Bila UMAFIA hujawa tajiri bado. Umafia ndio dira ya utajiri

Bila UMAFIA hujawa tajiri bado. Umafia ndio dira ya utajiri

Hakuna mfanyabiashara anayetoka nje na kutangaza siri za mambo anayoyafanya. Labda nikupe kisa kimoja cha Bakhresa, alienda Rwanda akasili jina la "Azania" huku akijua kabisa kuwa hilo jina ni la mshindani wake hapa Tanzania. Azania Flour alipokwenda Rwanda kusajili akakuta tayari jina linamilikiwa na Bakhresa.

Huo ndio umafia wenyewe unaongelewa hapa

View attachment 2749719
Hii mbona naskia bahresa alishindwa akarudisha jina la watu
 
Mipango ya Mungu au Shetani pia. Yesu alionyeshwa miliki yote ya dunia akisujudu tu! Lakin kwa upande wa Mungu pia lazima ufanye Kazi kubwa wewe ili vizaz vyako ndo vije kurithi mfano Daudi pamoja na kwamba ulikua ni Mapango wa Mungu lakini aliua ma elfu elfu kuweka njia sawa ndo kina warithi kina suleiman wanakuja kura raha na madem zake

Siri ya utajiri ndivyo ilivyo……
Lazima uteseke ili kizazi chako kijacho kile nguvu kazi yako, iwe kwa kuua au kudhulumu.
Empire nyingi zilitengenezwa kwa style hiyo
 
Kabisa mkuu....matajiri wanaishi maisha ya ajabu sana..yupo mmoja kula yake ni ya bei ya chini mno...haangalii TV hana starehe yeyote.......halafu anasoma sana...hajichanganyi na watu....akipewa mwaliko anatuma mwakilishi......T shirt zake na jeans zina miaka zaidi ya 10.....report za biashara zake anapenda kuziweka kwenye graph,histograms,pie chart etc.
graph,histograms,pie chart ..... Ideal for prompt DATA & TRENDS VISUALIZATION
 
Hizo zote porojo za mitaani tu. Bakhresa jina lake lina kosa gani hata atumie jina la Azania?

Wacheni kudanganyana, fanyezi kazi kwa bidii, hakuna aliyezaliwa na mali na hakuna aneondoka na mali. Tumezzikuta na tunaziwacha hapa hapa.
We demu huna akili, si ukaangalie kesi mahakamani ipo

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Mpaka ufikie level ya kuwa tajiri, ni lazima uwe umefanyiwa umafia hadi na wewe unakuwa mafia mkubwa.

Utajiri ni himaya, kila jicho linaiangalia himaya kwa husda. Kuna uchawi, ujambazi, figisu na michezo yote michafu.

Ukiwa tajiri utajilinda wewe na uzao wako kiroho, kimwili na kitàaluma ili usipitwe na teknolojia.

Bila kuwekeza kwenye teknolojia utajiri wako utakuwa ni wa muda mfupi tu.
Umafia ni nini?
 
Ya kina mark Zuckerberg utayaona wapi wakati uko mbali nayo??? Tena huyo mark ndo usimzungumzie huyo ndo mafia wa mamafia,,, hata hyo Facebook halikua wazo lake kuna mtu alimpelekea hlo wazo amuundie hyo app ,,,,guess what happened next!!!

Haya hapa juz juz kauza twitter kwa elon musk afu kazindua mtandao mwngne ambao ni C&P ya twitter!!
Acha uongo. Twitter haijawahi kumilikiwa na Mark Zuckerberg.
 
Mpaka ufikie level ya kuwa tajiri, ni lazima uwe umefanyiwa umafia hadi na wewe unakuwa mafia mkubwa.

Utajiri ni himaya, kila jicho linaiangalia himaya kwa husda. Kuna uchawi, ujambazi, figisu na michezo yote michafu.

Ukiwa tajiri utajilinda wewe na uzao wako kiroho, kimwili na kitàaluma ili usipitwe na teknolojia.

Bila kuwekeza kwenye teknolojia utajiri wako utakuwa ni wa muda mfupi tu.
Utajiri ni nini, na kuwekeza kwenye teknolojia, ipi hiyo? Utajiri hasa ni nini..kuwa na mali nyingi, pesa nyingi au happiness and peace, sielewi
 
Umenena ukweli kabisa hasa hapo kwa facebook.
Kitendo cha kumnunua whatsapp ndio umafia wenyewe. Yaani hiyo ni mbadala wa kuua ila kisasa.
Ni sawa na kampuni ya bus ya Ally's akiamua kununua kampuni ya bus ya Katarama wakati wapo ruti moja ya Dar-Mwanza.
Huo ndio umafia wenyewe.
Huo umafia ni kwenye akili zenu, mnaongea kana kwamba Zuckerberg aliwawekea bunduki kichwani watu wa Whatsapp na kuwaambia wamuuzie app yao au la ...

Tech guys wengi huwa wanaanzisha start ups ili waje waziuze, huwa hawana long term plans kwa sababu wengi wao huwa hawataki kuanza kuumiza vichwa jinsi ya ku-scale up biashara ya hizo app/ websites. Pia ofa inaweza kuwa kubwa mpaka mtu inabidi uuze, ukikataa kila mtu atakuona mwehu.

Wewe umeitaja Whatsapp tu lakini apps/websites nyingi maarufu haziendeshwi na waliozianzisha kuanzia Whatsapp, Instagram, Youtube, Twitter, LinkedIn, Paypal etc.
 
Maskini ni tatizo kubwa. hayo mawazo mgando yanakuja ukiwa na njaa. njia za kumiliki hela halali zipo nyingi bila umafia.

Maskini akishafeli maisha huwa anaona kila mwenye hels ni tapeli.

Tafuta hela tu hayk mawazo mgando utayasahau
Sidhani kama mleta mada anamanisha wizi na utapeli mbona Kuna wezi na matepeli kibao na ni masikini bado
 
Labda kama kuna kesi nyingine...ila hii alishinda.

Point ya mtoa mada ni kweli, biashara na roho ya Mama Theresa itakushinda; Labda usiwe mkubwa.
Au kanunua brand anailipia?. Mana naskia azania ni supplier mkubwa wa ngano afrika mashariki na kati kwa sasa na kama ni hivyo bahresa anauzia jina Hilo Rwanda tu
 
Mpaka ufikie level ya kuwa tajiri, ni lazima uwe umefanyiwa umafia hadi na wewe unakuwa mafia mkubwa.

Utajiri ni himaya, kila jicho linaiangalia himaya kwa husda. Kuna uchawi, ujambazi, figisu na michezo yote michafu.

Ukiwa tajiri utajilinda wewe na uzao wako kiroho, kimwili na kitàaluma ili usipitwe na teknolojia.

Bila kuwekeza kwenye teknolojia utajiri wako utakuwa ni wa muda mfupi tu.
UKWEILI AMABAO HAUSEMWI WAZI.
 
Back
Top Bottom