Bila kufanya haya, tusahau suala la kuondokana na Mgao wa Umeme

Rudia kusoma hicho chanzo linganisha cost ya hydro na compressed
 
Kwa hiyo hata HEP inahitaji eneo kubwa ndio lengo langu kukuambia hivyo zaidi ya miti milioni 2 ilikatwa
 
Rudia kusoma hicho chanzo linganisha cost ya hydro na compressed
Unajua cost huwa inapatikana vipi ? Na katika cost yao wameweka nini na nini, Na katika Bwawa waliloweka kuna kina kiasi gani na infrastructure kiasi gani ?

Haya mambo usiyachukulie juu juu tu fuatilia ni nini kimewekwa kwenye equation....; and how reliable an option is..., Hivi unajua 95% ya storage ya Energy Grid zote duniani ni Pumped Hydro ? (Au unadhani wao hawajui hayo)
 
Kwa hiyo hata HEP inahitaji eneo kubwa ndio lengo langu kukuambia hivyo zaidi ya miti milioni 2 ilikatwa
HEP hauamui tu kwamba uiweke sio kila nchi au kila sehemu ina uwezo huo.., ni bahati kuwa na vyanzo vyenye uwezo huo..., hata ukitaka vipi Jangwani huwezi kupata HEP.., Ni kama wewe upo Jangwani na kuna tende nyingi lakini unaweza upande nini kati ya zabibu na tende...
 
Ila ndugu. Pamoja na maswali yako mengi bado wengine wanafanya tena maamuzi haya yanafanywa na wenzetu wa hapa hapa nchi za kiafrika. Sie tunashindwaje? Niger tu wamefanya maamuzi juzi. Sasa kwa nini tushindwe?
 
Ila ndugu. Pamoja na maswali yako mengi bado wengine wanafanya tena maamuzi haya yanafanywa na wenzetu wa hapa hapa nchi za kiafrika. Sie tunashindwaje? Niger tu wamefanya maamuzi juzi. Sasa kwa nini tushindwe?View attachment 2827535
Unajua wewe unaweza ukawa na uwezo wa kula matunda fresh kutoka Shambani ila unashangaa kwanini usile matunda ambayo yamesindikwa kama vile anavyofanya jirani yako ambaye hana shamba..., Unajiuliza kwanini yeye anakula ya kusindika na mimi nisile (kumbe jibu huenda yeye hana shamba kama wewe)

Sasa tukirudi kwenye nchi yetu..., tunao uwezo wa kupata vyanzo lukuki vya umeme na wala vyanzo sio tatizo (from Geothermal to each and every other way).., Pia tunayo maporomoko ambayo yanaweza kutumika kwenye HEP (wengine hawana)..., sasa badala ya kusumbuka na kuweka farms za solar ambapo uzalishaji ni intermittent kwanini tusiweke au kuwapa fursa wananchi ambao kila mtu ana paa lake la nyumba akitaka aweke solar ? Utaona hapo kwamba tutakuwa tumepata hekari za kutosha ambazo hazipo centralized...; Kwa kuwa na farms na kuwapa watu ulaji wawauzie Tanesco huenda tukawa tumewazalishia watu fursa (kwa kuwauzia Tanesco Nishati at Premium Prices tena mchana hata kama mahitaji yakiwa madogo)...

Pia kutokana na kwamba sisi tuna bahati ya HEP tunaweza pia huo umeme wa jua unaozalishwa na kila mtanzania ukaweza kuwekwa kwenye grid na ukiwa excess ukatunzwa kwenye HEP kwa kurudisha maji kwenye reservours za juu kutoka chini...

Narudia tena Upatikanaji wa Nishati sio Tatizo kama kuweza kupata nishati hio wakati unaohitaji (yaani a continuous stable supply) na hilo mpaka leo ndio kikwazo cha renewable nyingi kama wind na solar; Generator na mafuta ni rahisi tu either unazima au unawasha kulingana na matumizi na ukizima sio kwamba yanaendelea kutumika yanabaki hata ukija wiki kesho unayatumia (solar umeme ulizalisha wa akiba mchana ili kutumika usiku lazima uwe na storage, which unless its HEP its costly)
 
Mkuu una maneno mengi sana ambayo mengi kwa mtazamo wangu ni fear of the unknown.

Kama hofu zako zingekuwa reality kamwe nchi zisingefanya maamuzi kwa kiwango hiki ku invest kwenye solar. Tena sio nchi tajiri tu, hadi nchi zenye uwezo wa chini yetu.

Kusema kweli ni maamuzi tu!
 
Mkuu nakwambia hata tukiwa na umeme wa Gesi wa uhakika kwa miaka 30-50 inatosha maana Yesu atakuwa amesharudi mara ya Pili na kutupeleka mbinguni/ Peponi kwenye raha tupu!!!.
Mbinguni hakuna usiku kwamba utahitaji umeme. Yesu tu ni mwanga wa kutosha.
Yohana 14:1-3 Yesu alisema anarudi haraka tumusubiri na tuwe tayari kumlaki hewani akija.
 
Cost inasemaje hapo kwenye source?
 
Umeelewa point yangu?
 
Fear of Unknown wapi mkuu wakati haya nayokupa ni kutokana na mambo yanayofanyika....

Kwanini uwe na solar farms wakati kuna smart meters ambazo zinaweza zikatumia real estate ambayo haitumiki kwa sasa na huo umeme ukatunzwa unadhani mapaa ya wananchi wote Tanzania au nusu ya wananchi ni sawa na hekari ngapi; na sababu hii ni decentralized unadhani itatumia mamilioni hayo ya dollar za subsidized money? (which is more efficient; navyosema mimi au kuwa na mahekari hapa na pale ya solar farms kwenye land ambayo ingekuwa utilized for other endeavor) ?

Kutumia solar pekee bila energy mix haiwezekani kwa sasa mpaka pale storage ya hio solar itakapokuwa at par na matumizi kwahio mpaka dakika hii solar ina mchango wake wala hakuna aliyesema isiwepo; Kwani solar sasa hivi Tanzania hazipo; Au unataka kampuni X ije ili iuzie Tanesco sijui MW 10 au 5 sijui at what price ili zitumike mchana ? au Tanesco ndio ifanye investment nyingine ya Powebanks - Si ndio yale yale na Dowans el al?

Ndio maana narudia tena mimi naongelea kitu practically na chenye manufaa ya mazingira yetu na kwa kutumia rasilimali zilizopo sasa na hio energy mix ninayoongelea mimi ni kwa kutumia kila chanzo chochote kitakachokuja kwa mtu yoyote na kuwekwa kwenye Grid so long as its cheaper kuliko Cost ambazo Tanesco anazilisha na Bwawa...,
 
Cost inasemaje hapo kwenye source?
Ngoja nikufikishe kwenye point
A; Pumped Hydro
Umeme unazalishwa kama kawaida peak time na ikifika ofpeak time yale maji ambayo yapo chini (energy yake ishatumiwa) yanatumiwa na pumps zilizopo tayari kurudisha maji juu na kwa kufanya hayo yote overall efficiency ni 80% yaani hapo energy loss is just around 20 percent.... Bwawa lipo; Pumps zipo na maji yapo; in short kila kitu tayari tunacho....

B: Compressed Air Energy Storage
Hapa nishati inatumika katika ku-compress air kwenye storage facility fulani (iwe caves au chochote kile) na ili angalau efficiency iwe nzuri iwe pressurized air mwisho wa siku inatumika kusukuma turbines) efficiency ya hii ni anywhere from 60 - 80% Sasa facility za hio air tutahifadhi wapi kwenye tanks, underground cavens au wapi ? Na hizi zitahitaji kujengwa au tayari zipo au tutafute tena pesa zetu ili tuwekeze hapa ? na kwanini tuwekeze hapa wakati pale juu panafaa na tayari papo na ni efficient ?

Now nieleweshe tena Kati ya A na B; kwa muktadha wa Tanzania ni ipi inafaa ?
 
Umeelewa point yangu?
Point yako haina mashiko kuwa na maporomoko ambayo yana energy na hio energy hauitumii ni kuwa na mtindio wa Ubongo..., wengine ambao hawana HEP sio kwamba hawataki bali sio feasible kwao kuwa nayo sababu hawana hio natural infrastructure...

Sasa kulalamika kwamba miti ilikatwa wakati marekani na nchi zilizoendelea wanatupa kila mwaka mamilioni ya miti chooni nadhani ni kuangalia mambo myopically...; Ni miti mingapi itakuwa saved kama gharama ya umeme ingeshuka kama inavyobidi ishuke (sababu production cost imepungua) kwa watu kuweza kutumia umeme badala ya kukata kuni ?
 
Nilisema humu narudia tena hata bwawa likianza uzalishaji mgao wa umeme hautaisha kwa mfumo wa uendeshaji uliopo!
 
Ngoja tuone, mambo ya serikali hayaendi hivyo...
 
Bila kuchukua ushauri huu kila siku tutaishia kuteua na kutengua
 
Elon Mask na kampuni zake amefanya sana uwekezaji kwenye solar hata akawa na kampuni inayojihulisha na mambo ya SOLA ENERGY tu . Hili suala la storage walikwisha lipatia ufumbuzi sio tatizo tena!! We don't have to invent the wheel!
 
Elon Mask na kampuni zake amefanya sana uwekezaji kwenye solar hata akawa na kampuni inayojihulisha na mambo ya SOLA ENERGY tu . Hili suala la storage walikwisha lipatia ufumbuzi sio tatizo tena!! We don't have to invent the wheel!
Hivi unaongea nini mkuu Storage ni nini ? Storage kwa solar ni battery na battery ambayo ina energy density kubwa bado Lithium which is expensive..., Unadhani watu wanaojaribu kwenye machanical storage, hydrogen storage n.k. wanapoteza muda ?

Kwa ufupi Renewable energies zote bottleneck ni Storage..., tukipata storage ya uhakika huenda hata energy ya jua kwenye Jangwa ingeweza ku-power dunia nzima..., ila ndio hivyo still watu wanaumiza vichwa kuboresha haya mambo
 
Kwa ufupi Renewable energies zote bottleneck ni Storage..., tukipata storage ya uhakika huenda hata energy ya jua kwenye Jangwa ingeweza ku-power dunia nzima..., ila ndio hivyo still watu wanaumiza vichwa kuboresha haya mambo
Mpaka hivi sasa Elon ameweza kuwa na storage capacity ya solar energy ya kuweza kutumika kwenye makazi ya Watu. In fact ameweza kuwapa umeme wa solar kwa matumizi ya mji mzima Kama majaribio huko Australia!!

Sisi hapa tungeanza na kuweza kuwapatia households umeme wa solar wa uhakika na baadae when technology will scale up storage then we shall scale up too!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…