Binadamu: Kiumbe chenye chanzo kisichojulikana, yupoyupo tu hana mwanzo wala mwisho

Binadamu: Kiumbe chenye chanzo kisichojulikana, yupoyupo tu hana mwanzo wala mwisho

Binadamu ni mwanaume na mwanamke.

Utofauti wa binadamu mwanaume na mwanamke hauna aliye uweka.

Upo kama ulivyo.
Unaposema "hakuna" aliyeuweka....Umejuaje haya yote na ukawa na uthibitisho ? tena ukiandika kwa kujiamini ? Tuelezee umejuaje ?
 
Ndio maana nmesema hizo na wewe ni fikra zako tu,

Alafu unamuita ajitokeze kwako ili kujidhihirisha uone kama yupo....Unadhani ni kina joti au Andambile kuwa unamuita vyovyote unavyotaka ?

Kwanza sioni haja ya kubishana kuhusu Mungu, Wewe ambae humuamini endelea kutokumuamini mimi ninaemuamini ntaendelea kumuamini full stop.
Hukatazwi kuamini Mungu wako huyo yupo, Huo ni uhuru wako wa kikatiba kufanya hivyo.

Lakini Mungu huyo hawezi na Kashindwa kufanya binadamu wote wamwamini yeye kwa vile uwezo huo hana na Mungu huyo Hayupo.
 
Unaposema "hakuna" aliyeuweka....Umejuaje haya yote na ukawa na uthibitisho ?
Kwa vile hajawahi kuwepo, hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.

Kama unajua yupo ungethibitisha kwamba yupo.

Na angefahamika yupo, ila mpaka sasa hakuna uthibitisho wowote wa uwepo wake.

Zaidi ya mawazo ya kufikirika tu.
tena ukiandika kwa kujiamini ? Tuelezee umejuaje ?
 
Infropreneur ni mtu makini sana, hakili yake inachakata kama mashine kwa kujibu swali na kulidadisi na kulihoji bila kufata mkumbo, ndo mtu bora kabisa hili badiko, nimefutiwa sana na yeye msimamo wake, ambacho hakipo kiuhalisia, nimejifunza sana kwake.
 
Hukatazwi kuamini Mungu wako huyo yupo, Huo ni uhuru wako wa kikatiba kufanya hivyo.

Lakini Mungu huyo hawezi na Kashindwa kufanya binadamu wote wamwamini yeye kwa vile uwezo huo hana na Mungu huyo Hayupo.
Kwako na kwa wasioamini ni kweli hayupo sikupingi,

Ila kwa sisi waamini YUPO.
 
Infropreneur ni mtu makini sana, hakili yake inachakata kama mashine kwa kujibu swali na kulidadisi na kulihoji bila kufata mkumbo, ndo mtu bora kabisa hili badiko, nimefutiwa sana na yeye msimamo wake, ambacho hakipo kiuhalisia, nimejifunza sana kwake.
Majibu yake mengi hayajikamilishi, Ukimuuliza swali anauliza swali ndani ya swali ulilouliza...Yani anatengeneza mazingira ya kukwepa maswali magumu kwake..

Rudi umfuatilie upya.
 
Kwa vile hajawahi kuwepo, hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.

Kama unajua yupo ungethibitisha kwamba yupo.

Na angefahamika yupo, ila mpaka sasa hakuna uthibitisho wowote wa uwepo wake.

Zaidi ya mawazo ya kufikirika tu.
Hujajibu swali linavyotakiwa kama kawaida yako, Nmeuliza umejuaje kuwa hayupo ? Na una uthibitisho gani ?

Umetumia kanuni gani kujua kuwa hayupo ? Nijibu direct bila kupindisha pindisha
 
Hujajibu swali linavyotakiwa kama kawaida yako, Nmeuliza umejuaje kuwa hayupo ? Na una uthibitisho gani ?

Umetumia kanuni gani kujua kuwa hayupo ? Nijibu direct bila kupindisha pindisha
Zaidi ya mwezi Sasa Infropreneur hajajibu swali lako hili...

Au chanzo kisicho na chanzo kimeshamtwaa!!!???
 
ikiwa sayansi ina amini katika homoni kitu ambacho untangable why me,nisiamini katika mungu?
Wapinga nadharia ya uwepo wa MUNGU wanasema kuwa hata sayansi nayo haiaminiki kwa 100%.

Hata kama wao wanatumia nadharia hizo hizo za kisayansi kupinga uwepo wa MUNGU.
 
Hili jambo la kujua mungu yupo au hayupo, si la kumlaumu mtu akisema mungu yupo au hayupo, ni sawa tu hii dunia tunaishi kwa utabiri tu sisi binadamu, ukweli pekee nauhasia na vitendo hatunao, kuhusu binadamu na dunia ilikuaje kuaje ikawa hivi mwenye jibu kamili hakuna, imani, na dini ni nyingi na zinapigana.
 
Mimi nataka kusema tu kuwa mungu hatuwezi kumjua,zaidi ya yale aliyoamua kutujulisha kuhusu yeye, na tunayoyaona na kuyasikia,nataka mjue kila kitu kina mtawala wake sasa nyinyi mkijikuta mnataka kupambana na mtawala wenu maana yake, hamko salama kifikra ,utake kumchimba mungu aliyekuumba na kutaka kumjua zaidi ya uwezo wako!! Utakosa majibu na utaishia pabaya na hiyo n roho ya uasi.
 
Hisia za uchungu na furaha Kwa binadamu zimezukaje zukaje??

Leo wanasimba wanauchungu Wa kufungwa, jee furaha yao imeondokaje!?
 
Mimi nataka kusema tu kuwa mungu hatuwezi kumjua,zaidi ya yale aliyoamua kutujulisha kuhusu yeye, na tunayoyaona na kuyasikia,nataka mjue kila kitu kina mtawala wake sasa nyinyi mkijikuta mnataka kupambana na mtawala wenu maana yake, hamko salama kifikra ,utake kumchimba mungu aliyekuumba na kutaka kumjua zaidi ya uwezo wako!! Utakosa majibu na utaishia pabaya na hiyo n roho ya uasi.
Imebadilika ujinga
 
Hujajibu swali linavyotakiwa kama kawaida yako, Nmeuliza umejuaje kuwa hayupo ? Na una uthibitisho gani ?

Umetumia kanuni gani kujua kuwa hayupo ? Nijibu direct bila kupindisha pindisha
Unathibitishaje kitu ambacho hakipo? Kitu kinachothibitishwa ni kile ambacho kipo, hauwezi kuthibitisha uwepo wa kitu ambacho hakipo.
 
Kuwepo kwa kitu kuthibitishwa kwake kanuni yake ni ipi??
Chief, anayesema kitu fulani hakipo hana cha kuthibitisha. Anayetakiwa kuthibitisha ni anayesema kitu fulani kipo, hii ni logic ya kawaida. Kanuni ya kuthibitisha ni kuonyesha, unaonyesha vipi kitu ambacho hakipo!?
Usijichanganye, mimi sipo kwenye kupinga au kukataa uwepo wa Mungu, lakini nikimuambia mtu Mungu yupo, natakiwa nimthibitishie huyo mtu kuwa Mungu yupo. Mtu akiniambia Mungu hayupo, wala hatakiwi kunithibitishia kuwa hayupo ila mimi kama ninajua yupo na ninahitaji ajue kuwa yupo, basi nitatakiwa kumuonesha uwepo wa Mungu, maana ya kuthibitisha inatakiwa kufanya kazi hapa na sio vinginevyo.
 
George Betram kwanza Ili utafute kitu si Lazima kuwe na kanuni ya kufuata?

Kwa mfano 2+2=4

Lakini mfano 2-2=0

Na mfano 2x2=4

Na mwisho 2÷2=0.

Ukiangalia kirahisi hapo juu ni kama kulikuwa hakuna haja ya kutumia kanuni zote nne za kihisabati kwani majibu ni kama yanafanana yaani 4 na 0.

Lakini Kila kanuni huwa na kanuni ya ya muendelezo ndani mwake. Kwa ivo kwenye kujua uwepo wa MUNGU ni lazima kanuni ya kimungu itumike.

Ukikataa kutumia kanuni ya kimungu kumtafuta Mungu huwezi kumpata Mungu!!
 
Back
Top Bottom