GE2025 Bila Tundu Lissu Kuachiliwa na CHADEMA Kuruhusiwa, uhalali wa Rais Samia Suluhu utahojiwa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kuna taarifa zisizo rasmi kuwa Polisi na wenzake wamemwambia kuwa ENDAPO Lissu atagombea na chama chake kushiriki uchaguzi basi POLISI hata wakiiba kura na kuwa-harass kiasi gani wapinzani bado CCM hawataweza kutoboa. Kwahio, the only option ni kuhakikisha kuwa CHADEMA inadhibitiwa iwe kihalali au kipumbavu (kama ilivyo sasa)
Duh 🙄 !
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Ni kweli. Rais Samia anaweza kushinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 tena kwa kishindo kweli kweli. Ni kweli. Mamilioni ya wanachama, mashabikiki na wapenzi wa Chama cha Mapinduzi wataenda kutiki kwenye sanduku la kura na kumpa kura Rais na kuandika historia ya Watanzania kumchagua Rais wa kwanza mwanamke Tanzania kuliongoza taifa letu kwa miaka mitano ijayo. Uwezekano wa Rais Samia kushinda kwa kweli haina shaka kwani ana rekodi yake inayoweza kuuzwa mbele ya Watanzania na anakuja kugombea akiwa na upepo wa ushindi ukimsukuma kama ngalawa ya Tanga. Ni kweli.

Ni kweli. Kwamba, uchaguzi huu mkuu utahusisha kundi la vyama mbalimbali vya upinzani na bila ya shaka tumeshaona wagombea mbalimbali wa Urais kutoka vyama vingine nao wakichukua fomu za kugombea Urais na hivyo ni wazi kuwa hautakuwa uchaguzi wa wa "ndiyo au hapana". Atakapoanza kampeni za kugombea Rais Samia ataenda "kupambana" na kundi la wapinzani ambao wamejipanga kushindana naye huku wengine wakigombea siyo kumpinga bali kumuunga mkono - kuna mmoja anasema hata akishidna atamuacha Rais Samia aendelee kukaa Ikulu! Ni kweli. Atakapotangazwa mshindi na chama chake kusherehekea anaweza kujitapa kuwa "uchaguzi huu ulikuwa mgumu kwelikweli". Ni kweli.

Ni kweli tena kwelikweli, kwamba CCM na mgombea wake wamejikuta na matatizo yao ya ndani wamejikuta wanafanya kazi kubwa ya kujipa uhalali wa kuwa wanakubalika kiasi cha kupindisha hata taratibu za ndani za chama na kusababisha minong'ono ya kuhoji uhalali mzima wa mchakato wa ndani. Kinachoshangaza sana ni kuwa japo tunasikia kelele na vigelegele vya "mama anaweza, mama anatosha, mama hadi 2030" inaonekana kuna watu ambao hawajiamini kiasi cha kutumia nguvu kubwa za kuzuia mijadala ya ndani.

Ni kweli vile vile kuwa ili kuweza kushinda uchaguzi huu ujao kwa mbinde na kwa upinde jitihada kubwa sana imefanyika kuiletea figisu Chama cha Demokrasia na Maendeleo ili kukivuruga na kama kuvurugika kimevurugika kwelikweli. Lakini kati ya vurugu zote za kisiasa hakuna iliyokivuruga chama hicho zaidi kutokea nje (external forces) kama jitihada ya kuhakikisha kuwa Tundu Lissu hawi mgombea wa Urais mwaka huu. Ukiondoa matatizo ya ndani ya CHADEMA (ambayo hujirudia kila baada ya miaka wakati wa uchaguzi wa mwenyekiti wao wa taifa) jitihada za kiserikali kuhakikisha kuwa Tundu Lissu hasimami kujenga hoja dhidi ya Serikali ya CCM na Rais Samia Suluhu Hassan zimefanyika kwa mafanikio makubwa. Ni kweli.

Kesi inayoitwa ya Uhaini dhidi ya Tundu Lissu, ni mojawapo ya kesi za kijinga kabisa kuweza kuletwa katika mahakama zetu na watu wenye akili timamu ambao hutambulishwa kama "wasomi". Kwa taifa ambalo limepitia kesi tatu (mbili bara na moja Zanzibar) kubwa za uhaini kesi hii ya Tundu Lissu siyo tu haina kichwa wala miguu kweli kweli kabisa haina mkia wala manyonya! Kwamba, wameamua kumshikilia Tundu Lissu kama mfungwa wa kisiasa ili tu asishiriki uchaguzi mkuu kama mgombea ni jambo la kiwoga, la aibu, na linatia doa kubwa katika utendaji wa mfumo wetu wa sheria.

Ningekuwa mimi TAL leo ningekubali hatia I would pleaded guilty) ili watoe hiyo hukumu yao ya kifo; wala nisingechukua muda kujitetea kila baada ya wiki na kuwabembeleza sijui wapeleke kesi Mahakama Kuu; as a matter of fact, ningesimama mute! Wao waendeshe kesi yao, mashahidi wao, na hukumu yao! Kuendelea kuwanukulia vifungu vya sheria kila baada ya wiki ni kucheza nao mchezo wa "tukuone maringo yako bingiribingiri mpaka chini" a.k.a "turinge bayoyo!".

Ni kweli uhalali wa ushindi wa Rais Samia utahojiwa siyo tu na Watanzania wa sasa bali na historia. Hataweza kutamba kuwa alishinda uchaguzi mkuu wa 2025 wakati mpinnzani mkuu kawekwa ndani. Ni sawa na kuingia ulingoni huku mshindani wake umemfunga kamba, mikono na miguu, umemuacha midogo tu aseme na kupiga kelele. Unadunda dunda ulingoni mashabiki wako wanashangilia kuwa uko fiti huku unamdunda mshindani wako hadi anaangukia kamba hawezi hata kuamka halafu unavishwa mkanda wa ushindi na kusifiwa kuwa umeshinda kwa knock out round ya kwanza!! kweli utabebwa mabegani na magari yataandamana kusherehekea lakini wenye macho watasema.... ni kweli.

Hivyo basi hakuna namna. Uhalali wa Rais Samia unategemea kuachiliwa kwa Tundu Lissu na kuruhusiwa kwama CHADEMA kushiriki uchaguzi mkuu bila kufungwa pingu shingoni, miguuni, na mikononi. Uchaguzi utafanyika hata bila reforms lakini uhalali wao wa kuwa madarakani utachochea upinzani zaidi wa serikali kuelekea 2030. Niwe wa kwanza kusema kuwa endapo TAL na CHADEMA hawatoruhusiwa kushikiri uchaguzi huu, Watanzania wajiandae kuona mwisho wa utawala wa CCM Rais Samia akiwa ni Rais wa mwisho wa CCM kuelekea 2030. Ule UNABII utaenda kutimia.

Ni kweli, tena kwelikweli.
Hii kesi ni ya kipekee, mwanadamu asipotenda hakika juu ya Lissu, Mungu atatenda hakika juu ya Lissu, ni suala la muda tu. Haya yote yanayotokea Mungu ameacha yatokee ili mapenzi yake yatimizwe. Pia ni fursa kwa wenye mamlaka kufuata njia ya kweli
 
Kuna watu walitakiwa kuishia kuwa walinzi,msekretary, wafagia ofisi, walitakiwa kuwa wauza genge, au wasimamizi wa maghala ya nafaka.

Ila kwasababu watu wenye Hekima walichagua kukaa kimya na kupuuza sampuli hii ya watu wa kawaida kabisa kupenyezwa na kupewa mamlaka kubwa ,leo tunavuna matokeo ya kuzembea.

Mkulima asipokuwa mkali na shamba lake na kucheza na nyani ,watamaliza mazao yote na yeye ndie atabeba hasara.

Watolewe. Hakuna namna.
Watolewe na nani !?? 😳
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Ni kweli. Rais Samia anaweza kushinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 tena kwa kishindo kweli kweli. Ni kweli. Mamilioni ya wanachama, mashabikiki na wapenzi wa Chama cha Mapinduzi wataenda kutiki kwenye sanduku la kura na kumpa kura Rais na kuandika historia ya Watanzania kumchagua Rais wa kwanza mwanamke Tanzania kuliongoza taifa letu kwa miaka mitano ijayo. Uwezekano wa Rais Samia kushinda kwa kweli haina shaka kwani ana rekodi yake inayoweza kuuzwa mbele ya Watanzania na anakuja kugombea akiwa na upepo wa ushindi ukimsukuma kama ngalawa ya Tanga. Ni kweli.

Ni kweli. Kwamba, uchaguzi huu mkuu utahusisha kundi la vyama mbalimbali vya upinzani na bila ya shaka tumeshaona wagombea mbalimbali wa Urais kutoka vyama vingine nao wakichukua fomu za kugombea Urais na hivyo ni wazi kuwa hautakuwa uchaguzi wa wa "ndiyo au hapana". Atakapoanza kampeni za kugombea Rais Samia ataenda "kupambana" na kundi la wapinzani ambao wamejipanga kushindana naye huku wengine wakigombea siyo kumpinga bali kumuunga mkono - kuna mmoja anasema hata akishidna atamuacha Rais Samia aendelee kukaa Ikulu! Ni kweli. Atakapotangazwa mshindi na chama chake kusherehekea anaweza kujitapa kuwa "uchaguzi huu ulikuwa mgumu kwelikweli". Ni kweli.

Ni kweli tena kwelikweli, kwamba CCM na mgombea wake wamejikuta na matatizo yao ya ndani wamejikuta wanafanya kazi kubwa ya kujipa uhalali wa kuwa wanakubalika kiasi cha kupindisha hata taratibu za ndani za chama na kusababisha minong'ono ya kuhoji uhalali mzima wa mchakato wa ndani. Kinachoshangaza sana ni kuwa japo tunasikia kelele na vigelegele vya "mama anaweza, mama anatosha, mama hadi 2030" inaonekana kuna watu ambao hawajiamini kiasi cha kutumia nguvu kubwa za kuzuia mijadala ya ndani.

Ni kweli vile vile kuwa ili kuweza kushinda uchaguzi huu ujao kwa mbinde na kwa upinde jitihada kubwa sana imefanyika kuiletea figisu Chama cha Demokrasia na Maendeleo ili kukivuruga na kama kuvurugika kimevurugika kwelikweli. Lakini kati ya vurugu zote za kisiasa hakuna iliyokivuruga chama hicho zaidi kutokea nje (external forces) kama jitihada ya kuhakikisha kuwa Tundu Lissu hawi mgombea wa Urais mwaka huu. Ukiondoa matatizo ya ndani ya CHADEMA (ambayo hujirudia kila baada ya miaka wakati wa uchaguzi wa mwenyekiti wao wa taifa) jitihada za kiserikali kuhakikisha kuwa Tundu Lissu hasimami kujenga hoja dhidi ya Serikali ya CCM na Rais Samia Suluhu Hassan zimefanyika kwa mafanikio makubwa. Ni kweli.

Kesi inayoitwa ya Uhaini dhidi ya Tundu Lissu, ni mojawapo ya kesi za kijinga kabisa kuweza kuletwa katika mahakama zetu na watu wenye akili timamu ambao hutambulishwa kama "wasomi". Kwa taifa ambalo limepitia kesi tatu (mbili bara na moja Zanzibar) kubwa za uhaini kesi hii ya Tundu Lissu siyo tu haina kichwa wala miguu kweli kweli kabisa haina mkia wala manyonya! Kwamba, wameamua kumshikilia Tundu Lissu kama mfungwa wa kisiasa ili tu asishiriki uchaguzi mkuu kama mgombea ni jambo la kiwoga, la aibu, na linatia doa kubwa katika utendaji wa mfumo wetu wa sheria.

Ningekuwa mimi TAL leo ningekubali hatia I would pleaded guilty) ili watoe hiyo hukumu yao ya kifo; wala nisingechukua muda kujitetea kila baada ya wiki na kuwabembeleza sijui wapeleke kesi Mahakama Kuu; as a matter of fact, ningesimama mute! Wao waendeshe kesi yao, mashahidi wao, na hukumu yao! Kuendelea kuwanukulia vifungu vya sheria kila baada ya wiki ni kucheza nao mchezo wa "tukuone maringo yako bingiribingiri mpaka chini" a.k.a "turinge bayoyo!".

Ni kweli uhalali wa ushindi wa Rais Samia utahojiwa siyo tu na Watanzania wa sasa bali na historia. Hataweza kutamba kuwa alishinda uchaguzi mkuu wa 2025 wakati mpinnzani mkuu kawekwa ndani. Ni sawa na kuingia ulingoni huku mshindani wake umemfunga kamba, mikono na miguu, umemuacha midogo tu aseme na kupiga kelele. Unadunda dunda ulingoni mashabiki wako wanashangilia kuwa uko fiti huku unamdunda mshindani wako hadi anaangukia kamba hawezi hata kuamka halafu unavishwa mkanda wa ushindi na kusifiwa kuwa umeshinda kwa knock out round ya kwanza!! kweli utabebwa mabegani na magari yataandamana kusherehekea lakini wenye macho watasema.... ni kweli.

Hivyo basi hakuna namna. Uhalali wa Rais Samia unategemea kuachiliwa kwa Tundu Lissu na kuruhusiwa kwama CHADEMA kushiriki uchaguzi mkuu bila kufungwa pingu shingoni, miguuni, na mikononi. Uchaguzi utafanyika hata bila reforms lakini uhalali wao wa kuwa madarakani utachochea upinzani zaidi wa serikali kuelekea 2030. Niwe wa kwanza kusema kuwa endapo TAL na CHADEMA hawatoruhusiwa kushikiri uchaguzi huu, Watanzania wajiandae kuona mwisho wa utawala wa CCM Rais Samia akiwa ni Rais wa mwisho wa CCM kuelekea 2030. Ule UNABII utaenda kutimia.

Ni kweli, tena kwelikweli.
Hata bila kampeni Samia anashinda kwasababu tume ya uchaguzi ni waajiriwa wake, polisi, mahakama,magereza vyote vyake. Ushindi wake hautokani na ushawishi au mvuto kwa WaTanzania.
 
TAL angegombea vipi wakati aliweka msimamo wa no reform no election? Hata angelikuwa hajafungwa asingegombea maana huo ndio msimamo wa chama na ndio maana CDM hakuna mgombea yoyote mpaka sasa si rais, ubunge wala udiwani. Kesi aliyo nayo haina mahusiano na chadema kutoshiriki uchaguzi, waliamua kwa hiari ya kutoshiriki na ndio ikasababisha mgawanyiko kati yao na kuzaa G55, hujayaona hayo?
Mpumbavu huyo sasa magoli yamehamishiwa kuhojiwa uhalali wa uraisi hahaa kutokea no reform kukinukisha hahaaa kazi mnayo uzuri wa samia hajibu yy kipole kipole ameshika samia anijibu sijui hajui jeuri ya wazanzibar anazisikia tu na hv mpina keshakula keki ya taifa mambo swariii baada ya 2 years mpina atarudi ccm
 
Nimesoma, nime elewa. Nimekumbuka kweli utabiri wa Shekh Yahaya Hussein...
 
Huwezi kuhalalisha haramu.
Ninavyofahamu CDM hawapo tayari kuingia kwenye uchaguzi na kiongozi wao ameenda mbali na kutaka kuukwamisha uchaguzi na kwa kinywa chake akikiri kuwa mhaini.
Mzee Mwanakijiji unataka kuweka precedence kwamba nchii hii uchaguzi maana yake ni ushiriki wa Chadema tu??

By the way Sidhani kama kuna Utawala haujawahi kuhojiwa au kutiliwa mashaka au kushutumiwa.kwa kuwa hii ni haki ya msingi ya kikatiba.
Haiwezekani kusimamisha uchaguzi kwa maoni na maslahi ya Tundu lissu halafu ukaacha matamanio ya watanzania zaidi ya milioni 60.
Sio kweli. Kinacholalamikiwa hadi leo hawataki kujibu wala kufanya marekebisbo, ni kuhusu Kanuni, sheria na taratibu chafu, za upendeleo na za kibabe za uchaguzi. Rejea 2019, 2020, 2024. Unawezaje kupata ujasiri kufanya upuuzi huu kuharibu billions za Watanzania kwa uchafuzi uliopangwa ? Kwa nini tusitukanwe manyani ??? Sheria inayompa mkurugenzi wa uchaguzi kumtangaza hata mwenye kura pungufu au kubadili matokeo umewahi kuiona wapi zaidi ya Tanzania. Hayo ni maajabu ya Tanzania pekee. Nchi maskini ya kutupwa haina vyoo vya shule halafu inachezea hela kwa kutuletea kiini macho na mazingaombwe ya uchaguzi. We are not serious. Hata ndani ya chama sisi wenyewe CCM tumeanza kutumia kura feki, na nguvu ya fedha. Haina maana.
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Ni kweli. Rais Samia anaweza kushinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 tena kwa kishindo kweli kweli. Ni kweli. Mamilioni ya wanachama, mashabikiki na wapenzi wa Chama cha Mapinduzi wataenda kutiki kwenye sanduku la kura na kumpa kura Rais na kuandika historia ya Watanzania kumchagua Rais wa kwanza mwanamke Tanzania kuliongoza taifa letu kwa miaka mitano ijayo. Uwezekano wa Rais Samia kushinda kwa kweli haina shaka kwani ana rekodi yake inayoweza kuuzwa mbele ya Watanzania na anakuja kugombea akiwa na upepo wa ushindi ukimsukuma kama ngalawa ya Tanga. Ni kweli.

Ni kweli. Kwamba, uchaguzi huu mkuu utahusisha kundi la vyama mbalimbali vya upinzani na bila ya shaka tumeshaona wagombea mbalimbali wa Urais kutoka vyama vingine nao wakichukua fomu za kugombea Urais na hivyo ni wazi kuwa hautakuwa uchaguzi wa wa "ndiyo au hapana". Atakapoanza kampeni za kugombea Rais Samia ataenda "kupambana" na kundi la wapinzani ambao wamejipanga kushindana naye huku wengine wakigombea siyo kumpinga bali kumuunga mkono - kuna mmoja anasema hata akishidna atamuacha Rais Samia aendelee kukaa Ikulu! Ni kweli. Atakapotangazwa mshindi na chama chake kusherehekea anaweza kujitapa kuwa "uchaguzi huu ulikuwa mgumu kwelikweli". Ni kweli.

Ni kweli tena kwelikweli, kwamba CCM na mgombea wake wamejikuta na matatizo yao ya ndani wamejikuta wanafanya kazi kubwa ya kujipa uhalali wa kuwa wanakubalika kiasi cha kupindisha hata taratibu za ndani za chama na kusababisha minong'ono ya kuhoji uhalali mzima wa mchakato wa ndani. Kinachoshangaza sana ni kuwa japo tunasikia kelele na vigelegele vya "mama anaweza, mama anatosha, mama hadi 2030" inaonekana kuna watu ambao hawajiamini kiasi cha kutumia nguvu kubwa za kuzuia mijadala ya ndani.

Ni kweli vile vile kuwa ili kuweza kushinda uchaguzi huu ujao kwa mbinde na kwa upinde jitihada kubwa sana imefanyika kuiletea figisu Chama cha Demokrasia na Maendeleo ili kukivuruga na kama kuvurugika kimevurugika kwelikweli. Lakini kati ya vurugu zote za kisiasa hakuna iliyokivuruga chama hicho zaidi kutokea nje (external forces) kama jitihada ya kuhakikisha kuwa Tundu Lissu hawi mgombea wa Urais mwaka huu. Ukiondoa matatizo ya ndani ya CHADEMA (ambayo hujirudia kila baada ya miaka wakati wa uchaguzi wa mwenyekiti wao wa taifa) jitihada za kiserikali kuhakikisha kuwa Tundu Lissu hasimami kujenga hoja dhidi ya Serikali ya CCM na Rais Samia Suluhu Hassan zimefanyika kwa mafanikio makubwa. Ni kweli.

Kesi inayoitwa ya Uhaini dhidi ya Tundu Lissu, ni mojawapo ya kesi za kijinga kabisa kuweza kuletwa katika mahakama zetu na watu wenye akili timamu ambao hutambulishwa kama "wasomi". Kwa taifa ambalo limepitia kesi tatu (mbili bara na moja Zanzibar) kubwa za uhaini kesi hii ya Tundu Lissu siyo tu haina kichwa wala miguu kweli kweli kabisa haina mkia wala manyonya! Kwamba, wameamua kumshikilia Tundu Lissu kama mfungwa wa kisiasa ili tu asishiriki uchaguzi mkuu kama mgombea ni jambo la kiwoga, la aibu, na linatia doa kubwa katika utendaji wa mfumo wetu wa sheria.

Ningekuwa mimi TAL leo ningekubali hatia I would pleaded guilty) ili watoe hiyo hukumu yao ya kifo; wala nisingechukua muda kujitetea kila baada ya wiki na kuwabembeleza sijui wapeleke kesi Mahakama Kuu; as a matter of fact, ningesimama mute! Wao waendeshe kesi yao, mashahidi wao, na hukumu yao! Kuendelea kuwanukulia vifungu vya sheria kila baada ya wiki ni kucheza nao mchezo wa "tukuone maringo yako bingiribingiri mpaka chini" a.k.a "turinge bayoyo!".

Ni kweli uhalali wa ushindi wa Rais Samia utahojiwa siyo tu na Watanzania wa sasa bali na historia. Hataweza kutamba kuwa alishinda uchaguzi mkuu wa 2025 wakati mpinnzani mkuu kawekwa ndani. Ni sawa na kuingia ulingoni huku mshindani wake umemfunga kamba, mikono na miguu, umemuacha midogo tu aseme na kupiga kelele. Unadunda dunda ulingoni mashabiki wako wanashangilia kuwa uko fiti huku unamdunda mshindani wako hadi anaangukia kamba hawezi hata kuamka halafu unavishwa mkanda wa ushindi na kusifiwa kuwa umeshinda kwa knock out round ya kwanza!! kweli utabebwa mabegani na magari yataandamana kusherehekea lakini wenye macho watasema.... ni kweli.

Hivyo basi hakuna namna. Uhalali wa Rais Samia unategemea kuachiliwa kwa Tundu Lissu na kuruhusiwa kwama CHADEMA kushiriki uchaguzi mkuu bila kufungwa pingu shingoni, miguuni, na mikononi. Uchaguzi utafanyika hata bila reforms lakini uhalali wao wa kuwa madarakani utachochea upinzani zaidi wa serikali kuelekea 2030. Niwe wa kwanza kusema kuwa endapo TAL na CHADEMA hawatoruhusiwa kushikiri uchaguzi huu, Watanzania wajiandae kuona mwisho wa utawala wa CCM Rais Samia akiwa ni Rais wa mwisho wa CCM kuelekea 2030. Ule UNABII utaenda kutimia.

Ni kweli, tena kwelikweli.
Haya ya kawaida sana na yatapita kama mengine. Hata uhalali wa J K Nyerere ulihojiwa na akina Christopher Kasangatumbo, kisha wakawekwa detention pale Isevya Tabora na Nyerere akatawala hadi alipoachia mwenuewe 1985

Ni Rais gani utawala wake haujawahi kuhojiwa hapa Tanzania?? Sema hapa nami nikutajie kundi lililohoji!!

Nyie Sukuma Gang tunajuwa hamjawahi kumkubali Samia kuanzia Magufuli anakufa, lakini Mungu ndiyo kapanga hamna namna mtapindua. Nakushauri Mzee Mwanakijiji kuanzia Oktoba kuwa na dawa za maumivu za kutosha maana hii ni mpaka 2030
 
Kama huu uchaguzi utafanyika bila uwepo wa Lissu na Chadema basi huu uchaguzi utakuwa wa hovyo zaidi tangu chaguzi za mfumo wa vyama vingi uanze mwaka 1995
Lissu ni nani mpaka uchaguzi uwe wa HOVYO? Mwaka 1995, 2000, 2005, 2010 na 2015 kwani Lissu alikuwa hajazaliwa wakati uchaguzi unafanyika?

Acheni kumuabudu MROPOKAJI
 
Ata akiachiwa bado hatashiriki uchaguzi kwasababu reforms walizotaka hazijafanyika
 
Nionacho kutokana na kelele, Lissu wanaweza kumuchia dakika za jioni sana iwe reform imefanyika au bado.

Na CDM inaweza/isiweze kushiriki uchaguzi ikiwa haina election programs so direct wakaamua kukaa nje ya uwanja na kuwa watazamaji.

Ila TAL kweli ndiye mpinzani wa kweli ktk siasa za Tanzania, Mbowe hakutegemea hiki anachokiona.
 
Endeleeni kugoma kushiriki msubiri nyakati zijazo. Tanzania haijawahi kuamini kwenye kikundi flani ndio kisikilizwe wao tu kuliko wengine. Haiwezekani.
Kwenye neno Tanzania weka CCM...hoja yako huenda ikawa na mantiki. Upofu huu ndio unatufanya tushindwe kutofautisha Nchi na Chama.
 
Si itajulikana ndio maana tunayo mahakama.
Mnataka tuwe na Taifa ambalo mtu akiamka asubuhi anaweza kuzua taharuki na kutokana na umaarufu wake aachwe tu.
Presumably ametenda kosa na ni lazima mahakama ihusike kuthibitisha au vinginevyo.
Ukitaka kuruka agana na nyonga...waswahili husema.
Wakati annanzisha harakati za kuupinga uchaguzi lazima alikuwa na Uelewa kuwa haitakuwa rahisi ,CCM au Serikali isingeweza kukubali na ni lazima ingemdhibiti...sasa plan B yake kichwani ilikuwa ni hii ya kutaka sympathy??
Kuhusu vyama vidogo kuingia kwenye uchaguzi ni haki yao na tukumbuke hata chadema ilikuwa ndogo sana for the past 20 years...na ilikuzwa na sisi wananchi baada ya kuiona CCM ikitaka kutekwa au kuacha njia yake..
Chadema pia ilikuzwa na itashushwa na wananchi walewale...na hapa sababu ni moja tu ...kutaka madaraka kwa njia ya ukorofi itakayoliacha taifa katika mgawanyiko.
Ilikuwepo NCCR ya Mrema
Ilikuwepo CUF ya Maalim
Ilikuwepo Chadema ya Mbowe
Sasa inaanza ACT ya Zitto na Chauma ya Salum Mwalimu.
Kamwe tusitake kuitisha mifumo ya kidemokrasia kwa mgongo wa Taasisi moja.
UPINZANI WA KWELI UTATOKA NDANI YA CCM ...Iliwahi kusemwa lakini bado sana kwa kuwa CCM imeendelea kuicheza karata yake vyema hadi sasa.
CCM inautambua mtandao wa kimaslahi sio leo tu bali toka enzi za Nyerere na kwa miaka yote imeendelea kuudhibiti bila kuyumbisha Taifa.
Wewe umekurupuka na inaonekana na huijui vizuri ccm Na pengine hata mfumo mzima wa siasa. Umewahi kujiuliza kwa nini ccm inaogopa reforms zinazotoa usawa Kwa vyama vyote.
Hivyo vyote ulivyovitaja ukiiondoa Chadema vimeegemea upande mmoja. ACT bila mgawanyo wa Zanzibar haipo vinginevyo waulize CUF alipoondoka Maalim Seif leo CUF iko wapi?
Hiyo Chaumma ni tawi linaloonekana wazi kuwa lipo kwa kazi Maalum.
Upinzani wa kweli utatoka ccm, ukweli usioujua huko nyuma kujiunga na ccm ilikuwa ni lazima ikiwa unataka kufanya shughuli yoyote hata kupata elimu ya juu. Kwa hiyo si ajabu kuwaona wapinzani ambao ni watu wazima kuwa na kadi za Tanu/Ccm.
Ccm ilishapoteza credibility Kwa Watanzania ndio sababu bila aibu mnaibuka kijinga watu maskini pikipiki na baiskeli vyenye jina la Mgombea as if ndiye anamiliki hicho chama.
Mahakama za kutenda haki unazozingumzia ndio zile alizozilalamika kada na mfadhili mkubwa wa ccm Rostam?
 
Na. M. M. Mwanakijiji

Ni kweli. Rais Samia anaweza kushinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 tena kwa kishindo kweli kweli. Ni kweli. Mamilioni ya wanachama, mashabikiki na wapenzi wa Chama cha Mapinduzi wataenda kutiki kwenye sanduku la kura na kumpa kura Rais na kuandika historia ya Watanzania kumchagua Rais wa kwanza mwanamke Tanzania kuliongoza taifa letu kwa miaka mitano ijayo. Uwezekano wa Rais Samia kushinda kwa kweli haina shaka kwani ana rekodi yake inayoweza kuuzwa mbele ya Watanzania na anakuja kugombea akiwa na upepo wa ushindi ukimsukuma kama ngalawa ya Tanga. Ni kweli.

Ni kweli. Kwamba, uchaguzi huu mkuu utahusisha kundi la vyama mbalimbali vya upinzani na bila ya shaka tumeshaona wagombea mbalimbali wa Urais kutoka vyama vingine nao wakichukua fomu za kugombea Urais na hivyo ni wazi kuwa hautakuwa uchaguzi wa wa "ndiyo au hapana". Atakapoanza kampeni za kugombea Rais Samia ataenda "kupambana" na kundi la wapinzani ambao wamejipanga kushindana naye huku wengine wakigombea siyo kumpinga bali kumuunga mkono - kuna mmoja anasema hata akishidna atamuacha Rais Samia aendelee kukaa Ikulu! Ni kweli. Atakapotangazwa mshindi na chama chake kusherehekea anaweza kujitapa kuwa "uchaguzi huu ulikuwa mgumu kwelikweli". Ni kweli.

Ni kweli tena kwelikweli, kwamba CCM na mgombea wake wamejikuta na matatizo yao ya ndani wamejikuta wanafanya kazi kubwa ya kujipa uhalali wa kuwa wanakubalika kiasi cha kupindisha hata taratibu za ndani za chama na kusababisha minong'ono ya kuhoji uhalali mzima wa mchakato wa ndani. Kinachoshangaza sana ni kuwa japo tunasikia kelele na vigelegele vya "mama anaweza, mama anatosha, mama hadi 2030" inaonekana kuna watu ambao hawajiamini kiasi cha kutumia nguvu kubwa za kuzuia mijadala ya ndani.

Ni kweli vile vile kuwa ili kuweza kushinda uchaguzi huu ujao kwa mbinde na kwa upinde jitihada kubwa sana imefanyika kuiletea figisu Chama cha Demokrasia na Maendeleo ili kukivuruga na kama kuvurugika kimevurugika kwelikweli. Lakini kati ya vurugu zote za kisiasa hakuna iliyokivuruga chama hicho zaidi kutokea nje (external forces) kama jitihada ya kuhakikisha kuwa Tundu Lissu hawi mgombea wa Urais mwaka huu. Ukiondoa matatizo ya ndani ya CHADEMA (ambayo hujirudia kila baada ya miaka wakati wa uchaguzi wa mwenyekiti wao wa taifa) jitihada za kiserikali kuhakikisha kuwa Tundu Lissu hasimami kujenga hoja dhidi ya Serikali ya CCM na Rais Samia Suluhu Hassan zimefanyika kwa mafanikio makubwa. Ni kweli.

Kesi inayoitwa ya Uhaini dhidi ya Tundu Lissu, ni mojawapo ya kesi za kijinga kabisa kuweza kuletwa katika mahakama zetu na watu wenye akili timamu ambao hutambulishwa kama "wasomi". Kwa taifa ambalo limepitia kesi tatu (mbili bara na moja Zanzibar) kubwa za uhaini kesi hii ya Tundu Lissu siyo tu haina kichwa wala miguu kweli kweli kabisa haina mkia wala manyonya! Kwamba, wameamua kumshikilia Tundu Lissu kama mfungwa wa kisiasa ili tu asishiriki uchaguzi mkuu kama mgombea ni jambo la kiwoga, la aibu, na linatia doa kubwa katika utendaji wa mfumo wetu wa sheria.

Ningekuwa mimi TAL leo ningekubali hatia I would pleaded guilty) ili watoe hiyo hukumu yao ya kifo; wala nisingechukua muda kujitetea kila baada ya wiki na kuwabembeleza sijui wapeleke kesi Mahakama Kuu; as a matter of fact, ningesimama mute! Wao waendeshe kesi yao, mashahidi wao, na hukumu yao! Kuendelea kuwanukulia vifungu vya sheria kila baada ya wiki ni kucheza nao mchezo wa "tukuone maringo yako bingiribingiri mpaka chini" a.k.a "turinge bayoyo!".

Ni kweli uhalali wa ushindi wa Rais Samia utahojiwa siyo tu na Watanzania wa sasa bali na historia. Hataweza kutamba kuwa alishinda uchaguzi mkuu wa 2025 wakati mpinnzani mkuu kawekwa ndani. Ni sawa na kuingia ulingoni huku mshindani wake umemfunga kamba, mikono na miguu, umemuacha midogo tu aseme na kupiga kelele. Unadunda dunda ulingoni mashabiki wako wanashangilia kuwa uko fiti huku unamdunda mshindani wako hadi anaangukia kamba hawezi hata kuamka halafu unavishwa mkanda wa ushindi na kusifiwa kuwa umeshinda kwa knock out round ya kwanza!! kweli utabebwa mabegani na magari yataandamana kusherehekea lakini wenye macho watasema.... ni kweli.

Hivyo basi hakuna namna. Uhalali wa Rais Samia unategemea kuachiliwa kwa Tundu Lissu na kuruhusiwa kwama CHADEMA kushiriki uchaguzi mkuu bila kufungwa pingu shingoni, miguuni, na mikononi. Uchaguzi utafanyika hata bila reforms lakini uhalali wao wa kuwa madarakani utachochea upinzani zaidi wa serikali kuelekea 2030. Niwe wa kwanza kusema kuwa endapo TAL na CHADEMA hawatoruhusiwa kushikiri uchaguzi huu, Watanzania wajiandae kuona mwisho wa utawala wa CCM Rais Samia akiwa ni Rais wa mwisho wa CCM kuelekea 2030. Ule UNABII utaenda kutimia.

Ni kweli, tena kwelikweli.
Kwa mfumo wa mahakama zetu ilivyo ni kazi, hii kesi ilipaswa kufutwa kitambo Sana.Unamfunga mpinzani Wako huku ukigombea peke yako...
 
Back
Top Bottom