GE2025 Bila Tundu Lissu Kuachiliwa na CHADEMA Kuruhusiwa, uhalali wa Rais Samia Suluhu utahojiwa

GE2025 Bila Tundu Lissu Kuachiliwa na CHADEMA Kuruhusiwa, uhalali wa Rais Samia Suluhu utahojiwa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Na. M. M. Mwanakijiji

Ni kweli. Rais Samia anaweza kushinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 tena kwa kishindo kweli kweli. Ni kweli. Mamilioni ya wanachama, mashabikiki na wapenzi wa Chama cha Mapinduzi wataenda kutiki kwenye sanduku la kura na kumpa kura Rais na kuandika historia ya Watanzania kumchagua Rais wa kwanza mwanamke Tanzania kuliongoza taifa letu kwa miaka mitano ijayo. Uwezekano wa Rais Samia kushinda kwa kweli haina shaka kwani ana rekodi yake inayoweza kuuzwa mbele ya Watanzania na anakuja kugombea akiwa na upepo wa ushindi ukimsukuma kama ngalawa ya Tanga. Ni kweli.

Ni kweli. Kwamba, uchaguzi huu mkuu utahusisha kundi la vyama mbalimbali vya upinzani na bila ya shaka tumeshaona wagombea mbalimbali wa Urais kutoka vyama vingine nao wakichukua fomu za kugombea Urais na hivyo ni wazi kuwa hautakuwa uchaguzi wa wa "ndiyo au hapana". Atakapoanza kampeni za kugombea Rais Samia ataenda "kupambana" na kundi la wapinzani ambao wamejipanga kushindana naye huku wengine wakigombea siyo kumpinga bali kumuunga mkono - kuna mmoja anasema hata akishidna atamuacha Rais Samia aendelee kukaa Ikulu! Ni kweli. Atakapotangazwa mshindi na chama chake kusherehekea anaweza kujitapa kuwa "uchaguzi huu ulikuwa mgumu kwelikweli". Ni kweli.

Ni kweli tena kwelikweli, kwamba CCM na mgombea wake wamejikuta na matatizo yao ya ndani wamejikuta wanafanya kazi kubwa ya kujipa uhalali wa kuwa wanakubalika kiasi cha kupindisha hata taratibu za ndani za chama na kusababisha minong'ono ya kuhoji uhalali mzima wa mchakato wa ndani. Kinachoshangaza sana ni kuwa japo tunasikia kelele na vigelegele vya "mama anaweza, mama anatosha, mama hadi 2030" inaonekana kuna watu ambao hawajiamini kiasi cha kutumia nguvu kubwa za kuzuia mijadala ya ndani.

Ni kweli vile vile kuwa ili kuweza kushinda uchaguzi huu ujao kwa mbinde na kwa upinde jitihada kubwa sana imefanyika kuiletea figisu Chama cha Demokrasia na Maendeleo ili kukivuruga na kama kuvurugika kimevurugika kwelikweli. Lakini kati ya vurugu zote za kisiasa hakuna iliyokivuruga chama hicho zaidi kutokea nje (external forces) kama jitihada ya kuhakikisha kuwa Tundu Lissu hawi mgombea wa Urais mwaka huu. Ukiondoa matatizo ya ndani ya CHADEMA (ambayo hujirudia kila baada ya miaka wakati wa uchaguzi wa mwenyekiti wao wa taifa) jitihada za kiserikali kuhakikisha kuwa Tundu Lissu hasimami kujenga hoja dhidi ya Serikali ya CCM na Rais Samia Suluhu Hassan zimefanyika kwa mafanikio makubwa. Ni kweli.

Kesi inayoitwa ya Uhaini dhidi ya Tundu Lissu, ni mojawapo ya kesi za kijinga kabisa kuweza kuletwa katika mahakama zetu na watu wenye akili timamu ambao hutambulishwa kama "wasomi". Kwa taifa ambalo limepitia kesi tatu (mbili bara na moja Zanzibar) kubwa za uhaini kesi hii ya Tundu Lissu siyo tu haina kichwa wala miguu kweli kweli kabisa haina mkia wala manyonya! Kwamba, wameamua kumshikilia Tundu Lissu kama mfungwa wa kisiasa ili tu asishiriki uchaguzi mkuu kama mgombea ni jambo la kiwoga, la aibu, na linatia doa kubwa katika utendaji wa mfumo wetu wa sheria.

Ningekuwa mimi TAL leo ningekubali hatia I would pleaded guilty) ili watoe hiyo hukumu yao ya kifo; wala nisingechukua muda kujitetea kila baada ya wiki na kuwabembeleza sijui wapeleke kesi Mahakama Kuu; as a matter of fact, ningesimama mute! Wao waendeshe kesi yao, mashahidi wao, na hukumu yao! Kuendelea kuwanukulia vifungu vya sheria kila baada ya wiki ni kucheza nao mchezo wa "tukuone maringo yako bingiribingiri mpaka chini" a.k.a "turinge bayoyo!".

Ni kweli uhalali wa ushindi wa Rais Samia utahojiwa siyo tu na Watanzania wa sasa bali na historia. Hataweza kutamba kuwa alishinda uchaguzi mkuu wa 2025 wakati mpinnzani mkuu kawekwa ndani. Ni sawa na kuingia ulingoni huku mshindani wake umemfunga kamba, mikono na miguu, umemuacha midogo tu aseme na kupiga kelele. Unadunda dunda ulingoni mashabiki wako wanashangilia kuwa uko fiti huku unamdunda mshindani wako hadi anaangukia kamba hawezi hata kuamka halafu unavishwa mkanda wa ushindi na kusifiwa kuwa umeshinda kwa knock out round ya kwanza!! kweli utabebwa mabegani na magari yataandamana kusherehekea lakini wenye macho watasema.... ni kweli.

Hivyo basi hakuna namna. Uhalali wa Rais Samia unategemea kuachiliwa kwa Tundu Lissu na kuruhusiwa kwama CHADEMA kushiriki uchaguzi mkuu bila kufungwa pingu shingoni, miguuni, na mikononi. Uchaguzi utafanyika hata bila reforms lakini uhalali wao wa kuwa madarakani utachochea upinzani zaidi wa serikali kuelekea 2030. Niwe wa kwanza kusema kuwa endapo TAL na CHADEMA hawatoruhusiwa kushikiri uchaguzi huu, Watanzania wajiandae kuona mwisho wa utawala wa CCM Rais Samia akiwa ni Rais wa mwisho wa CCM kuelekea 2030. Ule UNABII utaenda kutimia.

Ni kweli, tena kwelikweli.
Mtu anasema atakinukisha,unataka mamlaka isifuatilie kujua kwa kumdhibiti aliyeropoka?
Mnajidanganya sana,kwamba nyie nyumbu wa chadema ndio washindani wa ccm?,nyie ni si lolote,endeleeni kuzurula mahakamani
 
Kukinukisha siyo kosa la uhaini; unajua wangapo siyo tu wamewahi kusema watakinukisha lakini walikinukisha hadi Nyerere akasema "nchii hii inanuka..."? Na wengine wanakinukisha hadi leo.
 
Tafsrii ya kukinukishs ni nini?
 
G55 na Mbowe ndio waliuza silaha za TL kwa watawala bila TL kujijua amezungukwa na nani? Ndio hao wanataka kuwa mashahidi dhidi yake.

Binafsi sikuwahi kuwa shabiki wa TL ila kwa hili naomba tusihishie humu tu, tuonyeshe hisia za kweli dhidi ya tawala kandamizi ipo siku humu ndani tunatumia majina sio halisi tutayapata kama haya anayofanyiwa TL leo.
 
Huwezi kuhalalisha haramu.
Ninavyofahamu CDM hawapo tayari kuingia kwenye uchaguzi na kiongozi wao ameenda mbali na kutaka kuukwamisha uchaguzi na kwa kinywa chake akikiri kuwa mhaini.
Mzee Mwanakijiji unataka kuweka precedence kwamba nchii hii uchaguzi maana yake ni ushiriki wa Chadema tu??

By the way Sidhani kama kuna Utawala haujawahi kuhojiwa au kutiliwa mashaka au kushutumiwa.kwa kuwa hii ni haki ya msingi ya kikatiba.
Haiwezekani kusimamisha uchaguzi kwa maoni na maslahi ya Tundu lissu halafu ukaacha matamanio ya watanzania zaidi ya milioni 60.
Tundu Lissu hakuwa na uwezo na hana uwezo wa kuzuia uchaguzi usifanyike Tanzania. Na kama ulivyosema kuna mamilioni ya watu Tanzania wanaotaka uchaguzi ufanyike. Tundu hawezi kwa kusema tu kuwa uchaguzi usifanyike basi serikali iogope kuwa uchaguzi unaweza usifanyike. Lakini vile vile, Uhaini siyo kosa rahisi hivi walivyofanya; uhaini ni 'uasi dhidi ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania". Na hii inahusisha kutaka kuiondoa serikali halali madarakani kwa nguvu au kujaribu kutaka kuiondoa kwa nguvu.

Kosa ambalo Lissu angeweza kushtakiwa nalo ni ama "uchochezi" ambalo kwa kweli kauli zake zinaweza kulindwa na haki ya kutoa maoni. Maneno makali na yenye kuudhi yanalindwa na haki ya kutoa maoni. Nimesema mara kadhaa humu kuwa uhuru wa maoni haulindi maoni mazuri, ya kusifia na yenye kupendeza watawala.
 
Tunaamini Tundu Lissu hakukamatwa sio kw sababu anakosa bali kwa sababu ya Umahiri wake, uwezo wake, uzalendo wake, ujuzi wake na Utisho wake kwa maadui wake.
 
Some tymz tusichukulie hili jambo Kwa wepesi, hivi kauli alizotoa zingeleta madhara Kwa taifa ingekuwaje? Hata wakiamua kumuuacha abadilike Watz sio wapumbavu tuendeshwe Kwa mawazo ya mpuuzi m1.
Lakini watu kutekwa,bakwa, lawitiwa na rekodiwa video za uchi watanzania ndo wanapenda
 
Kwani serikali iliizuia CHADEMA isishiriki Uchaguzi Mkuu? Mbona tunakuwa kama Mbunge David McAllister wa Bunge la Ulaya; anasema "CHADEMA iruhusiwe kushiriki uchaguzi!" McAllister naweza kumlaumu mzembe hana taarifa za kutosha, lakini hata sisi tunaoishi nchini humu tunaandika CHDEMA iruhusiwe? Tunapswa kusema CHADEMA ilishindwa kufanya strategic calculation kwa kususia uchaguzi.

if I were you chief, ningeandika; Dawa iliyopo, viongozi wa CHADEMA warudi wawaambie wafuasI wao kuwa, 1. Walikosea hesabu kimkakati kuhusu kususia uchaguzi.

2. Waone mwanya wa kisheria au mafidhiano ya kuomba kuruhusiwa kushiriki uchaguzi. Ni lazima tuache kupenda kuonyesha kila kosa ni la serikali hata kama mtu katumia uhuru wake vibaya kwa kujisaidia sebleni kwake.
Kwamba cdm wanatakiwa kuendelea kushiriki kila uchaguzi hata kama madai yao ni ya haki, na ahadi za awali ilikuwa ni kufanyika kwa mabadiliko ya kweli? Maridhiano si ndio hayo yalishindikana kwa serekali kugoma kutekeleza yanayolalamikiwa?

Cdm ningewadharau sana kama wangekubali kushiriki uchaguzi wa kihuni, hata baada ya uchaguzi wa SM wa 2014 kuchezewa kama zilizopita. Huu utetezi wako ni wa watu wanaofumbia macho madai ya kweli, kwa kisingizio cha kutii sheria.
 
Huwezi kuhalalisha haramu.
Ninavyofahamu CDM hawapo tayari kuingia kwenye uchaguzi na kiongozi wao ameenda mbali na kutaka kuukwamisha uchaguzi na kwa kinywa chake akikiri kuwa mhaini.
Mzee Mwanakijiji unataka kuweka precedence kwamba nchii hii uchaguzi maana yake ni ushiriki wa Chadema tu??

By the way Sidhani kama kuna Utawala haujawahi kuhojiwa au kutiliwa mashaka au kushutumiwa.kwa kuwa hii ni haki ya msingi ya kikatiba.
Haiwezekani kusimamisha uchaguzi kwa maoni na maslahi ya Tundu lissu halafu ukaacha matamanio ya watanzania zaidi ya milioni 60.
Sasa kama amekiri kua ni mhaini,si utakua unashangaa kwanini kesi inachukua muda mrefu hivi?
Kwanini wasimnyinge tu fasta?
 
Kukinukisha siyo kosa la uhaini; unajua wangapo siyo tu wamewahi kusema watakinukisha lakini walikinukisha hadi Nyerere akasema "nchii hii inanuka..."? Na wengine wanakinukisha hadi leo.
Technicalities kisheria inaweza kutumika,tukiangalia basics za men's rea na actually reus kwa kiwango tunaweza pata ground za kumzuia tapeli lissu
 
Back
Top Bottom