PreGE2025 Bila VPN hauwezi kuingia X (Twitter) Tanzania. Vipi huko mnaotumia Facebook na Instagram?

PreGE2025 Bila VPN hauwezi kuingia X (Twitter) Tanzania. Vipi huko mnaotumia Facebook na Instagram?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
1_20250521_175722_0000.png

Kama unahitaji kufungua mtandao wa X ambao zamani ulikua unaitwa Twitter basi utaona kama simu yako inasumbua lakini kiuwalisia mtandao huo umefungiwa.

Mtandao wa kijamii wa x (twitter) umefungiwa nchini Tanzania baada ya akaunti mbalimbali za kiserikali na taasisi binafsi kuweza kudukuliwa jana.

2_20250521_175722_0001.png

Siku ya jumanne kupitia mtandao wa X akaunti ya polisi Tanzania iliweza kuchapisha chapisho la kushangaza baada ya kutangaza Rais kufa lakini kiuwalisia akaunti hiyo ilikua imedukuliwa na wahalifu wa mitandaoni na kuchapisha taarifa za Uongo.

Polisi waliweza kutolea taarifa ilo sakata kwa kusema inaendelea na uchunguzi kuhusu watu wote waliohusika na kudukua akaunti hiyo na kutoa machapisho ya Uongo mtandaoni.

Baada saa kadhaa mbele mtandao wa X umefungwa na haupatikani nchini Tanzania mpaka program ya Vpn, Watumiaji wengi wa mtandao huo toka Dar es salaam wanalalamika toka jana jioni mtandao wa X umefungiwa.

Je kuufunga mtandao wa X ndio suluhisho tuachie maoni yako?
 
Aisee, wahuni wakaweka na picha za ngono kabisa, hii ni aibu ya karne. Mambo ya computer yanahitaji akili smart.
 
Wakuu, Kunaweza kuwa na Mabandiki Mengi humu Jamvini Kueleza hali ya kutopatikana mtandao wa X tangu jana lakini naomba mods mliache ili bandiko Independently ili tuweze kujadili kwa kina insights za kwanini X haipo TZ kwa sasa

Baada ya Page kadhaa Za Taasisi Za umma na binafsi kuwa Hacked jana na Hackers hao kupelekea Kupost Vitu vya Kuleta Taharuki naona authority zimeona ziufungwe huo mtandao kwa muda

Mimi ninachoona Pengine hizi hacking ata zipo Plotted na Authorities ili tu kupata sababu ya Kuiondoa X hewani

Mtandao Wa X unafahamika kwa kuwa na Wafuasi wengi sana especially wana harakati na Una Connect sana na Nchi jirani kenya na uganda pamoja na Rwanda Kumekuwa Kuna midaharo Mingi sana ya Haki za Binadamu na Siasa ndani ya X

Hata maandamano ya Genz mwaka jana Kenya Yalikuwa mostly planned kwenye X kupitia Spaces ambazo ni kama Chatting room, Ilifika wakati Mpaka Rais Ruto alijoin izo space officially na kuadress Kuhusu maandamano na namna ya Vijana kutulia Hao Genz

Sasa X imekuwa Blacklisted lakini hakuna taarifa ya Kuelewaka kutoka kwenye mamlaka
 
Wanaahindwa kuwlewa kuwa kutumia VPN ni hatari zaidi
 
Hapaja wahi kuwepo uhuru wa habari zaidi tz,ukitaka kujua longa na P.
 
Sijawah liamini joka la kijani ex mpka uchaguzi uishe ndo itarejea
 
Imedukuliwe za wingine imezima yakwako hih au nawe umo kwenye group ya manjagu😎
 
Watawala wa bongo waonga sana aisee, sasa wanaogopa hata maneno tu? 😀 😀
 
mbona humu panatosha, wangeifungia jamii forum ningeteseka,,

lakini sijui tweeter, instagram na upupu wowote ule, wafungie tu,, mda wote ukiingia huko unakumbuna na picha za ovyo tu.
 
Back
Top Bottom