Acha ujinga kijana. Ukristo umeanzishwa na wazungu wa kiroma. Huko uyahudini kwa wayahudi original wala hawaujui huo ukristo kwa sababu haukuanzia katika nchi yao. Sisi waafrika wewe ukiwa mmoja wapo ndo wajinga, tumeletewa zigo la dini na kukimbilia kulipokea bila kuwaona au kuwa na ushahidi wa hao tunao ambiwa sijui mitume, sijui wafia dhambi zetu misalabani nk.
Jamaa walikuta mababu zetu wana amini vizuri na kupata matokeo chanya, hawa wakoloni wakaanza kudai eti babu zetu wanakufuru kwa kuamini mizimu, hivyo inatakiwa babu zetu wawaamini kina Yesu, Mwamedi nk. Lakini ukiangalia kimakini unakuta na hao walisema babu zetu waamini ni mizimu ile ile ya mababu wa wakoloni ambao wamewaaminisha babu zetu wawaombe wao kwa story za kuokolewa nk.
Yani mwafrika utumie maisha yako kuomba mizimu ya mababu wa kizungu, kiarabu, kiyahudi nk na kuacha ya kwako. Sasa tunajifanya tunaipenda na kuielewa story ya dini zaidi ya waliozileta. Hayo mambo ya plan B hata wewe unaweza kuyafanya mkuu, sio lazima wote tufanye kitu kimoja au tuwe na mawazo mamoja.
Ndomaana hata mapacha huwa na mawazo tofauti vilevile as long as hakuna kuvunja sheria za jukwaa, hakuna kuvunja sheria za nchi nk.