Bilionea Warren Buffett: Nikifariki mali zangu wapewe wenye uhitaji

Bilionea Warren Buffett: Nikifariki mali zangu wapewe wenye uhitaji

Uko sahihi mkuu!

Warren Buffett "hakuuokota" utajiri wake! Aliuhenyea!

Wakati Watanzania wa rika lake walipokuwa wanafurahia kuchezea tope walipokuwa na umri wa miaka saba, Warren yeye alikuwa akisoma vitabu vya biashara na uwekezaji nyumbani kwa Babu yake! Imagine mtoto wa miaka saba kusoma vitabu kama hivyo!

Wakati Watanzania wa rika lake walipokuwa wakiwaza jinsi ya kupata hela ya pipi walipokuwa na umri wa miaka tisaa, yeye alikuwa akifanya biashara ya kuuza magazeti na vizibo vya soda, na hela iliyopatikana, aliiwekeza kwa kufuata mwongozo wa vitabu alivyovisoma.

Mtanzania wa leo mwenye umri wa miaka kumi na sita akipewa milioni moja atafanyia nini? Kufikia huo umri, Warren alikuwa ameshanunua shamba lake binafsi kwa hela yake binafsi aliyoipata baada ya kufanyia kazi maarifa aliyojipatia kwa njia ya vitabu.

Hata alipoanza kupata hela nyingi, bado aliendelea kuwa makini sana na kila senti anayoipata. Ndiyo maana kuna wakati alikuwa na suti moja tu na shati moja jeupe, ambalo mara nyingi lilikuwa likifuliwa kwenye kola tu na pindo za mikononi.

Si kwamba alikuwa hapendi mavazi, hapana. Alikuwa "mbahili" ili aweze kutimiza ndoto zake, na alifanikiwa.
alilitambua lengo lake mapema katika umri ambao sisi tulikuwa tunafundishwa panzi ana miguu mingapi
 
Nashukuru mkuu, unajua kutembea kumenifundisha mengi sana
Nimetembea na kuishi nchi nyingi sana na ninaona binadamu wanavyoishi ila kwa Africa kuamka ni kazi sana inataka dedication
Hebu fikiria mtu anaiba billion za walipa kodi halafu baadhi ya wapuuzi wanasema eti hata mimi nisingeziacha
Sasa hapo unategemea maendeleo kweli
Kwanza ajali yaani wangenipa kazi hapo ningehakikisha miaka 3 ya kwanza 60% ya ajali zingeisha na miaka 5 mngekuwa mnashtuka mkisikia ajali imeuwa kama Ulaya
Najua watahoji HOW?
MAMA anipe kazi tu 😄
Mkuu, huwezi kulewa madaraka kweli 😄😄, Utaaza kuchota mihela na kuya transfer nje tena 😰
 
Mkuu, huwezi kulewa madaraka kweli 😄😄, Utaaza kuchota mihela na kuya transfer nje tena 😰
😄 mkuu usijali nimezaliwa kwenye hela siwezi kutamani hata siku moja
Father alikuwa ananipa nazihesabu nikiwa mdogo sana na ndugu zangu kama kuiba ningeanza huko

Hapa nilipo kuna jamaa aliniachia kampuni peke yangu ndio boss alirudi imezaa akaamua kunipa shares kwa hiyo jambo la kuzingatia katika Dunia hii ni Uaminifu na roho nzuri tu pamoja na ukarimu
 
Uko sahihi mkuu!

Warren Buffett "hakuuokota" utajiri wake! Aliuhenyea!

Wakati Watanzania wa rika lake walipokuwa wanafurahia kuchezea tope walipokuwa na umri wa miaka saba, Warren yeye alikuwa akisoma vitabu vya biashara na uwekezaji nyumbani kwa Babu yake! Imagine mtoto wa miaka saba kusoma vitabu kama hivyo!

Wakati Watanzania wa rika lake walipokuwa wakiwaza jinsi ya kupata hela ya pipi walipokuwa na umri wa miaka tisaa, yeye alikuwa akifanya biashara ya kuuza magazeti na vizibo vya soda, na hela iliyopatikana, aliiwekeza kwa kufuata mwongozo wa vitabu alivyovisoma.

Mtanzania wa leo mwenye umri wa miaka kumi na sita akipewa milioni moja atafanyia nini? Kufikia huo umri, Warren alikuwa ameshanunua shamba lake binafsi kwa hela yake binafsi aliyoipata baada ya kufanyia kazi maarifa aliyojipatia kwa njia ya vitabu.

Hata alipoanza kupata hela nyingi, bado aliendelea kuwa makini sana na kila senti anayoipata. Ndiyo maana kuna wakati alikuwa na suti moja tu na shati moja jeupe, ambalo mara nyingi lilikuwa likifuliwa kwenye kola tu na pindo za mikononi.

Si kwamba alikuwa hapendi mavazi, hapana. Alikuwa "mbahili" ili aweze kutimiza ndoto zake, na alifanikiwa.
Ili kufikia hatua ya utajiri, heshima ya pesa inahitajika sana.. Tofauti na hapo tutaishia kupata hela kula tu.
 
Njoo gombea mkuu! Una kura yangu na ya maelfu ya wana familia ya JF.

Tunataka viongozi wenye "macho" yanayoona.

"Macho" yako yanaona vizuri. Nafasi yako iko wazi. Njoo!
Nashukuru sana mkuu ingawa serikali imetutenga na kutuita Diaspora tusio na haki ila ipo siku watatupa haki yetu maana hata mirathi tumesamehe eti hatuna haki nayo. Nyie sawa tu 😄
 
Bilionea namba 5 duniani kwa mujibu wa jarida la Forbes, Warren Buffett baada ya mwanahisa mwenzake ndani ya kampuni ya ''Berkshire Hathaway'' Bwana Charlie Munger kutangulia mbele ya haki 28/11/2023

Kwenye jarida la Fortune Magazine, linaeleza kuwa kwenye barua iliyochapishwa na kampuni ya ''Berkshire Hathaway'' liliandika kuhusu uamuzi ambao uliazimiwa na familia hiyo tangu mwaka 2006 kuhusiana na kugawa mali za bilionea huyo kwa masikini.

Uamuzi ambao ulijadiliwa tena November mwaka huu pamoja na watoto wake watatu ambao wanakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 65 - 70, ni kuhusu kugawa asilimia 99 ya utajiri wa Bilionea huyo kwa familia masikini na watoto wake kuhakikisha hilo linafanyika kwa usimamizi wao.

Hapa kwetu Africa lini tutafikia hii hatua?, Au tuendelee kusindikiza dunia? 🥴🥴

Chanzo: Fortune Magazine.
Mali za mikataba hizo za wale jamaa!!

Hakuna tajiri was america ambae sio member was society ile!!

Ukifanya mema walau adhabu ya kuzimu au akhera utapunguziwa japo ni kweli.kwamba wewe ni WA kuzimu na motoni milele!!
 
Akifa atakuwa hana thamani nazo ndo maana anataka zitoke, angekuwa mtoaji kweli angetoa 50% sasa hivi badala 99% akifa
Humjui Buffett wewe. Tangu 2006 mpaka sasa alishagawa utajiri wa zaidi ya dola bilioni 50 kwenye mashirika ya watoto, maskini na miradi ya kijamii. Hiyo ni zaidi ya trilioni 125 za kibongo.
Anachofanya ni kupunguza kidogo kidogo na akifa ndio wagawe kabisa kilichobaki.
 
Kwanini urithi?

Kwanini atoe akifa...

Atoe sasa akiwa hai, sehemu fulani kwa hao wahitaji...

Kwa tunaoamini Mungu, tumeambiwa tutoe sadaka kwa wahitaji...

Ikiwa na maana tukiwa hai sio wafu...
Buffet na matajiri wengi wakubwa u aowajua wewe wametoa sana mali zao kusaidia watu na mpaka wanna foundation mtu Kama Buffet ana foundation kabisa ameshasaidia ma Billions hadi umri huo ila hapa leo tunazungumzia URITHI kwenye urithi kaamua hivyo...Mosi.

Pili, hizo Mali zipo in trwm of share ya Kampuni yake ya Barkshare inaamana yeye kumiliki huo utajiri hadi sasa ni inamaanisha anarndeleza shughuri za Biashara ambyo apart from kumpa utaji ndio purpose yake, passion na Icon so kurithisha kabla ya kufa inamaanisha ni kijiondoa kwenye Biashara ambayo ndio passion na purpose yake.
 
Uamuzi ambao ulijadiliwa tena November mwaka huu pamoja na watoto wake watatu ambao wanakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 65 - 70, ni kuhusu kugawa asilimia 99 ya utajiri wa Bilionea huyo kwa familia masikini na watoto wake kuhakikisha hilo linafanyika kwa usimamizi wao.
Watoto wasimamie ugawaji kama baba yao alivyousia.
 
Mali za mikataba hizo za wale jamaa!!

Hakuna tajiri was america ambae sio member was society ile!!

Ukifanya mema walau adhabu ya kuzimu au akhera utapunguziwa japo ni kweli.kwamba wewe ni WA kuzimu na motoni milele!!
Mjinga mwengine huyu hapa....hafu naye ana ndoto za kuja kuwa president
 
Back
Top Bottom