WANAUME, NAWAITA NJOOENI KWENYE JAMVI
ANGALIZO: Hapa ukija, njoo na hoja, usije na hisia zako
UTANGULIZI :Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wanaume wakisema mwanamke asiye na bikra hastahili kuolewa hastahili kutolewa mahari, abebwe mzobe mzobe mpaka ndoani
Ila nina swali moja kwa hawa wanaume wenye mtazamo huu: Kwani nani anayeondoa bikra ya mwanamke?
Si mwanaume naye anashiriki katika tendo hilo?
Sasa kwanini baadhi yenu mna nguvu nyingi za kuwananga wanawake wasio na bikra, lakini hamna nguvu hizo hizo za kuzungumzia wajibu wa wanaume wanaowashawishi na kuwatumia wasichana wadogo kingono?
Nasema hivyo kwa sababu kuna wasichana wanaoingia kwenye mahusiano ya kingono wakiwa bado wadogo, hawajakomaa vya kutosha kiakili na kihisia
Baadhi yao hudanganywa, hushawishiwa kwa ahadi mbalimbali au hutumiwa na watu wazima wanaotambua vizuri wanachokifanya
Mwisho hujikuta wamepoteza usichana wao
Cha kushangaza ni kwamba, mwanaume anaweza kushiriki katika mazingira yaliyosababisha mwanamke kupoteza bikra halafu baadaye akageuka na kumdharau mwanamke huyo kwa sababu hiyohiyo
Yaani wewe mwanaume ambae hukujitunza ambae unajua kila sample ya kei za wanawake
Unapata wapi nguvu ya kusema nataka mwanamke bikra?
Kwa usafi upi hasa ulionao?
Hao uliwachezea unataka nani ale makombo yako wewe unatafuta fresh?
Nimeingia mtandaoni kutafuta hali ya ukatili kingono kwa wasichani wenye umri mdogo
Kwa mujibu wa utafiti wa kitaifa wa Tanzania wa mwaka 2024 kuhusu ukatili dhidi ya watoto na vijana (VACS) asilimia 8.4 ya wanawake waliohojiwa wenye umri wa miaka 18–24 waliripoti kufanyiwa ukatili wa kingono kabla ya kufikisha miaka 18
Huu ni utafiti tu ambao wanawake wengine huogopa kufunguka
Lakini naamini wapo wengi zaidi na tunaona kesi nyingi hata hazipelekwi kwenye madawati huishia kumalizwa kwa ngazi ya familia
Wote tunajua haya mambo yapo tena hufanywa na watu wakaribu sana kwenye familia wale wa kuaminiwa na sio watu tu ni Wanaume wenzenu au hata nyinyi wenyewe 📌
Naomba nieleweke sio kwamba wanaume wote wako hivi. La hasha!
Kuna wanaume wanaoheshimu wanawake, wanaolinda watoto na wanaopinga kabisa vitendo hivi
Hoja yangu ni kwa wale wanaume wanaotaka mwanamke awe bikra wakati wa ndoa, lakini hawataki kuzungumzia wajibu wa mwanaume katika kulinda heshima na usalama wa wasichana
Hakuna bikra itatoka bila mwanaume au tuseme baiskeli?
Wanaume kwanini msianze kuhamasishana wenyewe kwa wenyewe kufunga zipu zenu na kuacha kurubuni wasichana kwenye umri mdogo?
Hivi hamuoni kua nyie ndio chanzo kikubwa?
Mwisho; Kama bikra ni kigezo cha thamani ya mwanamke, je thamani ya mwanaume anayeshiriki katika tendo hilo inapimwaje?
Kama mwanamke anatakiwa kuwajibika kwa historia yake ya kimapenzi, je, mwanaume naye hapaswi kuwajibika kwa matendo yake?
Na kama kweli tunataka kupunguza tatizo hili, kwanini tusianze kwa kuhamasisha heshima, uwajibikaji, kutowadanganya wasichana na kutowatumia watoto kingono?
Nina mengi ya kuandika hapa lakini muda hautoshi.
Kulinda bikra ya mwanamke ni jukumu la jamii nzima hasa hasa familia yake.
Ukisoma biblia watoto wa Yakobo walipoona dada Yao ametolewa bikra bila ya kuoleewa waliua ukoo mzima wa ile jamii iliyomfanyia vibaya dada Yao.
FUNZO: Baada ya kumfanya vibaya dada mtu unaona ile familia walitaka kumuoa yule Binti lakini familia ya Yakobo ndio waliona sio vyema wakaamua kuua ukoo mzima. Lakini funzo tunalopata ni kwamba ile jamii walikua na uungwana japo hawakupita njia sahihi.
Turudi kwenye jamii zetu za Afrika na hasa Tanzania. Kuna jamii zinataratibu za ovyo sana kuliko unavyoweza kufikiri au kutafakari au kuwatetea kama ulivyoainisha katika huu Uzi.
Binafsi niliishi Sumbawanga,Rukwa. Siku Moja nipo na dogo ametoka kumaliza darasa la saba kuna mpumbavu mtu mzima akaanza kumuita dogo. Yaani ilikua ni barabarani na watu wanapita nilimwambia kwa herufi mkubwa "NITAKUCHINJA MCHANA KWEUPE"
Nilipata funzo kwamba Kuna jamii zimeshaharibika na ukizichekea nawewe ni lazima uharibikiwe.
Moja ya jamii ilishaharibika ni hao ndugu wa Sumbawanga wao mtoto wa miaka 14,15,16 kuzalishwa ni kitu Cha kawaida kwao.
Kujibu swali lako ni kwamba haya maswala hayahusu wanaume tuu bali ni jamii nzima. Hivyo kama lawama inatakiwa kutupiwa jamii nzima.
MWISHO WA SIKU, SI UNAWEZA KUMDHARAU MTU KWA JAMBO AMBALO WEWE MWENYEWE ULICHANGIA KULITOKEA?
ShesRise_1 ✋️
Hapa mwisho nakupinga kwa herufi kubwa. Kwasababu hizi,
Mosi; Jukumu la kulinda bikra linamuhusu sana yule aliyeibeba hiyo bikra unless otherwise huyo mwanamke anamatatizo ya akili ndio hapo jamii itahusika kwa asilimia mia moja kuilinda hiyo bikra yake au papuchi yake kwasababu wasipofanya hivyo watajikuta wanalea mtoto mwingine. Hii inatokana na wanaume wenye upungufu wa akili. Hawa ni kazi sana kuwacontrol na pia hawajielewi na njia nyepesi kwao ilikua wafundishwe kupiga punyeto tuu.
Pili; Hupaswi kumlaumu mtu anaetaka kuoa Binti bikra eti kwasababu yeye alishahusika kwa namna Moja au nyingine kuzitoa hizo bikra. Hapa ni lazima utambue kwamba hiyo bikra ndio namna pekee ya binti kumuaminisha mwanaume kwamba yeye anajitambua na anafaa kuolewa.
Tatu: Kuna wanawake ni WAPUMBAVU, Sasa hawa ni chakula Cha wageni hivyo mwanaume kamili hafai kuoa mwanamke mpumbavu ambaye ni chakula Cha wageni/wapita njia. Ni bikra pekee inayotofautisha kati ya mwanamke anayejitambua na yule ambaye ni chakula Cha wageni.
Naomba kueleweka hapa wanawake WAPUMBAVU ni jamii ya wale wanawake ambao akichukizwa au kuuziwa bhasi anatafuta mtu wa kumuweka dudu, Hawa nao hutafuta kuolewa pia.
Nne: Wanawake wenye tamaa, Hawa wanawake hata ukiwalinda kwa mtutu ni lazima tuu atapoteza hiyo bikra. Sasa huyu nae unataka lawama zake watu wabebe kweli????
Yapo mengi sana lakini haya ni baadhi ya machache tuu.
Nafikiri badala ya kutupiana lawama inatikiwa tujifunze kutoka kwenye jamii zilizofanikiwa katika hili jambo. Hasa hasa tujifunze kwa wahindi, waarabu na wasukuma.