Bilioni 286 kujenga uwanja Mpya wa 'Samia Suluhu Hassan Arusha Stadium' Kwa ajili ya AFCON 2027

Hivi huu nchi ni ya wanasiasa wa CCM pekee, kwanini kila mradi unapachikwa kuna la mwanasiasa, hatuna vitu vya kujivunia zaidi ya hawa wanasiasa uchwala pamoja na chawa wao?
 
Nimesoma na kusikia kupitia vyombo vya habari kuwa Serikali itajenga uwanja wa mpira utakaogharimu Tshs.286 billion kule Arusha.

Uwanja huu utaingiza jumla ya watu 30,000 kinyume na Uwanja wa Mkapa unaoingiza watu 65,000. Binafsi mimi ninapingana na gharama kubwa ya uwanja huu.

Nitoe mfano Uwanja wa Mkapa ulijengwa kwa takriban T.shs.65 billioni na inachukua watu 65,000 vipi leo uwanja unaochukua watu 30,000 kujengwa kwa Tshs.286 billioni?

Nashauri tuelezwe vitu vya ziada vitakavyokuwemo kwenye uwanja huo zaidi ule wa Mkapa. Pamoja na vitu kupanda bei na shillingi ya Tanzania kushuka dhidi ya dola ya Marekani bado naona gharama hiyo ni ya juu sana.
 
Labda kutakuwa na social facilities...
Makumbi..pubs..cinemas..restaurants..rest rooms etc
 
Mwaka gani?
2004,jiulize vitu vimepanda mara 5 tokea mwaka huo hadi sasa?
Tambua uwanja ni mdogo kuliko wa Mkapa.
Tupige hela kwa kiasi wadau,tukifa hatuondoki na chochote,japo mliambiwa mle kulingana na urefu wa kamba.
Inasikitisha sana.
 
We jamaa ludi shule ukadai Ada yako, Pesa pamoja na Vitu hupanda thamani kadri ya Miaka inavyosogea mbele...... hata gari la gharama zaidi la Mwaka 2016 bei yake huwezi linganisha Bei ya Gari la Mwaka 2024 maana thamani ya vitu hupanda.
 
Hao hao mnaowaamini wezi ndiyo hao hao!
 
Tena kwa bei hiyo bado ni ndogo sana Kiwanja cha mpira cha Volkswagen kinachomilikiwa na Timu ya wolfsburg ya ujerumani kinaingiza watu 30,000 na Thamani yake ya ujenzi ilitumia zaidi ya Dola milion 200 ambayo ni sawa na zaidi ya bilioni 400+ za kitanzania.
 
We jamaa ludi shule ukadai Ada yako, Pesa pamoja na Vitu hupanda thamani kadri ya Miaka inavyosogea mbele...... hata gari la gharama zaidi la Mwaka 2016 bei yake huwezi linganisha Bei ya Gari la Mwaka 2024 maana thamani ya vitu hupanda.
Mkuu kuna kupanda kwa gharama,lakini siyo kwa kiwango Cha mara nne au tano.Usihalalishe upigaji na siyo kwamba nakuonea wivu kwasababu labda wewe ni mnufaika labda indirectly au directly.Tena uwanja ni mdogo ukilinganisha na WA Mkapa,inamaana gharama zingejifix kidogo.
Fikiria bei ya cement mwaka 2004 imepanda mara nne hadi sasa kwa mfuko?
Kuna vifaa kama nondo ni bei ndogo kwasasa,inamaana vingefidiwa.Pigeni Kwa kiasi wadau.Mtakufa bila chochote kama sisi,tukikutana huko kama kupo,tutawasema sana.
 
Duuuh! aiseee inamaana unajua gharama ya ujenzi wa nyumba yenye vyumba vitatu pale London ni sawa na ujenzi wa nyumba aina hiyohiyo pale Arusha?
Aisee...
 
Uwanja uitwe Ngorongoro Stadium na siyo vinginevyo. Tuache uchawa.
 
Elfu tano ya mwaka 1999 ni sawa na elfu tano ya mwaka 2024? ( Miaka 25 baadae)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…