Bila dhuluma wala kukimbiza wafanyabiashara, Rais Samia aweka rekodi ukusanyaji mapato

Nani analia na analia kwa lipi Mkuu,

Acheni kujipa mamlaka fake ya kuwasemea wananchi,

Nitajie kundi lolote linalo lia nani ntakambia kitu,


#KAZI IENDELEE KWA KASI & WELEDI ZAIDI
Makampuni ya simu yanalia mapato yameshuka kwa kiwango cha kutisha,mawakala wanalia biashara yao imeshuka,watanzania ni watu wakimya sina,ila wanaugulia moyoni maumivu haya
 
Unataka kusema ndani ya miezi hii michache wafanya biashara waliokimbia wameweza kurudi na kufanya biashara na kusimama imara hadi kufikia kiwango cha kulipa kodi kikamilifu!? Kuwa na akili basi ata kidogo.
Hawa timu Msoga unafikiri wanaakili basi
 
Hongera kwa Serikali kufikia malengo ya Kodi kufikia 93%.

Ila utofauti upo kwenye Kodi Mpya ambazo zimeanza kutozwa awamu hii ya 6 ambazo awamu ya 5 hazikwepo;

....Tozo za miamala ya Simu
....Kodi ya Majengo kupitia LUKU

Sisi Wananchi tunahitaji Kodi zetu tuzione kwenye uboreshaji wa huduma za afya angalau vifaa tiba na Wataalamu waongezwe kwenye vituo vya afya ambavyo sasa vinafika almost 450 Nchi Nzima, uboreshaji wa huduma za Elimu, Maji, Barabara, Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano n.k

Mambo ya kutumia kodi zetu hovyo kwa kuwa na Vikao vya Chama na Serikali mara Dodoma na Dar es Salaam hatutaki. Mchague Mkoa Mmoja kufanya Shughuli za Serikali sio kila siku kulipana maPerdiems na kutumbua kodi zetu
 
Kama haya ndo.mapato kwanini vijana hawajiliwi?
Hujasikia Rais Samia alisajiri miradi mipya 93 yenye thamani ya $1.6bl kwenye Siku zake 100 zilizotoa ajira 26,000?

Hujamsikia 01|05|2021 aliachilia ajira 40,000

Hujasikia ameachilia ajira 1,000 mambo ya ndani?

Hujasikia waisraeli wanaajiri vijana elfu 70?

#KAZI IENDELEE KWA KASI & WELEDI ZAIDI
 
wamesahau Tozo ,,wamesahau kwamba kunatozo ya sh 100 kwa kila litre ya mafuta iliyoongezwa..Lakini wanasahau magufuri aliweka mfumo wa kulipia electronically ambapo sasa wanaimarisha kidogo na hera yote unaiona
Hiyo mifumo ya kielekteonic mbona ipo kila nchi mkuu. Kenya,Uganda,Rwanda,nk. Ni mipango ya serikali iliyokuwa inatekelezwa.

Ni jambo zuri kutambua mafanikio ya kiongozi. Kwenye kodi,wapinga ramri na wanga walikuwa wanasema serikali ya Samia haitaweza kukusanya kodi kwa kubembeleza walipa kodi. Sasa,kwa mafanikio haya,inaonekana dhahiri kwamba utaratibu wa raisi samia wa ukusanyaji kodi una tija. Tumpongeze kwa mafanikio haya.
 
Mkuu CCM haitegemei pesa ya Serikali,

CCM inapata ruzuku zaidi 1bl kwa mwezi toka serikalini,

Ukiona tunafanya vikao ni kwa pesa yetu kama CCM sio kama serikali,

#KAZI IENDELEE KWA KASI & WELEDI ZAIDI
 
Naugana na wewe 100%

#KAZI IENDELEE KWA KASI & WELEDI ZAIDI
 
Unataka kusema ndani ya miezi hii michache wafanya biashara waliokimbia wameweza kurudi na kufanya biashara na kusimama imara hadi kufikia kiwango cha kulipa kodi kikamilifu!? Kuwa na akili basi ata kidogo.
Wasalaam mkuu,

Wewe unataka kubishana na namba?

Biashara sio Majumba biashara ni pesa,

Kwani kutoa pesa na kuagiza konteina China na kupokea mizigo kunatumia muda kiasi gani?

Siku 100 tu duniani kote zinatoa dira na mwanga wa kiongozi,

Endelea kujifunza kuwaza kizalendo mkuu,


#KAZI IENDELEE KWA KASI & WELEDI ZAIDI
 
Mkuu CCM haitegemei pesa ya Serikali,

CCM inapata ruzuku zaidi 1bl kwa mwezi toka serikalini,

Ukiona tunafanya vikao ni kwa pesa yetu kama CCM sio kama serikali,

#KAZI IENDELEE KWA KASI & WELEDI ZAIDI
Mkuu mkiona inafaa unaweza kushauri Chama pia, kwakuwa hizo Bilioni unazosema wanapata kutoka Serikalini ni matokeo ya Kodi zetu.

Hata kama wanapokea kama sadaka ndiyo zitumike hovyo? Hivi unajua Makatibu Kata wa CCM hawana Usafiri kuwawezesha kwenda Wilayani pamoja na kufanya ufuatiliaji kwenye Mashina?

Hizo Ruzuku zinazotumika kulipana maposho ya Dodoma - DSM huoni walikuwa wanaweza kununua walau pikipiki za 2 milioni kwa kila Katibu Kata wao??
 
Humo humo kuna tozo za simu humo humo kuna tozo za Luku
Harafu unaleta unafiki


magufuli hakutoza hizo
Kikwete hakutoza hizo
Mkapa hakutoza hizo


Kimberembere kibaya Sana

Chawa kama chawa
tozo za luku ndio zipi hizo
 
Mnatukamua tozo za miamala na kodi ya majengo alafu mnajisifu.
Huo ni mtazamo mpya wa ukusanyanji wa kodi, kila mwananchi sasa anachangia pato la taifa maskini kwa tajiri, maskini sasa anaweza kusimama kifua mbele kwamba na yeye ni muhimu katika Taifa - anachangia ujenzi wa kituo cha afya, madarasa na barabara. Kodi za majengo zimekuwapo zaidi ya miaka 10, kama kuna watu wanashangaa mwaka huu- hii ni dhahiri kuwa watu wengi walikuwa wanakwepa kulipa. Hongera kwa awamu ya Sita kwa kungamua hayo.
 
Hizo posho zinaongeza mzunguko wa pesa mifukoni mwa watu, na uchumi unakua kuliko kununua pikipiki - ambayo unaendeleza zaidi uchumi wa Uchina au India ambako pikipiki imetoka. Huyo jamaa aliyepata posho - atanunua nyanya, vitunguu, unga na mchele wa hapa hapa Tanzania.
 


Huyu Mama ni moto wa kuuota kwa mbali sana,

Kazi anazozifanya zinatisha sana,

Mungu ampe mia 2 tuendelee kuvuna hekima zake,

Tunakupenda Samia, Tuko na wewe hadi uchoke kuongoza


MIMI KAMA JABALI NIMEKUBALI MAPIGO YAKO SAMIA
 
Ajira zinatangazwa , nadhani unasikia.
Sema utamaduni wa pambio siuungi mkono kwani unaweza mharibu kiongozi mzuri.
Anataka ule ujinga wa miaka 5 iliyopita uendelee, jambo dogo tu linatangazwa kama ndiyo mwisho wa dunia!! Mambo aliyoyafanya huyu mother kwa hii miezi 6 ingekuwa awamu pendwa mtaani kusingekalika kwa maandamano ya kupongeza
 
Nani analia na analia kwa lipi Mkuu,

Acheni kujipa mamlaka fake ya kuwasemea wananchi,

Nitajie kundi lolote linalo lia nani ntakambia kitu,


#KAZI IENDELEE KWA KASI & WELEDI ZAIDI
Hamna anayelia, ni ujinga na wivu tu wa hawa jamaa!! Kufail kwa serikali na Tz kwa ujumla ndiyo furaha yao!! Chuki ya ajabu kabisa hii
 
We jamaa umefungua account hii kwa ajili ya kusifia tu awamu hii! Ila mwambie huyo bibi Tozo kwamba hakubaliki kabisaaaaa mitaani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…