumziwa hapo ambao kanisa litajengwa juu yake sio Petro!!.. kanisa la Mungu halijawahi kujengwa juu ya mtu wala kujengwa na mtu.

Bali Mwamba uliokuwa unazungumziwa hapo ni huo ufunuo Petro alioupokea wa YESU kuwa NI KRISTO, MWANA WA MUNGU ALIYE HAI.

Juu ya ufunuo huo ndio kanisa lake litajengwa..Yesu Kristo ndio Msingi wa kanisa, YEYE NDIO MWAMBA IMARA ambao kanisa litajengwa juu yake..na si juu ya mtu mwingine. Ndio maana waumini wa kanisa la Mungu wanajulikana kama Wakristo, sio waPetro…Kwasababu msingi sio Petro bali ni Kristo.

Ili tulithibitishe hilo vizuri, tusome mistari ifuatayo.

1 Wakorintho 3:10 “Kwa kadiri ya neema ya Mungu niliyopewa, mimi, kama mkuu wa wajenzi mwenye hekima, naliuweka msingi, na mtu mwingine anajenga juu yake. Lakini kila mtu na aangalie jinsi anavyojenga juu yake.

11 Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, YAANI YESU KRISTO”.

Na wala Petro hajawahi kusema popote kwamba yeye ndiye Mwamba.

Zaidi sana katika waraka wake kwa kinywa chake mwenyewe aliandika na kusema na kushuhudia kwamba Yesu ndiye, Mwamba na tena ndiye Jiwe kuu la pembeni.

Tusome,

1 Petro 2:3-8 “ikiwa mmeonja ya kwamba Bwana ni mwenye fadhili.

4 Mmwendee yeye, JIWE LILILO HAI, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye heshima.

5 Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo.

6 Kwa kuwa imeandikwa katika maandiko Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima, Na kila amwaminiye hatatahayarika.

7 Basi, heshima hii ni kwenu ninyi mnaoamini. Bali kwao wasioamini,

Jiwe walilolikataa waashi, Limekuwa jiwe kuu la pembeni.

8 Tena, Jiwe la kujikwaza mguu, na MWAMBA WA KUANGUSHA maana hujikwaza kwa neno lile, wasiliamini, nao waliwekwa kusudi wapate hayo”.

Huyo ni Petro, anayesema maneno hayo!..Sasa ingekuwa ndio ule mwamba ambao kanisa litajengwa juu yake, si angejitaja wazi kabisa hapo kuwa yeye ndio huo mwamba..lakini tunaona anaushuhudia mwamba mwingine ambao ni YESU!.

Tafsiri ya jina Petro sio Mwamba bali ni “jiwe”..tena “jiwe dogo, la kurusha”..

Kwahiyo kwa hitimisho ni kwamba Yesu ndio Mwamba, na si Petro, au kuhani yeyote au mwalimu yeyote, au mchungaji yeyote, au padri yeyote, au papa yeyote au kasisi yeyote au mtu mwingine yeyote.

Mtu anayechukua nafasi hiyo ya Kristo na kusema yeye ni mwamba basi huyo ni mpinga kristo.
 
Hakua na dini yeye alikuja kwa ajili ya wote na baada yake ndio ukatokea Ukristo ambao ni wafuasi wa Yesu Kristo.
Haya aliyafanya akiwa wapi?
Kwa nini awepo hapo na si sokoni?

Luka 4 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
¹⁴ Yesu akarudi kwa nguvu za Roho, akenda Galilaya; habari zake zikaenea katika nchi zote za kandokando.
¹⁵ Naye alikuwa akifundisha katika masinagogi yao, akitukuzwa na watu wote.
¹⁶ Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome.
¹⁷ Akapewa chuo cha nabii Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa,
¹⁸ Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,
¹⁹ Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.
 
Wakatoliki ndiyo UKRISTU wenyewe na UKRISTU ni UKATOLIKI. Hao wengine ni WAPROSTESTANTI, ni wanakondoo waliopotea ila siku ya hukumu watarudhishwa kundini.

KAMWE usibishe utakacho elekezwa na kanisa KATOLIKI kwa kuwa ndiyo lililokuwapo wakati Yesu Kristu anaondoka siku ya Pentekoste. Yesu mwenyewe ndiye aliyemkabidhi Simon Petro wanakondoo. Matayo 16:18. Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda
Lakin Yesu hakumwabudu mama yake wala hakuagiza wanafunzi wake wafanye hivyo...
Wakatoliki hawana hata uhusiano na Hilo jina ukristo ila wamejipachika Tu ili kutawala watu huko Roma Zamani hizo
 
Kanisa lilianza siku ya pentekost
Dini zilikuwepo kabla ya yesu

Dhehebu la kwanza lilianza vatican
Hiyo ni historia yako ya uwongo. Bakia nayo wewe na wanao. Hiwezi kubadili ukweli kwa chuki yako kwa UKATOLIKI
 
  • Mshangao
Reactions: 511
Hiyo ni historia yako ya uwongo. Bakia nayo wewe na wanao. Hiwezi kubadili ukweli kwa chuki yako kwa UKATOLIKI
Tupe historia ya kweli
Unataka kusema romani ilianza kabla ga siku ya pentekoste sio
 
  • Thanks
Reactions: 511
Lakin Yesu hakumwabudu mama yake wala hakuagiza wanafunzi wake wafanye hivyo...
Wakatoliki hawana hata uhusiano na Hilo jina ukristo ila wamejipachika Tu ili kutawala watu huko Roma Zamani hizo
Hujui ukichoandika. Wakatoliki HAWAMUABUDU Bikira Maria bali wanamuheshimu. Katika maombi wanamuomba AWAOMBEE kwa Mungu. Acheni upotoshaji
 
Hujui ukichoandika. Wakatoliki HAWAMUABUDU Bikira Maria bali wanamuheshimu. Katika maombi wanamuomba AWAOMBEE kwa Mungu. Acheni upotoshaji
Biblia inasema hakuna wakukuombea
Na ndio sababu ya pazia kupasuka siku aliyokufa yesu kwamb sisi wenyewe tuingie uweponi mwa Mungu tumuombe shida zetu sio kuhani ama mtu fulan akakuwakilishe

Ndomana nasema romani sio ukristo maana wanapinga kitu wanachosema wanakiamini
 
  • Thanks
Reactions: 511
hata hivyo wakatolik, hawaamini katika biblia peke yake, wanaamini pia katika tamaduni,pia wanaweza kutunga jambo lao na ikawa hivo
mfano ubatizo wa watoto wachanga. biblia inasema unatakiwa kuamini kwanza ndo ubatizzwe wao wanasema siyo lazima
Kusema wanaongeza....Hakuna kitu kama hicho.
 
Tupe historia ya kweli
Unataka kusema romani ilianza kabla ga siku ya pentekoste sio
Hii hapa.
Roman Catholic imeanza Karne ya kwanza na Kiongozi wa kanisa akiwa Mt Petro (Mathayo 16:18). Anahesabiwa kama first pope

Kulikuwa hakuna dhehebu jingine hadi mwaka 1054 wakati the Great schism ambapo kanisa la Mashariki (Orthodox) lilijitenga kutoka kwenye Ukatoliki. Catholic ikabakia Vatican na Orthodox ikawa na makao yake makuu Constatinople (Istanbul ya sasa)

Then mwaka 1521 Martin Luther alijitenga na Ukatoliki.

Anglican ilitokea mwaka 1575 baada ya Mfalme Henry VIII naye akaanzisha Anglican church

Hellen White mwaka 1844 naye akaanzisha SDA

Nao mapentekoste wakatokea kipindi cha great depression mwanzoni mwa karne ya 19

Sasa na wewe nitajie kidhehebu chako ni kipi! Kama siyo nyie mnasali kwa MWAMPOSA
 
Unaelewa unachokiandika
Hujui ata roman ilianza 300bk
Yan unataka useme petro alikuwa papa
Wapi io imeandikwa
Petro hajawah kukanyaga vatikan yenu maisha yake yote
Na asingeweza kushiriki uchafu wa ibada zenu za kipagani

Andiko ilo halijasema alikuwa padri ila mm ntakuonyesha andiko linalosema petro hakuwa na hayo madhehebu yenu wala.mtume wowote

Kumbuka kanisa na dhehebi ni tofaut
Kanisa linafata maandiko tuu

Dhehebu halijali atakama si maandiko ila walikaa wakapitisha kwao ni safi

Kanisa la kwanza lilianza jerusalem sio vatikan
Ila dhehebu la kwanza ndo lilianza uko kwenye mji wa shetani vatican

Chochote unachokisema dhibitisha na maandiko
Ukiongeza kitu chochote ama ukapunguza kwenye maandiko ukafanya biblia iseme kitu ambacho hakikusema maandiko yansema
Utaongezewa mapigo yale ya ufunuo
Na ukipunguza utaondolewa sehem yako mbingun
 
Nimeamua Kukuchukulia Kama Mpuuzi mmoja Mpaka pale utakapoproove Ulichokuwa unasema kuwa Nilidanganya..

Shukrani kwa andiko lako refu Lisilokuwa na maana yoyote La kucopy na Kupaste..

Ushauri wangu wa mwisho kabisa Jitahidi Utafute sana Elimu maana huna hata kidogo
[/QUOTE

Elimu ipi?.
Ya unajimu na nyota,miti shamba,utabibu ama ya quantum physics?.

Turud kwenye swali langu,kama huwezi jibu sema.
Ni kwa namna hipi unataka nikuamini wewe na sio Muhammad ama Bi Aisha?.
 
Ni tofauti mkuu wakatoliki walikubali na vitabu vingine ambavyo vinakubaliana na mafundisho yao mengine ya uongo kama kuwaombea wafu, ibada za sanamu, unywaji wa pombe nk ambayo kwenye vitabu vilivyokubaliwa na wengine vile 66 haviyakubali ndiyo utaona biblia yao ina vitabu kama wamakabayo, sira nk
Sira ni Apocrypha book, hujui unachokiandika.
 
Hii hapa.
Roman Catholic imeanza Karne ya kwanza na Kiongozi wa kanisa akiwa Mt Petro (Mathayo 16:18). Anahesabiwa kama first pope

Kulikuwa hakuna dhehebu jingine hadi mwaka 1054 wakati the Great schism ambapo kanisa la Mashariki (Orthodox) lilijitenga kutoka kwenye Ukatoliki. Catholic ikabakia Vatican na Orthodox ikawa na makao yake makuu Constatinople (Istanbul ya sasa)

Then mwaka 1521 Martin Luther alijitenga na Ukatoliki.

Anglican ilitokea mwaka 1575 baada ya Mfalme Henry VIII naye akaanzisha Anglican church

Hellen White mwaka 1844 naye akaanzisha SDA

Nao mapentekoste wakatokea kipindi cha great depression mwanzoni mwa karne ya 19

Sasa na wewe nitajie kidhehebu chako ni kipi! Kama siyo nyie mnasali kwa MWAMPOSA
Wale kina Mwamposa Yale siyo Makanisa (Churches) bali ni huduma (Ministries).
 
Sasa kama makanisa mengine yamekua formed miaka zaidi ya elfu baada ya ukatoliki nani aliyejitenga hapo
Sio kweli kuwa yote yalijitenga na ukatoliki
Mitume na wafuasi wao wallisambaa kote ulimwenguni hawakwenda Roma Tu

Na ni upotofu kusema kanisa la kwanza likianzia Roma na mwanzilishi wa kanisa ni binadamu Petro.Hiyo kufuru .Kanisa la Kikristo mwanzilishi ni Yesu Kristo mwenyewe ma ndio maana tunaitwa Wakristo sio Wapetro

Kanisa la Yesu Kristo likianxishwa na Kristo mwenye Israel na lilianza kule Yesu akiwa na wanafunzi wake wakisali pamoja na hata alipoondoka duniani makanisa ya Wakristo yalikuwrlepo walikuwa wakisali nyumba kwa nyumba

Baadaye makanisa hayo yakisambaa sehemu nyingi mgano Nyaraka za Paulo zinaandikwa kwa makanisa mbalimbali yaliko nchi tofauti tofauti mfano waraka kwa kanisa lililoko Rumi,waraka kwa kanisa la Korintho ,kwa kanisa la waebrania nk hivyo makanisa yalikuwapo kabla hata hilo Roman katholi na Yalianzishwa na mitume tofauti tofauti na wafuasi waliosambaa kutokea ISRAEL hata kitabu cha ufunuo tunaona malaika akiyaandika nyaraka makanisa tofauti tofauti mengi kama Kanisa la Pergamo nk waweza soma kuanzia ufunuo sura ya pili nk makanisa organised kabisa yalikuwepo ambayo yalikuwa na Maaskofu,mitume,walimu,wainjilisti na wachungaji Maaskofu wala hawakuanzia Roma wamo ndani ya agano jipya muda mrefu kabla hao Maaskofu wa Roma hawajaanza kuwepo

Watu kusali kama kanisa wakikusanyika wakiwa na uongozi kabisa ilianza Israel kukiwa na hadi wazee wa kanisa na wa kufanya huduma nyingine za kijamii kama alizokuwa akifanya Stephano

Roman Catholic ni tawi tu la dini ya Kikristo kama yalivyo matawi mengine lenye imani zake tofauti na matawi mengine kama na yenyewe yalivyo tofauti na kanisa la Roman Catholic

Wanahistoria baadhi wana tatizo huchanganya historia ya Kanisa katoliki la Roma na matawi yake na Historia ya Ukristo.Historia ya Ukristo iko tofauti na historia ya kanisa la Roman Catholic. Historia ya Ukristo inaanzia Israeli alipozaliwa Yesu mkuu wa Kanisa wakati Historia ya Kanisa la Roman Catholic inasnzia Roma Italia.Ukianxia kuongelea Ukristo unaanzia Israel na jinsi ulivyosambaa nchi mbalimbali kupitia mitume mbalimbali ikiwemo Roma na jinsi uliivyosambaa kutoka hizo nchi.mbalimbali sio moja Roma tu na kwenda kwingine sehemu mbalimbali
Historia ya uongo ile ya kusema ukristo ukienda Roma ndio.ukaanzia pale ndio ukaanza kusambaa dumiani kutokea Roma ni historia ya uongo uliokubuhu .Dini ya Roman Katoliki ndio ikisnzia Roma na kuanza kusambaa sehemu mbalimbali duniani kuanzisha matawi ya dini ya Roman Katoliki
 
Unaelewa unachokiandika
Hujui ata roman ilianza 300bk
Yan unataka useme petro alikuwa papa
Wapi io imeandikwa
Petro hajawah kukanyaga vatikan yenu maisha yake yote
Na asingeweza kushiriki uchafu wa ibada zenu za kipagani

Andiko ilo halijasema alikuwa padri ila mm ntakuonyesha andiko linalosema petro hakuwa na hayo madhehebu yenu wala.mtume wowote

Kumbuka kanisa na dhehebi ni tofaut
Kanisa linafata maandiko tuu

Dhehebu halijali atakama si maandiko ila walikaa wakapitisha kwao ni safi

Kanisa la kwanza lilianza jerusalem sio vatikan
Ila dhehebu la kwanza ndo lilianza uko kwenye mji wa shetani vatican

Chochote unachokisema dhibitisha na maandiko
Ukiongeza kitu chochote ama ukapunguza kwenye maandiko ukafanya biblia iseme kitu ambacho hakikusema maandiko yansema
Utaongezewa mapigo yale ya ufunuo
Na ukipunguza utaondolewa sehem yako mbingun
Kanisa la kwanza lililoanzishwa na Mtume Petro ni Roman Catholic, period

Hadi 2054 kabla ya the Great schism kulikuwa kanisa moja, je ni lipi hilo? Mbona majibu yako wazi

Niambie kidhehebu chako kilianza lini ? Siyo unakomaa kubishia Ukatoliki kwa chuki zako
 
Back
Top Bottom