Binadamu: Kiumbe chenye chanzo kisichojulikana, yupoyupo tu hana mwanzo wala mwisho

Binadamu: Kiumbe chenye chanzo kisichojulikana, yupoyupo tu hana mwanzo wala mwisho

Unaposema Mwanadamu " hakuumbwa" Lakini hapo hapo unasema kuwa hakuna ajuaye Mwanadamu kawaje yupo duniani, unajichanganya!!

Mkuu Kama hujui kitu hujui tu

Tatizo lako unalazimisha LAZIMA ijulikane

Tatizo lingine wengi mnafikiria mambo ya zama za kale na kale kwa kutumia fikra za karine hii

Haya maandishi tunayoyatumia sasa ni ya miaka ya karibuni wakati binadamu anastaarabika..... wewe mababu zako wanne tu hapo nyuma walikua hawajui kusoma wala kuandika hadi walipokuja wakoloni
Hata urudi vizazi mia nyuma wanachojua wao ni kwamba walizaliwa na mama zao kama unavyojiona wewe...... then baada ya hapo kama umezaliwa korea utakua buddha, kama umezaliwa Iran utakua mshia kama umezaliwa kwa wa hadzabe ungekuwa unaabudu mapango

Inawezekana tukawa “tumeumbwa” lakini hakuna anayejua

Dhana ya muumbaji kupitia vitabu vya imani vimeshindwa kabisaaaa kuthibitisha uwepo wa muumba zaidi ya kutaka watu waamini tu
 
Wanashangaza sana Hawa Atheists!

Wao wanaamini Kuunda ila hawaamini Kuumba [emoji38].

We are the Image of God

Mungu anaumba

Wanaadamu tuna Unda.

You can't Ignore God the Almighty!

Ni ufinyu wa Kufikiri

Mkuu unablah blah nyingi

Thibitisha uwepo wa huyo muumba

Sisi tunachotaka ni uthibitisho tu sio blah blah
 
Kwani Mungu ni nani/Nini???

Ukisema Mungu yupo ama hayupo bila ya kujua Mungu ni nani/Nini utakuwa unapuyanga tu.

Knowing God should be by default and not by accident of geography and history

Yaani Muumba kaumba dunia hii mamiaka mamilioni lakini babu zako wa majuzi tu vizazi vitatu au vinne walikua hawajui kuhusu Mungu na vitabu vyake hadi wakoloni walipokuja na hivyo vitabu na kuwachukua utumwa......... hivi huwa mnatumia akili gani kuamini huu ujinga mkuu?
 
Anayezungumziwa hapa ni Mungu muumba wa vyote unavyovijua na Usivyovijua!

Tatizo lako unabisha halafu mvivu wa kutafuta maarifa ya kumjua muumba wako.

Nishasema toka mwanzo watu wakafanye research Juu ya Inner Sound na Spirituality/Elimu roho ......utakuja kukaa kimya mwenyewe na utaacha kubwatuka hovyo Mitandaoni humu!

Ndio shida ya waamini Mungu hii
Kwanza mnahakikisha mnamficha mungu asiyekuwepo mahali ambapo hapapo...... ROHONI ndio wapi sasa? [emoji23][emoji23]
 
Knowing God should be by default and not by accident of geography and history

Yaani Muumba kaumba dunia hii mamiaka mamilioni lakini babu zako wa majuzi tu vizazi vitatu au vinne walikua hawajui kuhusu Mungu na vitabu vyake hadi wakoloni walipokuja na hivyo vitabu na kuwachukua utumwa......... hivi huwa mnatumia akili gani kuamini huu ujinga mkuu?
Kwanza siyo kweli kwamba Babu zetu walikuwa hawajui kama Mungu yupo.

Halafu kujua ama kutokukujua hakuondoi uwepo wa Mungu.
 
Kwanza siyo kweli kwamba Babu zetu walikuwa hawajui kama Mungu yupo.

Halafu kujua ama kutokukujua hakuondoi uwepo wa Mungu.

Huu ndio ugumu wa dhana ya mungu

Kuna Mungu wangapi kwani?
Yule Mungu Fundi kapenta wa galilaya ndio Allah? Ndio mungu wa mababu zako walikua wanamuamini kwenye mapango?
 
Huu ndio ugumu wa dhana ya mungu

Kuna Mungu wangapi kwani?
Yule Mungu Fundi kapenta wa galilaya ndio Allah? Ndio mungu wa mababu zako walikua wanamuamini kwenye mapango?
Kwanza dhana ya Mungu haihusishi majina.

Na kwa maelezo yako inaonesha kuwa unaamini Mungu anatakiwa awe mmoja.

Wewe unasema huamini kama Kuna Mungu. Hii nadharia ya kutaka Mungu awe mmoja unaitoa wapi??
 
hata magar yakitazamana saiv jinsi yalivyo mengi barabarani yatakuwa yanasema hivi hivi kuwa sisi (magari) hatuna mwanzo wala mwisho tupo tupo tuu hatueleweki na tutaendelea kuwepo barabarani siku zote ...hayo magar hayajui kuwa kuna gari la kwanza lililo vumbuliwa na kiumbe ambaye ni binadamu..... bila shaka haya magari yatakuwa yanajidanganya tuu pasipokujua aliyeyavumbua (binadamu) akitaka anayatoa barabarani muda wowote na kuyaharibu au kuyatengeneza tena kama atakavoona yeye mwenyewe
Hivyo Kuna mtu amelitengeneza,analitumia Na pia anaweza kuliangamiza Sio!?{ Je mtengenezaji yupo Kwa ajili ya Gari ama Gari lipo kwaajili YA mtengenezaji!?)
 
Hivyo Kuna mtu amelitengeneza,analitumia Na pia anaweza kuliangamiza Sio!?{ Je mtengenezaji yupo Kwa ajili ya Gari ama Gari lipo kwaajili YA mtengenezaji!?)
Kutumia mfano huu Wa gari, kimantiki nadhani hitimisho lake sijui kama litashabihiana na mjadala uliopo.

Mmelipa Gari uhai, fikra na utashi. Lazima mjadala utapotea njia.
 
Kwanza dhana ya Mungu haihusishi majina.

Na kwa maelezo yako inaonesha kuwa unaamini Mungu anatakiwa awe mmoja.

Wewe unasema huamini kama Kuna Mungu. Hii nadharia ya kutaka Mungu awe mmoja unaitoa wapi??
Kwanza Nashukuru kutambua kwamba Mungu ni dhana

Kwahiyo huwa creator wapo wengi kumbe?
Kwa hiyo fundi kapenta labda aliumba pua na kucha, Allah labda akaumba tumbo na miguu, miungu ya mababu zako labda ikaumba makalio na vikojoleo nk nk?

Usitoke nje ya swali lako la msingi......

Mkuu be specific ili tupunguze mjadala...... ni muumba gani exactly unaye MUAMINI wewe ili tujadili uwepo wake
 
Mkuu be specific ili tupunguze mjadala...... ni muumba gani exactly unaye MUAMINI wewe ili tujadili uwepo wake
Bila shaka ni Muumba huyu⤵️

Qur'an, Surah Al-Mulk 67:3
"Aliye umba mbingu saba kwa matabaka. Huoni hitilafu yoyote katika uumbaji wa Mwingi wa Rehema. Hebu rudia kutazama tena! Unaona hitilafu yoyote!?"

" [And] who created seven heavens in layers.[1] You do not see in the creation of the Most Merciful any inconsistency. So return [your] vision [to the sky]; do you see any breaks!?"
 
Kwanza Nashukuru kutambua kwamba Mungu ni dhana

Kwahiyo huwa creator wapo wengi kumbe?
Kwa hiyo fundi kapenta labda aliumba pua na kucha, Allah labda akaumba tumbo na miguu, miungu ya mababu zako labda ikaumba makalio na vikojoleo nk nk?

Usitoke nje ya swali lako la msingi......

Mkuu be specific ili tupunguze mjadala...... ni muumba gani exactly unaye MUAMINI wewe ili tujadili uwepo wake
Nashangaa umeshindwaje kuelewa kuwa Mungu ni dhana na dhana siyo kitu bali ni msingi wa falsafa!!

Maswali yako yanaturudisha kwenye swali langu la msingi. Nani kakwambia kuwa Mungu anatakiwa awe mmoja wakati wewe huamini kuwa kuna Mungu??

Kwa nini unataka kuushusha mjadala Kwa kuleta maswali ya nani kaumba nini kwenye mwili wa Mwanadamu??
 
Unakuta mtu anauliza eti unaamini Muumba gani,...
Wakati ipo wazi kabisa kwamba kama ambavyo lugha zipo tofauti basi hata neno Mungu(Muumba) lipo tofauti kwa Nchi na Jamii tofauti tofauti kutokana na lugha zao, kinacho matter ni Sifa za huyo Muumba.

Mfano kwenye lugha tofauti tofauti Muumba anatamkwa kama ifuatavyo,.... ⤵️
In Spanish, it's "Dios." In Croatian, it's "Bog." In Arabic, it's "الله" (Allah). In Aramaic, it's "ܐܠܗܐ" (Alaha). In Swahili, it's "Mungu." Different languages, but the same concept in each one.
 
hateeb10 nashukuru Kwa ufafanuzi wako.
Nimejaribu kumwelewesha kuwa Mungu ni dhana na siyo kitu au mtu, Lakini Bado haelewi.

Swali la msingi la chanzo cha binadamu ni nini WANALIKWEPA wanaleta mjadala kama Mungu yupo ama hayupo wakati siyo mada ya mjadala huu.
 
Mkuu jibu umepewa kwamba HAIJULIKANI..... sasa kama hujaridhika na hilo jibu njoo na FACTS zako za jibu sahihi tufunge mjadala

Ni matumaini yangu sasa umeanza kupata mwangaza kwamba “mungu” ni “dhana” na sio halisia
Endelea kuuliza maswali tukupe MADINI naamini soon utakuja kubaini jinsi dhana ya mungu ilivyo ya kitapeli
 
Back
Top Bottom