Bikra ya Mwanamke: Kwanini Lawama Zinaishia Kwa Mwanamke Pekee?

Bikra ya Mwanamke: Kwanini Lawama Zinaishia Kwa Mwanamke Pekee?

Mtoto wa wa kike wa miaka 11 12 13 14 15 16 17 una mrubuni huku ukitaka akukatae
Kwanini usitafute mabinti wa miaka 18 + hivi hapa unatetea nini?

mtoto wa kiume ni ufahari kutoa bikra kwa binti mdogo au kwa mke wake?

Mtoto analindwa na jamii nzima mkiwemo nyie wanaume kwanini mnajitoa na kusiliba tamaa zenu?

Wanaanza ngono mapema na akina nani?

Kidume sio?
Kwanini hammshauri huyo kidume kutofanya ngono na watoto wakike katika umri mdogo

jukumu hilo mnataka liwe la mtoto wa kike ?
wanaume wa ki africa mmerogwa na nani?

Sasa kwanini msilaumu hao waliozitoa kwa makundi huku nyie mkibaki kutamani tu

Hamuoni adui wenu ni mwanaume mwenzenu?
Mkuu kuna namna unataka jamii ibadili mindset au niaje ila jua kua mwanaume na mwanamke ni tofauti na wanatofautiana katika aspects nyingi mno.

Hilo la bikra, mtolewaji (girl) kwake ina thamani kubwa kuliko kwa mtoaji.
Mtoaji hatahesabiwa kazitoa ngapi ila mtolewaji asipokua nayo itafahamika kua alishashenyentwa bila kujali alifanya na nani, wakati gani na alifanya na mwanaume wa umri gani nk.

Mwanaume hana hizo limits, anaweza lala na wanawake 1000 ila ikifika zamu yako na usiwe na means yoyote ya kuprove jamaa kalala na wanawake wangapi , na anaweza akakwambia hajawahi ukamuamini.
Kwa mwanamke ni bikra tu, asipokua nayo ni wazi kuna jamaa alishachovya.
 
Nature ipo na linapokuja suala la mahusiano itamuhukumu mwanaume kwa vigezo vya uchumi na uthabiti wa maisha yake, itamuhukumu mwanamke kwa vigezo vya umri na alivyojitunza. Sasa kama umeanzisha uzi ili upewe majibu yanayokufurahisha, then keep staying in your delusional comfort zone
Jibu kuntu hili.

Mwanamke asie bikra ni moja kwa moja amepigwa miti hata akiwa na tabia nzuri, mwema, mnyenyekevu ila hawezi mzidi yule alie bikra.
 
Mkuu kuna namna unataka jamii ibadili mindset au niaje ila jua kua mwanaume na mwanamke ni tofauti na wanatofautiana katika aspects nyingi mno.

Hilo la bikra, mtolewaji (girl) kwake ina thamani kubwa kuliko kwa mtoaji.
Mtoaji hatahesabiwa kazitoa ngapi ila mtolewaji asipokua nayo itafahamika kua alishashenyentwa bila kujali alifanya na nani, wakati gani na alifanya na mwanaume wa umri gani nk.

Mwanaume hana hizo limits, anaweza lala na wanawake 1000 ila ikifika zamu yako na usiwe na means yoyote ya kuprove jamaa kalala na wanawake wangapi , na anaweza akakwambia hajawahi ukamuamini.
Kwa mwanamke ni bikra tu, asipokua nayo ni wazi kuna jamaa alishachovya.
Upo sahihi chief
 
WANAUME, NAWAITA NJOOENI KWENYE JAMVI

ANGALIZO: Hapa ukija, njoo na hoja, usije na hisia zako

UTANGULIZI :Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wanaume wakisema mwanamke asiye na bikra hastahili kuolewa hastahili kutolewa mahari, abebwe mzobe mzobe mpaka ndoani

Ila nina swali moja kwa hawa wanaume wenye mtazamo huu: Kwani nani anayeondoa bikra ya mwanamke?

Si mwanaume naye anashiriki katika tendo hilo?

Sasa kwanini baadhi yenu mna nguvu nyingi za kuwananga wanawake wasio na bikra, lakini hamna nguvu hizo hizo za kuzungumzia wajibu wa wanaume wanaowashawishi na kuwatumia wasichana wadogo kingono?

Nasema hivyo kwa sababu kuna wasichana wanaoingia kwenye mahusiano ya kingono wakiwa bado wadogo, hawajakomaa vya kutosha kiakili na kihisia
Baadhi yao hudanganywa, hushawishiwa kwa ahadi mbalimbali au hutumiwa na watu wazima wanaotambua vizuri wanachokifanya

Mwisho hujikuta wamepoteza usichana wao

Cha kushangaza ni kwamba, mwanaume anaweza kushiriki katika mazingira yaliyosababisha mwanamke kupoteza bikra halafu baadaye akageuka na kumdharau mwanamke huyo kwa sababu hiyohiyo

Yaani wewe mwanaume ambae hukujitunza ambae unajua kila sample ya kei za wanawake
Unapata wapi nguvu ya kusema nataka mwanamke bikra?

Kwa usafi upi hasa ulionao?
Hao uliwachezea unataka nani ale makombo yako wewe unatafuta fresh?

Nimeingia mtandaoni kutafuta hali ya ukatili kingono kwa wasichani wenye umri mdogo

Kwa mujibu wa utafiti wa kitaifa wa Tanzania wa mwaka 2024 kuhusu ukatili dhidi ya watoto na vijana (VACS) asilimia 8.4 ya wanawake waliohojiwa wenye umri wa miaka 18–24 waliripoti kufanyiwa ukatili wa kingono kabla ya kufikisha miaka 18

Huu ni utafiti tu ambao wanawake wengine huogopa kufunguka
Lakini naamini wapo wengi zaidi na tunaona kesi nyingi hata hazipelekwi kwenye madawati huishia kumalizwa kwa ngazi ya familia

Wote tunajua haya mambo yapo tena hufanywa na watu wakaribu sana kwenye familia wale wa kuaminiwa na sio watu tu ni Wanaume wenzenu au hata nyinyi wenyewe 📌


Naomba nieleweke sio kwamba wanaume wote wako hivi. La hasha!

Kuna wanaume wanaoheshimu wanawake, wanaolinda watoto na wanaopinga kabisa vitendo hivi


Hoja yangu ni kwa wale wanaume wanaotaka mwanamke awe bikra wakati wa ndoa, lakini hawataki kuzungumzia wajibu wa mwanaume katika kulinda heshima na usalama wa wasichana

Hakuna bikra itatoka bila mwanaume au tuseme baiskeli?

Wanaume kwanini msianze kuhamasishana wenyewe kwa wenyewe kufunga zipu zenu na kuacha kurubuni wasichana kwenye umri mdogo?

Hivi hamuoni kua nyie ndio chanzo kikubwa?

Mwisho; Kama bikra ni kigezo cha thamani ya mwanamke, je thamani ya mwanaume anayeshiriki katika tendo hilo inapimwaje?

Kama mwanamke anatakiwa kuwajibika kwa historia yake ya kimapenzi, je, mwanaume naye hapaswi kuwajibika kwa matendo yake?

Na kama kweli tunataka kupunguza tatizo hili, kwanini tusianze kwa kuhamasisha heshima, uwajibikaji, kutowadanganya wasichana na kutowatumia watoto kingono?

MWISHO WA SIKU, SI UNAWEZA KUMDHARAU MTU KWA JAMBO AMBALO WEWE MWENYEWE ULICHANGIA KULITOKEA?

ShesRise_1 ✋️
Wajibu wa mwanaume ni mmoja tu, akikutoa bikra akuoe.
 
Mwizi ale njama na mlinzi, afanikiwe kuiba mali, kisha aanze kumbananga yule mlinzi hafai.

Utamshangaa mlinzi au mwizi?
 
uzi mrefu mno unachosha kusoma ila nilichokielewa ni lawama za bikra tu
 
WANAUME, NAWAITA NJOOENI KWENYE JAMVI

ANGALIZO: Hapa ukija, njoo na hoja, usije na hisia zako

UTANGULIZI :Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wanaume wakisema mwanamke asiye na bikra hastahili kuolewa hastahili kutolewa mahari, abebwe mzobe mzobe mpaka ndoani
Nikweli, hastahili kuolewa

Ila nina swali moja kwa hawa wanaume wenye mtazamo huu: Kwani nani anayeondoa bikra ya mwanamke?

Si mwanaume naye anashiriki katika tendo hilo?

Sasa kwanini baadhi yenu mna nguvu nyingi za kuwananga wanawake wasio na bikra, lakini hamna nguvu hizo hizo za kuzungumzia wajibu wa wanaume wanaowashawishi na kuwatumia wasichana wadogo kingono?
Bikra ni ya mwanamke yeye ndio anazaliwa na bikra wla sio mwanaume na yeye ndie ana mamlaka na uamzi 100% wakuamua itoke au isitoke na nani aitoe.

Mwanaume hausiki kwenye ishu hii, Mwanaume anamtongoza mwanamke iwe kumuoa au kumchezea yeye atasimama na lengo lake na wala hakufungi kamba na kuitoa hio bikra.

Mimi nakutongoza na kukucheba wala sijari wewe kama nitakutoa bikra hilo sio jukumu langu kabisa jukumu langu mimi kama mwanaume kwenye sctor ya mahusiano ni kuimarisha uchumi wangu basi.

Ukinilaumu mimi kwa bikara ambayo ni yako wewe ni matumizi mabaya ya akili na wala mimi hainiounguzii chochote ila kwako still bikra huna na utakataliwa na wanaume timamamu.
Nasema hivyo kwa sababu kuna wasichana wanaoingia kwenye mahusiano ya kingono wakiwa bado wadogo, hawajakomaa vya kutosha kiakili na kihisia
Baadhi yao hudanganywa, hushawishiwa kwa ahadi mbalimbali au hutumiwa na watu wazima wanaotambua vizuri wanachokifanya

Mwisho hujikuta wamepoteza usichana wao
Ukiwa unatoa hoja kama hii usitengeneze DEFENSIVE TRAP, weka umri huyo msichana mdogo unayemzunguzia ni wa umri gani kama ni chini ya 18 upo sahihi na nitaungana upande wako kwenye hii mada.

Ila kama juu ya 18 yeye ni mtu mzima hata atongozwe na mwanaume wa miaka 70.
Cha kushangaza ni kwamba, mwanaume anaweza kushiriki katika mazingira yaliyosababisha mwanamke kupoteza bikra halafu baadaye akageuka na kumdharau mwanamke huyo kwa sababu hiyohiyo

Yaani wewe mwanaume ambae hukujitunza ambae unajua kila sample ya kei za wanawake
Unapata wapi nguvu ya kusema nataka mwanamke bikra?
Hakuna concept au msamiati wa kujitunza kwa mwanaume, yaani hakuna neno kujitunza hilo ni kwa mwanaume tu ukifosi kuleta 50/50 kwenye suala la kibaolojia biana ya Me na Ke utaumia sana hakuna hio 50/50 Mwanaume amependelewa sana kwenye upande wa kibaolojia kuliko mwanake.

Wajibu wa kujitunza ni wako wewe mwanamke kwani wewe hujui kuwa umeumbwa na bikra, hujui kuwa maumbile yako yatatanuka, hujui kuwa utaitwa malaya, hujui kuwa utakuwa single mother....Kuna matokeo mengi mabaya kwa mwanamke kama hajajutunza ila sio kwa mwanamume.

So usilazimishe 50/50 au kulaumu wanaume mlaumu aliyeumba hivyo basi.
Kwa usafi upi hasa ulionao?
Hao uliwachezea unataka nani ale makombo yako wewe unatafuta fresh?
Wamechezewa wao ni midoli talking as if mwanaume anakuja anatomasa anachoneka. Huna akili, huna maamuzi, huna ubongo.

Kuchezewa hilo ni tatizo lako sio la mwanaume, mwanaume ana matatizo yake ya kiuchumi sio umuongezee matatizo.
Nimeingia mtandaoni kutafuta hali ya ukatili kingono kwa wasichani wenye umri mdogo

Kwa mujibu wa utafiti wa kitaifa wa Tanzania wa mwaka 2024 kuhusu ukatili dhidi ya watoto na vijana (VACS) asilimia 8.4 ya wanawake waliohojiwa wenye umri wa miaka 18–24 waliripoti kufanyiwa ukatili wa kingono kabla ya kufikisha miaka 18

Huu ni utafiti tu ambao wanawake wengine huogopa kufunguka
Lakini naamini wapo wengi zaidi na tunaona kesi nyingi hata hazipelekwi kwenye madawati huishia kumalizwa kwa ngazi ya familia
Akiyetolewa bikra chini ya 18 hapa ndio mwanaume ana makosa nakubali.
Wote tunajua haya mambo yapo tena hufanywa na watu wakaribu sana kwenye familia wale wa kuaminiwa na sio watu tu ni Wanaume wenzenu au hata nyinyi wenyewe 📌


Naomba nieleweke sio kwamba wanaume wote wako hivi. La hasha!

Kuna wanaume wanaoheshimu wanawake, wanaolinda watoto na wanaopinga kabisa vitendo hivi


Hoja yangu ni kwa wale wanaume wanaotaka mwanamke awe bikra wakati wa ndoa, lakini hawataki kuzungumzia wajibu wa mwanaume katika kulinda heshima na usalama wa wasichana

Hakuna bikra itatoka bila mwanaume au tuseme baiskeli?

Wanaume kwanini msianze kuhamasishana wenyewe kwa wenyewe kufunga zipu zenu na kuacha kurubuni wasichana kwenye umri mdogo?

Hivi hamuoni kua nyie ndio chanzo kikubwa?
Madam, Hii ni Sector ya mahusino nikwambie hiki uweke akilini.

Kwenye mahusino mwanume ni ECONOMIC BEING n mwanamke ni BOLOGICAL BEING kwamaana mwanaume anathaminiwa kwa uchumi ndio maana utasikia kauli tafuta pesa, mwanaume suluari, masikini, siolewi na mwanaume asiye na pesa nk

Ila mwanamke anathaminiwa kwa BIOLOJIA yake ndio maana utasikia Hana bikra, linliowaya, single mother, maziwa kandambili nk.

Hivyo kila mtu anawajibika kwenye uoande wake mwanamke jitunze kibaojia mwanaume jiimalishe kiuchumi.

Sasa ukisema kwmba wanaume waanze kujipa majuku ya kurinda na kusimamia wanaume kwenye upande wao wa kulinda bikra ni kufanya wanaume wache uoande wao waingilie uoande mwengine je wanawake nao kwanini hawajadiri kuhusu kuimarisha uchumi za wanaume hili wasikataliwe kiwa wnaume masikini.

So acvoding to you wanawake mwanaume kuwa masikini na wanawake kimkataa ni tatizo la mwanaume 100% ila mwanamke kuwa single mother na kukataliwa na wanaume ni letu wote...Huu ubinafsi ni wa kiwango gani.
Mwisho; Kama bikra ni kigezo cha thamani ya mwanamke, je thamani ya mwanaume anayeshiriki katika tendo hilo inapimwaje?
Thamani ya mwanume ni uchumi wake
Kama mwanamke anatakiwa kuwajibika kwa historia yake ya kimapenzi, je, mwanaume naye hapaswi kuwajibika kwa matendo yake?
Hapswi kuwajibika, mwanaume anawajibika kwenye uchumi wake walasio historia yake.

Mwanaume anapimwa kwa future yake, mwanamke anapimwa ka past yake.
Na kama kweli tunataka kupunguza tatizo hili, kwanini tusianze kwa kuhamasisha heshima, uwajibikaji, kutowadanganya wasichana na kutowatumia watoto kingono?
Hili sio tatizo la jamii, na wla sio tatizo ata first ila unalazimisha kuwa tatizo na tukisema ni tatizo basi ni lwa wanawake sio jamii.
MWISHO WA SIKU, SI UNAWEZA KUMDHARAU MTU KWA JAMBO AMBALO WEWE MWENYEWE ULICHANGIA KULITOKEA?

ShesRise_1 ✋️

BITTOMLINE
"Kwenye sector ya mahusiano Mmwanaume ni Economic being na mwanmke ni Biolojical being kila upande usiamame na majukumu yake usitokee upande mmoja ukataka uonde mwengine ungilie kusaidia upande mwengine matatizo yao na mala nyingi upande huu hua ni jinsia KE unaoende ku play Victim"

Bil kusahau Mwnaume
*Usioe single mothe
*usioe maziwa yamelala
*usioe zaidi ya miaka 27
*usioe asiyejitunz mwili kitambi
 
Hapa hakuna wakutipiwa lawama
Kinachoshangaza ni wanaume kujitoa kwenye hili swala kama vile vile hawahusiki
Mimi nahusika endpo na mimi nitakuwa nina bikra kama mimi sina bikra wewe ndio mwenye bikra unanihusishaje kwenye tatizo la bikra kutoka.

Wewe unajua bikara ukiwa huna ni tatizo then unaenda kuitoa wakati huo unayeshirikiananae yeye wla hapati hilo tatizo la hio bikra kutoa then unataka mkae wote mlie na kujadiri pamoja kulinda hio bikra ...What thinking is this.

Yaani kama kusema waziri wa maafa wa nchi X akajadiri kuzuia maafa ya nchi Y wakati hayo maafa hayamuhusu.
 
Kwanini utongoze huku ukijua unaemtongoza huna nia ya kumuoa

Hii ni akili gani mkuu?
Kwanini wewe mwanmke usikatae kutoa mpaka uolewe, nani hapo hana akili mimi nisiye athirika au wewe unayeathirika??...MOSI.

PILI...hakuna mwanaume anayetongoza kwaajiri ya kichezea ila matendo na tabia zako wewe mwanamke ndio mwanaume atasema huyu niponae ila hakuna mke napiga tu.
 
Duu ila wewe dada ngoja nikujibu au nijibie kama unavyotaka tuone nani mjinga, Maana haiwezekani shida yako alafu uniulize mimi maswali as if mimi ndio ninmtapata shida
Naanza na wewe kwanini utongoze huku ukijua huna nia ya kumuoa jibu swali acha kurukaruka mkuu
Namtongoza hili nimchezee that
Jibu swali langu hapo juu kwanza
Lishajibiwa
Kwanini wewe usiende kwao kama kweli unampenda
Nyie hua mnarubuni mpaka watoto wa shule ya msingi
Kwahiyo unataka aende kwako kusema kapata mchumba?
Siendi kwao kwasababu namchezea
Jibu maswali yangu kwanza
 
Sea Beast
Ume ni quote zaidi karibu mara 5
Sijui hata ni kujibu quote gani niache ipi

Labda niseme hivi asante kwa maoni yako na karibu tena 🙏🙏
 
Back
Top Bottom