GE2025 Bila Tundu Lissu Kuachiliwa na CHADEMA Kuruhusiwa, uhalali wa Rais Samia Suluhu utahojiwa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Ukiondoa matatizo ya ndani ya CHADEMA (ambayo hujirudia kila baada ya miaka wakati wa uchaguzi wa mwenyekiti wao wa taifa) jitihada za kiserikali kuhakikisha kuwa Tundu Lissu hasimami kujenga hoja dhidi ya Serikali ya CCM na Rais Samia Suluhu Hassan zimefanyika kwa mafanikio makubwa. Ni kweli.
Bibi yangu mwenye kadi ya TANU TAL anamuita KIMBUNGA yaan kila akiangalia habari utamsikia anasema "njooni mmuone KIMBUNGA" akimaanisha njooni mumuone Tundu Antipas Lissu, KIMBUNGA hakifungiwi gerezani mkumbusheni yule Mama anaejifanya Kiziwi kumbe anasikia
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Ni kweli. Rais Samia anaweza kushinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 tena kwa kishindo kweli kweli. Ni kweli. Mamilioni ya wanachama, mashabikiki na wapenzi wa Chama cha Mapinduzi wataenda kutiki kwenye sanduku la kura na kumpa kura Rais na kuandika historia ya Watanzania kumchagua Rais wa kwanza mwanamke Tanzania kuliongoza taifa letu kwa miaka mitano ijayo. Uwezekano wa Rais Samia kushinda kwa kweli haina shaka kwani ana rekodi yake inayoweza kuuzwa mbele ya Watanzania na anakuja kugombea akiwa na upepo wa ushindi ukimsukuma kama ngalawa ya Tanga. Ni kweli.

Ni kweli. Kwamba, uchaguzi huu mkuu utahusisha kundi la vyama mbalimbali vya upinzani na bila ya shaka tumeshaona wagombea mbalimbali wa Urais kutoka vyama vingine nao wakichukua fomu za kugombea Urais na hivyo ni wazi kuwa hautakuwa uchaguzi wa wa "ndiyo au hapana". Atakapoanza kampeni za kugombea Rais Samia ataenda "kupambana" na kundi la wapinzani ambao wamejipanga kushindana naye huku wengine wakigombea siyo kumpinga bali kumuunga mkono - kuna mmoja anasema hata akishidna atamuacha Rais Samia aendelee kukaa Ikulu! Ni kweli. Atakapotangazwa mshindi na chama chake kusherehekea anaweza kujitapa kuwa "uchaguzi huu ulikuwa mgumu kwelikweli". Ni kweli.

Ni kweli tena kwelikweli, kwamba CCM na mgombea wake wamejikuta na matatizo yao ya ndani wamejikuta wanafanya kazi kubwa ya kujipa uhalali wa kuwa wanakubalika kiasi cha kupindisha hata taratibu za ndani za chama na kusababisha minong'ono ya kuhoji uhalali mzima wa mchakato wa ndani. Kinachoshangaza sana ni kuwa japo tunasikia kelele na vigelegele vya "mama anaweza, mama anatosha, mama hadi 2030" inaonekana kuna watu ambao hawajiamini kiasi cha kutumia nguvu kubwa za kuzuia mijadala ya ndani.

Ni kweli vile vile kuwa ili kuweza kushinda uchaguzi huu ujao kwa mbinde na kwa upinde jitihada kubwa sana imefanyika kuiletea figisu Chama cha Demokrasia na Maendeleo ili kukivuruga na kama kuvurugika kimevurugika kwelikweli. Lakini kati ya vurugu zote za kisiasa hakuna iliyokivuruga chama hicho zaidi kutokea nje (external forces) kama jitihada ya kuhakikisha kuwa Tundu Lissu hawi mgombea wa Urais mwaka huu. Ukiondoa matatizo ya ndani ya CHADEMA (ambayo hujirudia kila baada ya miaka wakati wa uchaguzi wa mwenyekiti wao wa taifa) jitihada za kiserikali kuhakikisha kuwa Tundu Lissu hasimami kujenga hoja dhidi ya Serikali ya CCM na Rais Samia Suluhu Hassan zimefanyika kwa mafanikio makubwa. Ni kweli.

Kesi inayoitwa ya Uhaini dhidi ya Tundu Lissu, ni mojawapo ya kesi za kijinga kabisa kuweza kuletwa katika mahakama zetu na watu wenye akili timamu ambao hutambulishwa kama "wasomi". Kwa taifa ambalo limepitia kesi tatu (mbili bara na moja Zanzibar) kubwa za uhaini kesi hii ya Tundu Lissu siyo tu haina kichwa wala miguu kweli kweli kabisa haina mkia wala manyonya! Kwamba, wameamua kumshikilia Tundu Lissu kama mfungwa wa kisiasa ili tu asishiriki uchaguzi mkuu kama mgombea ni jambo la kiwoga, la aibu, na linatia doa kubwa katika utendaji wa mfumo wetu wa sheria.

Ningekuwa mimi TAL leo ningekubali hatia I would pleaded guilty) ili watoe hiyo hukumu yao ya kifo; wala nisingechukua muda kujitetea kila baada ya wiki na kuwabembeleza sijui wapeleke kesi Mahakama Kuu; as a matter of fact, ningesimama mute! Wao waendeshe kesi yao, mashahidi wao, na hukumu yao! Kuendelea kuwanukulia vifungu vya sheria kila baada ya wiki ni kucheza nao mchezo wa "tukuone maringo yako bingiribingiri mpaka chini" a.k.a "turinge bayoyo!".

Ni kweli uhalali wa ushindi wa Rais Samia utahojiwa siyo tu na Watanzania wa sasa bali na historia. Hataweza kutamba kuwa alishinda uchaguzi mkuu wa 2025 wakati mpinnzani mkuu kawekwa ndani. Ni sawa na kuingia ulingoni huku mshindani wake umemfunga kamba, mikono na miguu, umemuacha midogo tu aseme na kupiga kelele. Unadunda dunda ulingoni mashabiki wako wanashangilia kuwa uko fiti huku unamdunda mshindani wako hadi anaangukia kamba hawezi hata kuamka halafu unavishwa mkanda wa ushindi na kusifiwa kuwa umeshinda kwa knock out round ya kwanza!! kweli utabebwa mabegani na magari yataandamana kusherehekea lakini wenye macho watasema.... ni kweli.

Hivyo basi hakuna namna. Uhalali wa Rais Samia unategemea kuachiliwa kwa Tundu Lissu na kuruhusiwa kwama CHADEMA kushiriki uchaguzi mkuu bila kufungwa pingu shingoni, miguuni, na mikononi. Uchaguzi utafanyika hata bila reforms lakini uhalali wao wa kuwa madarakani utachochea upinzani zaidi wa serikali kuelekea 2030. Niwe wa kwanza kusema kuwa endapo TAL na CHADEMA hawatoruhusiwa kushikiri uchaguzi huu, Watanzania wajiandae kuona mwisho wa utawala wa CCM Rais Samia akiwa ni Rais wa mwisho wa CCM kuelekea 2030. Ule UNABII utaenda kutimia.

Ni kweli, tena kwelikweli.
Uchaguzi bila chadema ni sawa na kula Ugali bila mboga, vyama vingine si vya upinzani ni vyama bendera fuata upepo havifai kuitwa vyama vya upinzani
 
Bahati mbaya sana RA na JMK wanaangalia zaidi maslahi yao binafsi tu hata taifa likiangamia hawajali
 
Mkongwe wa jf. Huwa tunawamiss sana. Kama wao ndani ya chama hawajiamini kiasi cha kupindusha kanuni zao unadhani wataruhusu mropokaji Lisu aingie barabarani? Kumuachia Lisu aingie barabarani na huo mgawanyiko wa ndani ya chama mama hatafika hata misa ya kwanza. Nionavyo mimi Lisu ataachiwa pale baada ya mama na genge lake kujihakikishia kiti. Hiyo ni baada ya oktoba 29 na si vinginevyo.
Lisu ataachiwa na kuna Tamko toka UN na pia Trump la kuwaonya Tanzania watende haki kuwepo na Tume huru ya uchaguzi vyama vyote vishiriki uchaguzi na Tundu Lisu aachiwe mara moja
 
Kwani serikali iliizuia CHADEMA isishiriki Uchaguzi Mkuu? Mbona tunakuwa kama Mbunge David McAllister wa Bunge la Ulaya; anasema "CHADEMA iruhusiwe kushiriki uchaguzi!" McAllister naweza kumlaumu mzembe hana taarifa za kutosha, lakini hata sisi tunaoishi nchini humu tunaandika CHDEMA iruhusiwe? Tunapswa kusema CHADEMA ilishindwa kufanya strategic calculation kwa kususia uchaguzi.

if I were you chief, ningeandika; Dawa iliyopo, viongozi wa CHADEMA warudi wawaambie wafuasI wao kuwa, 1. Walikosea hesabu kimkakati kuhusu kususia uchaguzi.

2. Waone mwanya wa kisheria au mafidhiano ya kuomba kuruhusiwa kushiriki uchaguzi. Ni lazima tuache kupenda kuonyesha kila kosa ni la serikali hata kama mtu katumia uhuru wake vibaya kwa kujisaidia sebleni kwake.
Hiyo namba mbili naona sasa ni kujidharirisha kwa Chadema. Waenda kuomba kwa nani? Kwamba haki ya kushiriki fair election inaombwa!!!. Wahakikishie Chadema kwamba option ya Kisheria inaweza kuwasaidia katika mazingira ya sasa. Surely ni kupoteza muda tu.
 
Chadema wana haki ya kudai Tume huru kukataa makandokando yote toka ccm pasipo kuwanyenyekea kwani ni haki kidemokrasia
 
Ningekuwa mimi TAL leo ningekubali hatia I would pleaded guilty) ili watoe hiyo hukumu yao ya kifo; wala nisingechukua muda kujitetea kila baada ya wiki na kuwabembeleza sijui wapeleke kesi Mahakama Kuu; as a matter of fact, ningesimama mute! Wao waendeshe kesi yao, mashahidi wao, na hukumu yao! Kuendelea kuwanukulia vifungu vya sheria kila baada ya wiki ni kucheza nao mchezo wa "tukuone maringo yako bingiribingiri mpaka chini" a.k.a "turinge bayoyo!".
Tatizo hata kesi haijafika hatua ya yeye ku-plead guilty. Inaweza isifike huko!
 
Mpumbavu huyo sasa magoli yamehamishiwa kuhojiwa uhalali wa uraisi hahaa kutokea no reform kukinukisha hahaaa kazi mnayo uzuri wa samia hajibu yy kipole kipole ameshika samia anijibu sijui hajui jeuri ya wazanzibar anazisikia tu na hv mpina keshakula keki ya taifa mambo swariii baada ya 2 years mpina atarudi ccm
Alisema ni Chura kiziwi hawezi jibu
 
Uchaguzi bila chadema ni sawa na kula Ugali bila mboga, vyama vingine si vya upinzani ni vyama bendera fuata upepo havifai kuitwa vyama vya upinzani
Ni muda wa vyama hivyo angalau kuonekana vipo na kuvuna kodi zetu. Baada ya uchaguzi they are simply as good as a toilet paper.
 
Na huo ndio ukweli CCM wanaenda kukizika chama wenyewe kwa huu ujinga wanaoufanya..!!
Wanajizikaje wakati wataua ikulu?.Ukishaingia ikulu umemaliza.Chadema ndio wanaojizika maana hawatakua popote sio bungeni sio ikulu.
 
Some tymz tusichukulie hili jambo Kwa wepesi, hivi kauli alizotoa zingeleta madhara Kwa taifa ingekuwaje? Hata wakiamua kumuuacha abadilike Watz sio wapumbavu tuendeshwe Kwa mawazo ya mpuuzi m1.
 
Mkurupuko ukisikia neno chadema tu kunyeleo kinapwita
Hujaelewa.
Kuna uhaini unaofanywa na mtu mmoja? Yaani mtu apange uhaini dar mbele ya media aachwe akalale kwake regeta atoke tegeta akakamatiwe mbinga?
Mwambie ukweli huyu nyang'au hajui chochote! Uhaini unatangazwa hadharani na mtu mmoja?
 
Chadema wanajiona wao ndio wa Tanzania pekee,kwani ili uchaguzi uwe halali lazima chadema washiriki?
Wanajipa umuhimu wasiokua nao.Wanasahau kua cha muhimu ni nchi sio vyama.vyama viliikuta nchi na vitaondoka ila viondokee vikiiacha nchi salama.
 
Mkubwa heshima yako umemaliza hapa uhalali watakosa ila TAL ndio game changer wa hizi siasa tumelishwa sana viini macho kwenye siasa za upinzani kwa muda wote kumbe tawala ndio wana rule kote kote nakuamua nani akae wapi ila ile January 21 ndio zilipozaliwa siasa za upinzani tunaelekea pazuri
Sahihi kabisa. Januari mwaka 2025 ndio tulijua kwa wazi nani huwa anauza na kununua wapinzani wa nchi hii. Kaua NCCR, kaua CUF, now anapambana luua Chadema kwa kila namna. Ila tusiupuzie matamko ya wachungaji na maaskofu. Wakushupaza shingo hawa wanasiasa wataangamia
 
Mimi nachojua tutazuia uchaguzi aisesiku hyo kama hujipendi nenda kapige kura😞😤..mmetuzoea sana mbwa nyinyi
 
Mwambie ukweli huyu nyang'au hajui chochote! Uhaini unatangazwa hadharani na mtu mmoja?
Hajui lolote huyu. Anafikiri kutaja tu utawala wa sheria kunatosha mtu kuwa muumini wake.? Wanamshikiria mtu kwasababu za kushindwa kujibu anayohubiri kisha wanasingizia UHAINI???
 
Back
Top Bottom