Suala la kuwa "single mother" au kutokuwa na "BIKRA" ni suala ambalo limeshika mijadala mingi kwenye jamii kwa sasa!!
Lakini naona wengi wao tunazungumzia zaidi matokeo lakini hautangalii chanzo zaidi.....kwanini tumefika hapa... kwanini tumekuwa na wimbi kubwa la kupotea kwa "BIKRA" na ongezeko kubwa la wamama wanaoitwa "Single mother"
Mkuu walau wewe umenielewa
Nimefurahi sana kupata comment kama hii tatizo liko hapo wanalaumu mtoto wakike wanambebesha mzigo mkubwa huku wakimsahau mwanaume ambae ndio chanzo
Inafahamika ya kuwa hizo "BIKRA" na "single mother" havitokei pasi na kuhusika kwa mwanaume kwa kuwa ukamilifu wake unamhitaji mwanaume iwe moja kwa moja au kwa njia za mkato!!
Wanaume wanaongea like wao hawahusiki nikisoma comment nasikitika mpaka najiuliza imekuaje tuna jamii kama hii?
Sidhani kama bikra ya mwanamke huwa inatoka kwa kujiingiza vidole yeye mwenyewe au mwanamke anaweza kubeba mimba kwa kujiingiza vidole yeye mwenyewe yote hayo yanaonyesha jinsi gani mwanamume anashiriki kikamilifu kwenye kusababisha hiki kinacholalamikiwa kwa sasa kwenye jamii.......
Mwanaume anashiriki kikamilifu kabisa ila wanaume wa hapa wanasema et hajamlazimisha binti kukubali yaan yeye anatongoza ili akataliwe ona akili zao
Kwa tafsiri nyingine ni kwamba ingekuwa wanaume wangeamua kutofanya fanya mapenzi au ngono mpaka waoe automatically kusingekuwa na mwanamke asiyekuwa kuwa na bikra.....ingekuwa wanaume tungeamua kuishi na kushikamana na wanawake tuliowazalisha ni dhahiri kuwa kusingekuwa na single mother kwa kuwa matokeo ya haya mambo wanaume tunashiriki moja kwa moja kwa kuwa kutokea kwake kinahitaji uwepo au ushiriki wa jinsia mbili!!
Hili ndio mwarobaini ila hawa wanaume mafisi hawataki kulisikia
Huku wao wakidai bikra
Wanasema mwenye mamlaka ya kulinda bikra ni mwanamke kuna muda nikisoma comment najiuliza hivi mtu huyu ana watoto kweli?
Swali lang linakuja kwanini jamii haioni huu uovu wa wanaume wa kulala na wanawake ambao hawajawaoa au kuwapa mimba holela wanawake na kuwaacha kwanini lawama zinapelekwa kwa wahanga pekee!!?
Ni mfumo dume
Karne hii mwanaume kua na mfumo dume ni swala la hovyo hovyo kabisa
mufumo dume hufanywa na wanaume waoga wasiojiamini
Wanaamua kujilinda kwa kugeuka madikteta
Kama vijana wa kiume wangekuwa wameyashinda matamanio yao mpaka watakapooa maana hakuna binti ambaye angeharibikiwa vivo hivyo kwa kuwapa mimba maana hayo matendo yanafuatana kwani mimba ni matokeo ya ngono kitendo kinapelekea mwanamke kupoteza usichana wake!!!!
Vijana wakiume ndio wanatongoza hawa ndio wa kukazaniwa wao ndio wana anzisha safari ya uharibifu kuwarubuni mabinti wadogo
Wanaacwa na kusifiwa ni vidume
Huku lawama akibebeshwa mwanamke ajabu sana
Nadhani ifike wakati hili jambo tuliangalie kwa mapana na marefu zaidi kuliko kuyaangalia matokeo peke yake na kuwalaumu wahanga tu!!
Naunga mkono hoja mkuu
Sio wote waliokutwa na masahibu haya ni waovu na viruka njia wengine ni wahanga wa wanaume mabazazi , matapeli na walaghai.... unaweza usinielewe kama huna mtoto wa kike aliyevunja ungo na kuingia katika usichana!!!
TUJITAFAKARI
Hata kama hawana watoto waangalie kwenye jamii
mf:.muda uliopita nimeona IG huko arusha kuna baba wa kambo kamuingilia mtoto wa mwaka 1 na miezi
Mama alienda saluni tena mtoto wa kiume
Je huyo mtoto angewezaje kukataa ?
Jamii yetu bado sana
Mfumo dume u selfish ndio tunauweza