Bilioni 286 kujenga uwanja Mpya wa 'Samia Suluhu Hassan Arusha Stadium' Kwa ajili ya AFCON 2027

Bilioni 286 kujenga uwanja Mpya wa 'Samia Suluhu Hassan Arusha Stadium' Kwa ajili ya AFCON 2027

Serikali imeingia mkataba wa kuanza Ujenzi wa uwanja Mpya Jijini Arusha Maarufu kama Samia Suluhu Hassan Stadium ambao ni Mahsusi Kwa Ajili ya Maandalizi ya AFCON 2027.

Uwanja huo utagharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 286.

Kazi iendelee 👇👇

View: https://youtu.be/q05ytnyfpa0?si=jLrsYa4X_7tKcjKO

============

Serikali kupitia wizara ya Sanaa ,Utamaduni na Michezo leo Machi 19, 2024 imesaini mkabata wa ujenzi wa Uwanja wa Dokta Samia Suluhu Hassani wenyewe thamani ya shilingi bilioni mia mbili na themanini na Sita ambao utatumika katika michuano ya mataifa Afrika AFCON 2027 inayoandaliwa na nchi za Tanzania, Kenya na Uganda

Akizungumza na waandishi wa habari Waziri wa Michezo Dokta Damasi Ndumbaro amesema Lengo la uwanja huo kujengwa mkoani Arusha ni kuchochea maendeleo ya sekta utalii kupitia michezo.

View attachment 2938864View attachment 2938865View attachment 2938866View attachment 2938989View attachment 2938990

Hivi huu nchi ni ya wanasiasa wa CCM pekee, kwanini kila mradi unapachikwa kuna la mwanasiasa, hatuna vitu vya kujivunia zaidi ya hawa wanasiasa uchwala pamoja na chawa wao?
 
Nimesoma na kusikia kupitia vyombo vya habari kuwa Serikali itajenga uwanja wa mpira utakaogharimu Tshs.286 billion kule Arusha.

Uwanja huu utaingiza jumla ya watu 30,000 kinyume na Uwanja wa Mkapa unaoingiza watu 65,000. Binafsi mimi ninapingana na gharama kubwa ya uwanja huu.

Nitoe mfano Uwanja wa Mkapa ulijengwa kwa takriban T.shs.65 billioni na inachukua watu 65,000 vipi leo uwanja unaochukua watu 30,000 kujengwa kwa Tshs.286 billioni?

Nashauri tuelezwe vitu vya ziada vitakavyokuwemo kwenye uwanja huo zaidi ule wa Mkapa. Pamoja na vitu kupanda bei na shillingi ya Tanzania kushuka dhidi ya dola ya Marekani bado naona gharama hiyo ni ya juu sana.
 
Nimesoma na kusikia kupitia vyombo vya habari kuwa Serikali itajenga uwanja wa mpira utakaogharimu Tshs.286 billion kule Arusha. Uwanja huu utaingiza jumla ya watu 30,000 kinyume na Uwanja wa Mkapa unaoingiza watu 65,000. Binafsi mimi ninapingana na gharama kubwa ya uwanja huu. Nitoe mfano Uwanja wa Mkapa ulijengwa kwa takriban T.shs.65 billioni na inachukua watu 65,000 vipi leo uwanja unaochukua watu 30,000 kujengwa kwa Tshs.286 billioni?. Nashauri tuelezwe vitu vya ziada vitakavyokuwemo kwenye uwanja huo zaidi ule wa Mkapa. Pamoja na vitu kupanda bei na shillingi ya Tanzania kushuka dhidi ya dola ya Marekani bado naona gharama hiyo ni ya juu sana.
Labda kutakuwa na social facilities...
Makumbi..pubs..cinemas..restaurants..rest rooms etc
 
Mwaka gani?
2004,jiulize vitu vimepanda mara 5 tokea mwaka huo hadi sasa?
Tambua uwanja ni mdogo kuliko wa Mkapa.
Tupige hela kwa kiasi wadau,tukifa hatuondoki na chochote,japo mliambiwa mle kulingana na urefu wa kamba.
Inasikitisha sana.
 
We jamaa ludi shule ukadai Ada yako, Pesa pamoja na Vitu hupanda thamani kadri ya Miaka inavyosogea mbele...... hata gari la gharama zaidi la Mwaka 2016 bei yake huwezi linganisha Bei ya Gari la Mwaka 2024 maana thamani ya vitu hupanda.
 
Kwajinsi nilivyomsikiliza mh waziri,niseme tu kunawakati tunatakiwa kuwa na maamuzi magumu sana(magufuli style) ili tusonge mbele.Hao watu waziri anaosema wanaleta ujanja ujanja Arusha wapo wengi sana.Emu fikiria mradi mkubwa kama huo walikuwa wanataka kufanya yao mbele ya waziri bila kuogopa je ni miradi mingapi tusiyoijuwa au watu wangapi waliofanyiwa mambo kama hayo?Ningekuwa mwenye maamuzi muda huu wangekua wako makwao wanachunga mbuzi watendaji wa aina hiyo.Arusha inaitajika kupitia fagio la kuwaondoa watendaji wasiokuwa na nia ya maendeleo bali mambo yao binafsi.
Bil 286 ni fedha nyingi sana kama zingepelekwa kwenye miradi mingine na kusimamiwa kikamilifu,ila kama serikali imeamua kujenga uwanja inabidi kuwa makini sana katika kusimamia fedha hizo ili zifanye kazi husika iliyokusudiwa.
Hao hao mnaowaamini wezi ndiyo hao hao!
 
Tena kwa bei hiyo bado ni ndogo sana Kiwanja cha mpira cha Volkswagen kinachomilikiwa na Timu ya wolfsburg ya ujerumani kinaingiza watu 30,000 na Thamani yake ya ujenzi ilitumia zaidi ya Dola milion 200 ambayo ni sawa na zaidi ya bilioni 400+ za kitanzania.
 
We jamaa ludi shule ukadai Ada yako, Pesa pamoja na Vitu hupanda thamani kadri ya Miaka inavyosogea mbele...... hata gari la gharama zaidi la Mwaka 2016 bei yake huwezi linganisha Bei ya Gari la Mwaka 2024 maana thamani ya vitu hupanda.
Mkuu kuna kupanda kwa gharama,lakini siyo kwa kiwango Cha mara nne au tano.Usihalalishe upigaji na siyo kwamba nakuonea wivu kwasababu labda wewe ni mnufaika labda indirectly au directly.Tena uwanja ni mdogo ukilinganisha na WA Mkapa,inamaana gharama zingejifix kidogo.
Fikiria bei ya cement mwaka 2004 imepanda mara nne hadi sasa kwa mfuko?
Kuna vifaa kama nondo ni bei ndogo kwasasa,inamaana vingefidiwa.Pigeni Kwa kiasi wadau.Mtakufa bila chochote kama sisi,tukikutana huko kama kupo,tutawasema sana.
 
Tena kwa bei hiyo bado ni ndogo sana Kiwanja cha mpira cha Volkswagen kinachomilikiwa na Timu ya wolfsburg ya ujerumani kinaingiza watu 30,000 na Thamani yake ya ujenzi ilitumia zaidi ya Dola milion 200 ambayo ni sawa na zaidi ya bilioni 400+ za kitanzania.
Duuuh! aiseee inamaana unajua gharama ya ujenzi wa nyumba yenye vyumba vitatu pale London ni sawa na ujenzi wa nyumba aina hiyohiyo pale Arusha?
Aisee...
 
Uwanja uitwe Ngorongoro Stadium na siyo vinginevyo. Tuache uchawa.
 
Nimesoma na kusikia kupitia vyombo vya habari kuwa Serikali itajenga uwanja wa mpira utakaogharimu Tshs.286 billion kule Arusha.

Uwanja huu utaingiza jumla ya watu 30,000 kinyume na Uwanja wa Mkapa unaoingiza watu 65,000. Binafsi mimi ninapingana na gharama kubwa ya uwanja huu.

Nitoe mfano Uwanja wa Mkapa ulijengwa kwa takriban T.shs.65 billioni na inachukua watu 65,000 vipi leo uwanja unaochukua watu 30,000 kujengwa kwa Tshs.286 billioni?

Nashauri tuelezwe vitu vya ziada vitakavyokuwemo kwenye uwanja huo zaidi ule wa Mkapa. Pamoja na vitu kupanda bei na shillingi ya Tanzania kushuka dhidi ya dola ya Marekani bado naona gharama hiyo ni ya juu sana.
Elfu tano ya mwaka 1999 ni sawa na elfu tano ya mwaka 2024? ( Miaka 25 baadae)
 
Back
Top Bottom