Binafsi Bado nina imani na Rais Samia kutuletea Tanzania iliyo bora zaidi

Binafsi Bado nina imani na Rais Samia kutuletea Tanzania iliyo bora zaidi

Rasterman

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2015
Posts
33,894
Reaction score
44,117
Ndugu zangu pamoja na mambo mengi yaliyopita tangu Tupate uhuru ni wazi kuwa kwa sehemu fulani Rais Samia amekuwa Rais Bora miongoni mwa waliokuwa bora.

Hili linakuja kutokana na mchango wake mkubwa hasa ktk kuleta ajira, na kuongeza fedha ktk mzunguko wa miradi ya kitaifa. Kama miradi hiyo itaketa faida au la ni jambo lingine. Kama itakamilika kwa wakati au la ni mjadala mwingine.

Lakini pia nasikia kuna maridhiano yanaendelea (hatuna uhakika maana hatujatangaziwa), hili pekee kama linaendelea ni dalili njema ya kuipata Tanzania tuitakayo.

Ofcourse, mtu mwenye njaa ya hitajio la jambo fulani ataona kama muda unachelewa lakini kila lenye heri lahitaji kuvuta subira.

Naamini kinachoendelea kiko katika nia njema na muda ndio utaongea.

Hongera Rais Samia na wadau woote wanaosongesha Nchi katika mwelekeo sahihi.
 
Ndugu zangu pamoja na mambo mengi yaliyopita tangu Tupate uhuru ni wazi kuwa kwa sehemu fulani Rais Samia amekuwa Rais Bora miongoni mwa waliokuwa bora.
Tuendelee kumpa Muda Rais ajipange sawa sawa
 
Mambo mazuri yanakuja vuta subira.

Yale wanayohitaji Wapinzani ndio hayo hayo wanahitaji watanzania
Umejibu kwa kwa busara ya Hali ya juu Sana Bila kejeli wala kumuumiza mwingine asiye muumini wa kile unachoamini. Hongera Kaka
 
Mimi namuona Raisi Samia kama Raisi mwanamageuzi, itaji la vijana ni ukuaji wa uchumi, kwa kuipa uhuru sekta binafsi kuwekeza na kufanya biashara, na ili ndilo analolipigania, kama akifanikiwa kwa haraka basi ajira na vibarua vitaongezeka, mzunguko wa hela utakuepo kwa kiasi fulani, vijana wataweza kujiajiri kwa kuzunguka uku na huko kutafuta fursa. Namuona pia kama Raisi asiependa ubabe wa kisiasa, namuombea atembee katika haki kwa vyama vya kisiasa.
 
Umejibu kwa kwa busara ya Hali ya juu Sana Bila kejeli wala kumuumiza mwingine asiye muumini wa kile unachoamini. Hongera Kaka
Kabisa kabisa Mkuu.
Nchi ni yetu sote kwa nini tuumizane kihisia bila sababu?
 
Mimi namuona Raisi Samia kama Raisi mwanamageuzi, itaji la vijana ni ukuaji wa uchumi, kwa kuipa uhuru sekta binafsi kuwekeza na kufanya biashara...
Kabisa kabisa na sisi wengine tunaendelea kumwombea mafanikio.

Mafanikio yake ni mafanikio yetu. Mungu amsimamie
 
Rubbish, toka ameingia madarakani ameanzisha mradi gani mkubwa zaidi ya hii ya marehemu na imemshinda ?
 
Kweli mitazamo inayofanana, mimi namuomba kama wengineo waliomtangulia ambao nao walisema kama huyu kwamba wangetuvusha.
Badala yake wametuangusha na wakutuinua bado hajapatikana maana wote ni wale wale tu wanatofautiana majina tu.
Upo sahihi huyu ni mbovu kuwahi kutokea akipewa tuzo za mchongo anajiona ni kiongozi bora kumbe ni bure kabisa
 
Kweli mitazamo inayofanana, mimi namuomba kama wengineo waliomtangulia ambao nao walisema kama huyu kwamba wangetuvusha.
Badala yake wametuangusha na wakutuinua bado hajapatikana maana wote ni wale wale tu wanatofautiana majina tu.
Ni kweli kama unavyosema watanzania wengi wamekata tamaa kutokana na uzoefu kama ulivyoeleza. Lakini pia ni vizuri kuto generalize maana ya Mungu ni mengi.
 
B

Bwana Benjamini wewe ulitaka aanzieshe mipya wakati hata iliyopo haijaisha? Let us be fair.
Mwenzake alipoingia pamoja na kwamba alikuwa dikteta lakini ndani ya miezi 4 alishaanzisha miradi kibao huyo hata mmoja labda kwa upande wa kwao Zanzibar.
 
Kweli mitazamo inayofanana, mimi namuomba kama wengineo waliomtangulia ambao nao walisema kama huyu kwamba wangetuvusha.
Badala yake wametuangusha na wakutuinua bado hajapatikana maana wote ni wale wale tu wanatofautiana majina tu.
Kabisa mkuuu
Chama cha mambuzi ni lazima wafe wote kwanza. Hakuna mtu pale katika kile chama mwenye dhamira ya kuleta mageuzi yenye tija. Ni mambo ya zimamoto na kucheza na akili za wadanganyika. Imeisha hiyo.
 
Back
Top Bottom